Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
62 : 2

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱلَّذِينَ هَادُواْ وَٱلنَّصَٰرَىٰ وَٱلصَّٰبِـِٔينَ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَلَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Hakika Waumini wa ummah huu waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake na wakatekeleza Sheria Yake, na wale waliokuwa kabla ya kutumilizwa Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, miongoni mwa ummah waliopita katika Mayahudi, Wanaswara na Wasabai (Sābiūn), nao ni watu walioko kwenye tabia za maumbile na hawana dini maalumu wanayoifuata, wote hawa wakimuamini Mwenyezi Mungu, imani ya sawa iliyotakasika, wakaiamini Siku ya kufufuliwa na Malipo na wakafanya amali zenye kumridhi Mwenyezi Mungu, basi thawabu zao zimethibiti kwa Mola wao. Wao hawatakuwa na khofu juu ya mambo yao ya Akhera ambayo wao watayakabili. Na wala wao hawatahuzunika juu ya mambo ya dunia waliyoyakosa. Ama baada ya kutumilizwa Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie yeye, kuwa ni mwisho wa Manabii na Mitume, kwa watu wote, Mwenyezi Mungu Hatakubali dini, kwa yoyote, isipokuwa ile aliyokuja nayo ambayo ni Uislamu. info
التفاسير:

external-link copy
63 : 2

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَكُمۡ وَرَفَعۡنَا فَوۡقَكُمُ ٱلطُّورَ خُذُواْ مَآ ءَاتَيۡنَٰكُم بِقُوَّةٖ وَٱذۡكُرُواْ مَا فِيهِ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ

Na kumbukeni, enyi Wana wa Isrāīl, tulipochukua kutoka kwenu ahadi ya mkazo ya kumuamini Mwenyezi Mungu na kumpwekesha kwa ibada, na tukaliinua jabali la Tūr juu yenu na tukawaambia, “Chukueni, kwa bidii na jitihadi, Kitabu tulichowapa na mkitunze. Na mkitofanya hivyo, tutaliangusha hili jabali juu yenu liwafinike, na msiisahau Taurati kwa maneno na vitendo, mpate kunicha na kuiogopa adhabu Yangu.” info
التفاسير:

external-link copy
64 : 2

ثُمَّ تَوَلَّيۡتُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَۖ فَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ لَكُنتُم مِّنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Kisha mlienda kinyume na mkaasi mara nyingine, baada ya kuchukuwa ahadi ya mkazo na kunyanyuliwa jabali, kama desturi yenu daima. Na lau si wema wa Mwenyezi Mungu na rehema Yake kuikubali toba yenu na kuyasamehe makosa yenu, mungalikuwa ni wenye hasara ya duniani na ya Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
65 : 2

وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلَّذِينَ ٱعۡتَدَوۡاْ مِنكُمۡ فِي ٱلسَّبۡتِ فَقُلۡنَا لَهُمۡ كُونُواْ قِرَدَةً خَٰسِـِٔينَ

Hakika mlijua, enyi kongamano la Mayahudi na Wanaswara, adhabu iliyowapata mababu zenu waliopita, watu wa kijiji kilichoasi amri ya Mwenyezi Mungu katika yale aliyowachukulia ahadi ya kuitukuza Siku ya Jumamosi. Wakafanya hila ya kuvua samaki siku ya Jumamosi kwa kuweka mitego na kufukua mashimo. Walipofanya hivyo, Mwenyezi Mungu aliwageuza kuwa manyani wenye kudharauliwa. info
التفاسير:

external-link copy
66 : 2

فَجَعَلۡنَٰهَا نَكَٰلٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهَا وَمَا خَلۡفَهَا وَمَوۡعِظَةٗ لِّلۡمُتَّقِينَ

Tukakifanya kijiji hicho ni mazingatio kwa watu wa vijiji vya karibu ambao itawafikia habari yake na vituko vilivyotokea huko, na ni mazingatio kwa mwenye kufanya madhambi kama hayo baada yake. Na pia tulikifanya ni mawaidha kwa watu wema, wapate kujua kuwa wao wako kwenye haki, ili wasimame imara juu yake. info
التفاسير:

external-link copy
67 : 2

وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦٓ إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُكُمۡ أَن تَذۡبَحُواْ بَقَرَةٗۖ قَالُوٓاْ أَتَتَّخِذُنَا هُزُوٗاۖ قَالَ أَعُوذُ بِٱللَّهِ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡجَٰهِلِينَ

Na Kumbukeni, enyi wana wa Isrāīl, makosa ya mababu zenu, ushindani wao mwingi na kujadiliana kwao na Mūsā, rehema na amani zimshukie, pindi alipowaambia, “Hakika Mwenyezi Mungu Anawaamuru mchinje ng’ombe.” Wakasema, wakiwa na kiburi, “Unatufanyia mzaha na kutuchezea?” Mūsā akawajibu, “Ninajilinda kwa Mwenyezi Mungu nisiwe ni miongoni mwa wanaofanya stihizai.” info
التفاسير:

external-link copy
68 : 2

قَالُواْ ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَۚ قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٞ لَّا فَارِضٞ وَلَا بِكۡرٌ عَوَانُۢ بَيۡنَ ذَٰلِكَۖ فَٱفۡعَلُواْ مَا تُؤۡمَرُونَ

Walisema, “Tuombee Mola wako atufafanulie sifa ya ng’ombe huyu.” Akawajibu, “Mwenyezi Mungu Anawaambia kwamba sifa yake ni asiwe mkubwa wa miaka wala mdogo. Yeye ni wa katikati baina ya uzee na ujana, basi fanyeni haraka kutii amri ya Mola wenu.” info
التفاسير:

external-link copy
69 : 2

قَالُواْ ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا لَوۡنُهَاۚ قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٞ صَفۡرَآءُ فَاقِعٞ لَّوۡنُهَا تَسُرُّ ٱلنَّٰظِرِينَ

Wakarudi kwenye kujadili kwao wakisema, “Mwambie Mola wako Atufafanulie rangi yake.” Akasema kuwaambia, “Yeye anasema kwamba huyo ni rangi ya manjano iliyoiva sana, anayemtia furaha mwenye kumwangalia.” info
التفاسير: