《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼

页码:close

external-link copy
92 : 3

لَن تَنَالُواْ ٱلۡبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُواْ مِمَّا تُحِبُّونَۚ وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَيۡءٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٞ

KABISA HAMTAFIKIA wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda. Na kitu chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua. info

Enyi Waumini! Hamtoipata kheri kaamili mnayo itaka na itakayo mridhisha Mwenyezi Mungu ila mkitoa katika vitu mnavyo vipenda na mkatoa katika Sabili Llahi, Njia ya Mwenyezi Mungu, kwa namna mbali mbali. Na chochote mnacho kitoa, kidogo na kikubwa, kilio bora au chenginecho, Mwenyezi Mungu anakijua. Kwani Yeye ni Mwenye Kujua, hapana kitu kilioko mbinguni au duniani kinacho fichikana naye.

التفاسير:

external-link copy
93 : 3

۞ كُلُّ ٱلطَّعَامِ كَانَ حِلّٗا لِّبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِلَّا مَا حَرَّمَ إِسۡرَٰٓءِيلُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ مِن قَبۡلِ أَن تُنَزَّلَ ٱلتَّوۡرَىٰةُۚ قُلۡ فَأۡتُواْ بِٱلتَّوۡرَىٰةِ فَٱتۡلُوهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Kila chakula kilikuwa halali kwa Wana wa Israili isipo kuwa alicho jizuilia Israili mwenyewe kabla haijateremshwa Taurati. Sema: Leteni Taurati muisome ikiwa nyinyi ni wasema kweli. info

Mayahudi waliwatoa kombo Waislamu kwa kuhalalisha baadhi ya vyakula kama nyama ya ngamia na maziwa yake. Wakadai kuwa hayo yaliharimishwa na sharia ya Ibrahim. Mwenyezi Mungu Subhanahu aliwarudi madai yao hayo kwa kubainisha kuwa vyakula vyote vilikuwa halali kwa Wana wa Yaakub (ndiye Israil) kabla ya kuteremka Taurati, ila alicho jizuia Yaakub mwenyewe kwa sababu zilizo mkhusu yeye tu, basi na wao wakijiharimishia nafsi zao. Mwenyezi Mungu akamuamrisha Nabii wake awatake walete uthibitisho wa Taurati kuwa sharia ya Ibrahim imeharimisha hayo kama wao wanasema kweli. Wakashindwa, wakanywea.

التفاسير:

external-link copy
94 : 3

فَمَنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Na wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu baada ya hayo, basi hao ndio madhaalimu. info

Ilipo thibiti kuwa wameemewa basi wenye kumsingizia uwongo Mwenyezi Mungu baada ya hoja hizo, hao ndio walio selelea na udhaalimu wao, na wanastahiki kuitwa Madhaalimu.

التفاسير:

external-link copy
95 : 3

قُلۡ صَدَقَ ٱللَّهُۗ فَٱتَّبِعُواْ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Sema: Mwenyezi Mungu amesema kweli. Basi fuateni mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. info

Baada ya kushindwa kwao Mwenyezi Mungu amemuamrisha Nabii wake awabainishie kuwa ukweli wa Mwenyezi Mungu umethibiti katika ayasemayo. Basi ifuateni Sharia ya Ibrahim anayo kutakeni muifuate, na nyinyi mnaikanusha. Hii ni mbali kabisa na hizo Dini za uwongo, kwani Ibrahim hakuwa miongoni mwa washirikina.

التفاسير:

external-link copy
96 : 3

إِنَّ أَوَّلَ بَيۡتٖ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكٗا وَهُدٗى لِّلۡعَٰلَمِينَ

Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, (Makka) iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote. info

Katika kufuata mila ya Ibrahim ni kuelekea wakati wa Swala Nyumba aliyo ijenga, na kwenda kuhiji huko. Mwenyezi Mungu amebainisha hayo kwa kusema: Hakika Nyumba ya awali kwa ukongwe na utukufu aliyo ijaalia Mwenyezi Mungu iwe ni ya ibada kwa watu ni hiyo iliyoko Makka (au Bakka kama pia inavyoitwa). Nayo ina kheri nyingi na manufaa, na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ameijaalia iwe na baraka. Nayo Nyumba hiyo ni pahali pa uwongofu kwa watu kwa kuhiji na kuelekea wakati wa Swala.

التفاسير:

external-link copy
97 : 3

فِيهِ ءَايَٰتُۢ بَيِّنَٰتٞ مَّقَامُ إِبۡرَٰهِيمَۖ وَمَن دَخَلَهُۥ كَانَ ءَامِنٗاۗ وَلِلَّهِ عَلَى ٱلنَّاسِ حِجُّ ٱلۡبَيۡتِ مَنِ ٱسۡتَطَاعَ إِلَيۡهِ سَبِيلٗاۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِيٌّ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu. info

Zipo dalili wazi za kuonyesha utakatifu wake huo Msikiti wa Makka na kuzidi fadhila zake. Miongoni mwa hizo ni hapo alipo kuwa akisimama Nabii Ibrahim a.s. kwa kuswali. Na pia kuwa anaye ingia humo huwa amesalimika halimpati ovu. Na kuhiji Makka ni waajibu wa kila mtu awezae kwenda. Na mwenye kukataa, akaiasi amri ya Mwenyezi Mungu, na akaipinga Dini yake, basi khasara itamuangukia mwenyewe, na Mwenyezi Mungu anajitosha, hawahitajii watu wote.

التفاسير:

external-link copy
98 : 3

قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعۡمَلُونَ

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnakanusha ishara za Mwenyezi Mungu, na ilhali kuwa Mwenyezi Mungu ni Shahidi kwa yote mnayo yatenda? info

Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la amemuamrisha Mtume wake awahizi Watu wa Kitabu kwa kuendelea kwao kukufuru na kupotoka na kupotosha, akasema: Enyi Watu wa Kitabu! Huo ukafiri wenu hauna sura wala maana. Kwa sababu gani mnakanusha dalili, na hoja za Mwenyezi Mungu zenye kuthibitisha Unabii na Ukweli wa Muhammad? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuvijua vitendo vyenu na atakulipeni malipo yake.

التفاسير:

external-link copy
99 : 3

قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ مَنۡ ءَامَنَ تَبۡغُونَهَا عِوَجٗا وَأَنتُمۡ شُهَدَآءُۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnamzuilia aliye amini Njia ya Mwenyezi Mungu mkiitafutia kosa, na hali nyinyi mnashuhudia? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yatenda. info

Enyi Watu wa Kitabu! Vipi mnajaribu kumgeuza mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kuifuata Haki aache Njia Iliyo Nyooka ya Mwenyezi Mungu wa Kweli, na mnajaribu kuikosoa Njia hiyo, na nyinyi mnajua kuwa hiyo ndiyo Haki? Wala Mwenyezi Mungu hakughafilika na vitendo vyenu, naye atakulipeni kwavyo.

التفاسير:

external-link copy
100 : 3

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تُطِيعُواْ فَرِيقٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ يَرُدُّوكُم بَعۡدَ إِيمَٰنِكُمۡ كَٰفِرِينَ

Enyi mlio amini! Mkiwat'ii baadhi ya walio pewa Kitabu watakurudisheni kuwa makafiri baada ya Imani yenu. info

Mwenyezi Mungu anawahadharisha Waumini na vitimbi vya baadhi ya Watu wa Kitabu,(Mayahudi na Wakristo), vya uchochezi wao wa udanganyifu kwa kusema: Mkiwat'ii baadhi ya Watu wa Kitabu katika yale wanayo yaeneza ya kutilisha shaka katika Dini yenu, itakuwa mnarajea tena kwenye upotovu baada ya uwongofu, na wakurejezeni muwe makafiri baada ya kuwa ni Waumini.

التفاسير: