Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
275 : 2

ٱلَّذِينَ يَأۡكُلُونَ ٱلرِّبَوٰاْ لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ ٱلَّذِي يَتَخَبَّطُهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ مِنَ ٱلۡمَسِّۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡبَيۡعُ مِثۡلُ ٱلرِّبَوٰاْۗ وَأَحَلَّ ٱللَّهُ ٱلۡبَيۡعَ وَحَرَّمَ ٱلرِّبَوٰاْۚ فَمَن جَآءَهُۥ مَوۡعِظَةٞ مِّن رَّبِّهِۦ فَٱنتَهَىٰ فَلَهُۥ مَا سَلَفَ وَأَمۡرُهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِۖ وَمَنۡ عَادَ فَأُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Wale wenye kuamiliana kwa riba- nayo ni nyongeza juu ya rasilmali-, hawainuki kutoka kwenye makaburi yao Siku ya Mwisho isipokuwa ni kama anavyoinuka yule anayepigwa na Shetani akapatwa na wazimu. Hivo ni kwa kuwa wao walisema kwamba biashara ni kama riba, kwa kuwa yote mawili ni halali na yanapelekea mali kuongezeka. Mwenyezi Mungu Akawakanusha na Akabainisha kwamba Yeye Amehalalisha biashara na Ameharamisha riba. Kwa kuwa katika kuuza na kununua kuna nafuu kwa watu binafsi na kwa jamii na katika riba kuna unyonyaji, hasara na maangamivu. Basi mwenye kumfikia yeye makatazo ya Mwenyezi Mungu ya riba akakomeka, achukue iliyopita kabla ya kumfikia yeye uharamu wake, na hana makosa kwa hilo. Na mambo yake ya siku zake za baadae yako kwa Mwenyezi Mungu. Akiwa ataendelea na toba yake, basi Mwenyezi Mungu Hapotezi malipo ya wenye kufanya wema; na akiwa atarudia kwenye riba, basi kitendo chake hiko baada ya kufikiwa na makatazo ya Mwenyezi Mungu, kitamfanya astahili mateso, kwa kuwa hoja imesimama juu yake. Kwa ajili ya hii Alisema Mwenyezi Mungu, «Basi hao ni watu wa Motoni; Wao ndani yake watakaa milele». info
التفاسير:

external-link copy
276 : 2

يَمۡحَقُ ٱللَّهُ ٱلرِّبَوٰاْ وَيُرۡبِي ٱلصَّدَقَٰتِۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ

Mwenyezi Mungu Anaiyondoa riba yote au Anamnyima mlaji riba baraka ya mali yake asinufaike nayo. Na Anazikuza sadaka na kuzifanya ziwe nyingi na Anawaongezea malipo wenye kutoa sadaka maradufu na Anawabarikia katika mali yao. Na Mwenyezi Mungu Hampendi kila mwenye kushikilia kwenye ukafiri wake, mwenye kujihalalishia ulaji riba, mwenye kukolea nadani ya dhambi na haramu na kumuasi Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
277 : 2

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Hakika wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakatenda matendo mema, wakatekeleza Swala kama Alivyoamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakatoa Zaka za mali yao, wana thawabu kubwa zinazowahusu wao mbele ya Mola wao na Mruzuku wao. Na hawatapatwa na woga katika Akhera yao, wala masikitiko juu ya mambo mazuri ya kilimwengu waliyoyakosa. info
التفاسير:

external-link copy
278 : 2

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَذَرُواْ مَا بَقِيَ مِنَ ٱلرِّبَوٰٓاْ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na mkamfuata Mtume Wake, muogopeni Mwenyezi Mungu na muache kutaka ziada iliyosalia juu ya rasilmali zenu, ambayo mlistahiki kupata kabla riba haijaharamishwa, iwapo imani yenu ni ya kidhati kimaneno na kivitendo. info
التفاسير:

external-link copy
279 : 2

فَإِن لَّمۡ تَفۡعَلُواْ فَأۡذَنُواْ بِحَرۡبٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۖ وَإِن تُبۡتُمۡ فَلَكُمۡ رُءُوسُ أَمۡوَٰلِكُمۡ لَا تَظۡلِمُونَ وَلَا تُظۡلَمُونَ

Msipokomeka na hilo mlilokatazwa na Mwenyezi Mungu, basi kuweni na yakini ya vita kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na mkirudi kwa Mola wenu na mkaacha kula riba, ni haki yenu mchukue madeni yenu bila ya nyongeza, hamumdhulumu yoyote kwa kuchukua zaidi ya rasilmali zenu wala hamudhulumiwi na yoyote kwa kupunguza kiwango cha pesa mlichokopesha. info
التفاسير:

external-link copy
280 : 2

وَإِن كَانَ ذُو عُسۡرَةٖ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيۡسَرَةٖۚ وَأَن تَصَدَّقُواْ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Na iwapo mdaiwa hawezi kulipa, mpeni muhula mpaka Mwenyezi Mungu Atakapomfanyia sahali riziki na kuwarudishia mali yenu. Na mkiacha rasilmali yote au baadhi yake mkamuondolea mdaiwa, hilo ni bora zaidi kwenu, mkiwa mnajua fadhila yake ya kuwa hilo ni bora kwenu katika ulimwengu na Akhea. info
التفاسير:

external-link copy
281 : 2

وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا تُرۡجَعُونَ فِيهِ إِلَى ٱللَّهِۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا كَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na itahadharini, enyi watu, Siku matakaporejeshwa kwa Mwenyezi Mungu, nayo ni Siku ya Kiyama, mtakapo kuorodheshwa kwa Mwenyezi Mungu ili Awahesabu na Amlipe kila mmoja miongoni mwenu kwa alilolitenda la kheri au la shari bila ya kufikiwa na maonevu. Katika aya hii pana ishara kwamba kujiepusha na mapato ya riba yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu, ni kukamilisha Imani na haki za Imani za kutekeleza Swala, kutoa Zaka na kufanya amali njema. info
التفاسير: