Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
49 : 2

وَإِذۡ نَجَّيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ

Kumbukeni neema Yetu juu yenu, tulipowaokoa nyinyi na mateso ya Fir'awn na wafuasi wake, waliokuwa wakiwaonjesha nyinyi adhabu kali sana, wakiwaua watoto wenu wa kiume kwa wingi na kuwaacha wanawake wenu kwa kutumika na kudhalilishwa. Katika hilo, ni mtihani kwenu kutoka kwa Mola wenu. Na katika kuokolewa kwenu na yeye, ni neema kubwa ambayo inapasa kwenu mumshukuru Mwenyezi Mungu Aliyetukuka katika kila zama zenu na vizazi vyenu. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 2

وَإِذۡ فَرَقۡنَا بِكُمُ ٱلۡبَحۡرَ فَأَنجَيۡنَٰكُمۡ وَأَغۡرَقۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ

Kumbukeni neema Yetu juu yenu, tulipoipambanua bahari kwa ajili yenu na tukafanya ndani yake njia kavu, mkavuka na tukawaokoa na Fir'awn na askari wake na msizame majini. Fir'awn na askari wake walipoingia kwenye njia mlizopitia, tuliwazamisha majini mbele ya macho yenu. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 2

وَإِذۡ وَٰعَدۡنَا مُوسَىٰٓ أَرۡبَعِينَ لَيۡلَةٗ ثُمَّ ٱتَّخَذۡتُمُ ٱلۡعِجۡلَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَنتُمۡ ظَٰلِمُونَ

Kumbukeni neema Yetu juu yenu, tulipompa Musa agizo la masiku arubaini la kuiteremshiwa Taurati, iwe ni uongofu na nuru kwenu, na punde tu alipoondoka mlichukua fursa ya kuwa yeye hayupo kwa muda mchache, mkamfanya ndama, mliyomtengeneza kwa mikono yenu, kuwa ni mungu wenu wa kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu. Huu ni ukanushaji Mwenyezi Mungu mbaya kabisa. Na nyinyi mlikuwa madhalimu kwa kumfanya ndama ni Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 2

ثُمَّ عَفَوۡنَا عَنكُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Kisha tukawasamehe kitendo hiki kibaya, tukakubali toba yenu baada ya kurudi Musa kwa kutarajia kuwa mtamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema Zake na fadhila Zake juu yenu, na hamtaendelea kwenye ukafiri na uasi. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 2

وَإِذۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡفُرۡقَانَ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ

Na Kumbukeni neema Yetu juu yenu, tulipompa Mūsā Kitabu chenye kupambanua baina ya haki na batili- nacho ni Taurati- ili muongoke na mtoke kwenye upotevu. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 2

وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ إِنَّكُمۡ ظَلَمۡتُمۡ أَنفُسَكُم بِٱتِّخَاذِكُمُ ٱلۡعِجۡلَ فَتُوبُوٓاْ إِلَىٰ بَارِئِكُمۡ فَٱقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ عِندَ بَارِئِكُمۡ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Na Kumbukeni neema Zetu kwenu, aliposema Mūsā kuwaambia watu wake, “Hakika nyinyi mlijidhulumu nafsi zenu kwa kumfanya ndama ni mungu, basi tubieni kwa Muumba wenu kwa kuuana nyinyi kwa nyinyi. Kufanya hivyo ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu kuliko kukaa milele Motoni.” Na nyinyi mlifuata amri hiyo, ndipo Mwenyezi Mungu Akawafanyia wema kwa kuikubali toba yenu. Hakika Yeye, Aliyetukuka, ni Ndiye Mwingi wa kukubali toba za wenye kutubia miongoni mwa waja wake na ni Ndiye Mwenye kuwarehemu. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 2

وَإِذۡ قُلۡتُمۡ يَٰمُوسَىٰ لَن نُّؤۡمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى ٱللَّهَ جَهۡرَةٗ فَأَخَذَتۡكُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ

Na Kumbukeni pindi mliposema, “Ewe Mūsā! Hatutakuamini kuwa maneno tunayoyasikia kutoka kwako ni maneno ya Mwenyezi Mungu mpaka tumuone Mwenyezi Mungu waziwazi,” ukashuka moto kutoka mbinguni, na nyinyi mnauona kwa macho yenu, ukawaua kwa sababu ya madhambi yenu na ujasiri wenu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 2

ثُمَّ بَعَثۡنَٰكُم مِّنۢ بَعۡدِ مَوۡتِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Kisha tukawahuisha baada ya kufa kwenu kwa kimondo cha moto, ili muishukuru neema ya Mwenyezi Mungu kwenu. Kifo hiki kilikuwa ni adhabu kwao, kisha aliwafufua wakaendelea kuishi mpaka muda wao kumalizika. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 2

وَظَلَّلۡنَا عَلَيۡكُمُ ٱلۡغَمَامَ وَأَنزَلۡنَا عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَنَّ وَٱلسَّلۡوَىٰۖ كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ

Na Kumbukeni neema Zetu mlipokuwa mnahangaika kwenye ardhi, tukawaletea kiwingu cha kuwafinika ili kiwakinge na joto la jua, tukawateremshia mann, nacho ni ktu kifananacho na gundi chenye ladha ya asali; na tukawateremshia salwa, nayo ni aina ya ndege wafananao na tomboro; na tukawaambia, “Kuleni vitu vizuri tulivyowaruzuku na msiende kinyume na dini ya Mwenyezi Mungu,” lakini hamkufuata amri. Na wao hawakutudhulumu sisi kwa kuzikanusha neema hizi, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao, Kwani mwisho mbaya wa dhuluma utawarudia wao. info
التفاسير: