《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼

页码:close

external-link copy
109 : 3

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرۡجَعُ ٱلۡأُمُورُ

Na kila kilichomo Mbinguni na kilichomo Ardhini ni cha Mwenyezi Mungu; na mambo yote yatarejea kwa Mwenyezi Mungu. info

Na vyote viliomo Mbinguni na Ardhini ni vya Mwenyezi Mungu peke yake, ni vyake kwa kuviumba, na kuvimiliki, na kuvisarifu. Na marejeo ya mambo yao ni kwake Yeye. Kwa hivyo humlipa kila mmoja kama anavyo stahiki.

التفاسير:

external-link copy
110 : 3

كُنتُمۡ خَيۡرَ أُمَّةٍ أُخۡرِجَتۡ لِلنَّاسِ تَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَتَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَتُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِۗ وَلَوۡ ءَامَنَ أَهۡلُ ٱلۡكِتَٰبِ لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۚ مِّنۡهُمُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَأَكۡثَرُهُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu. info

Nyinyi Umma wa Muhammad ni bora ya umati alio umba Mwenyezi Mungu kwa manufaa ya watu, maadamu mtaamrisha ut'iifu na mtakataza maasi, na mtakuwa ni wenye kumuamini Mwenyezi Mungu kwa Imani safi na ya kweli. Na lau kuwa Watu wa Kitabu wangeli kuwa ni wakweli katika imani yao kama nyinyi, basi ingeli kuwa ni bora kwao kuliko walivyo. Walakini baadhi yao ni Waumini, na wengi wao wameikiuka mipaka ya Imani na yanayo pasa.

التفاسير:

external-link copy
111 : 3

لَن يَضُرُّوكُمۡ إِلَّآ أَذٗىۖ وَإِن يُقَٰتِلُوكُمۡ يُوَلُّوكُمُ ٱلۡأَدۡبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ

Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa. info

Hao wapotovu hawawezi kukudhuruni nyinyi kama walivyo kuandalieni, wala hawakuathirini. Ijapo kuwa mtapata maudhi kwao, lakini athari yake haiselelei. Na hata wakipigana nanyi wataingia kiwewe wakimbie wasipambane nanyi, na hapo mwishoe hawatopata ushindi juu yenu maadamu nyinyi mtashikamana na kuamrisha mema na kukataza maovu.

التفاسير:

external-link copy
112 : 3

ضُرِبَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلذِّلَّةُ أَيۡنَ مَا ثُقِفُوٓاْ إِلَّا بِحَبۡلٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَحَبۡلٖ مِّنَ ٱلنَّاسِ وَبَآءُو بِغَضَبٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَضُرِبَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلۡمَسۡكَنَةُۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَانُواْ يَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَيَقۡتُلُونَ ٱلۡأَنۢبِيَآءَ بِغَيۡرِ حَقّٖۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَواْ وَّكَانُواْ يَعۡتَدُونَ

Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu. Na wakastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na wamepigwa na unyonge. Hayo ni kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakiwauwa Manabii pasina haki; hayo ni kwa sababu waliasi na walikuwa wakiruka mipaka. info

Na Mwenyewe Subhana ameeleza kuwa lazima watapata madhila popote watapo kutikana, ila wakifungamana kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu na ahadi ya Waislamu. Na wao wamestahiki wapate ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pia Mwenyezi Mungu amewajaalia lazima uwafikie unyonge na unyenyekevu kwa wengineo. Na hayo ni kwa sababu ya kukataa kwao Ishara zote za Mwenyezi Mungu zinazo onyesha Unabii wa Muhammad s.a.w. na vile kuridhi kwao hapo zamani kuuliwa Manabii ambako hakuwezi kuwa ni kwa haki, bali ni kwa uasi wao na uadui wao.

التفاسير:

external-link copy
113 : 3

۞ لَيۡسُواْ سَوَآءٗۗ مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ أُمَّةٞ قَآئِمَةٞ يَتۡلُونَ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ ءَانَآءَ ٱلَّيۡلِ وَهُمۡ يَسۡجُدُونَ

Wote hao si sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo watu walio simama baraabara, wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia wanasujudu. info

Watu wa Kitabu si wote sawa sawa. Miongoni mwao wapo walio simama msimamo mwema, wa uadilifu, wanakisoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu nyakati za usiku wakiswali.

التفاسير:

external-link copy
114 : 3

يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَيَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَيُسَٰرِعُونَ فِي ٱلۡخَيۡرَٰتِۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanakimbilia katika mambo ya kheri. Na hao ndio miongoni mwa watenda mema. info

Wanaamini kweli kuwepo Mwenyezi Mungu, na kuwa Yeye ni Mmoja tu. Wanaamini Mitume wote, hawamuabudu ila Mwenyezi Mungu. Na wanaamini kuwa itafika Siku ya Kiyama; wanaamrisha ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu, na wanakataza maasi, na wanawania kutenda mambo ya kheri. Hawa kwa Mwenyezi Mungu huhisabiwa miongoni mwa watenda wema.

التفاسير:

external-link copy
115 : 3

وَمَا يَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَلَن يُكۡفَرُوهُۗ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِٱلۡمُتَّقِينَ

Na kheri yoyote wanayo ifanya hawatanyimwa malipwa yake. Na Mwenyezi Mungu anawajua wachamngu. info

Kheri yoyote wanayo ifanya watu hao hawatonyimwa thawabu zake. Na Mwenyezi Mungu amezizunguka kwa kuzijua na kuziweza hali zao na malipo yao.

التفاسير: