Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
30 : 2

وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِنِّي جَاعِلٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ خَلِيفَةٗۖ قَالُوٓاْ أَتَجۡعَلُ فِيهَا مَن يُفۡسِدُ فِيهَا وَيَسۡفِكُ ٱلدِّمَآءَ وَنَحۡنُ نُسَبِّحُ بِحَمۡدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَۖ قَالَ إِنِّيٓ أَعۡلَمُ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Kumbuka, ewe Mtume, Aliposema Mola wako kuwaambia Malaika, “Mimi nitawaweka watu kwenye ardhi, ili waiimarishe kwa kupishana: wakiondoka watu watakuja wengine baada yao.” Wakasema, “Ewe Mola wetu! Tufundishe na utuongoze, ni kwa hekima gani kuwaumba hawa, pamoja na kuwa mambo yao yatakuwa ni kuleta uharibifu katika ardhi na kumwaga damu kwa dhulma na uonevu, na hali sisi tuko chini ya amri yako: tunakuepusha na mabaya maepusho yanayonasibiana na Sifa zako njema na utukufu Wako, na tunakusifu kwa kila sifa za ukamilifu na utukufu?” Mwenyezi Mungu Akasema kuwaambia, “Mimi najua msiyoyajua kuhusu uzito wa maslahi katika kuwaumba wao.” info
التفاسير:

external-link copy
31 : 2

وَعَلَّمَ ءَادَمَ ٱلۡأَسۡمَآءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمۡ عَلَى ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ فَقَالَ أَنۢبِـُٔونِي بِأَسۡمَآءِ هَٰٓؤُلَآءِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na ili kubainisha utukufu wa Ādam, Amani imshukiye, Mwenyezi Mungu Alimfundisha majina ya vitu vyote, kisha Akaviorodhesha hivyo vitu kwa Malaika na kuwaambia, “Niambieni majina ya vitu hivi vilivyoko, ikiwa nyinyi ni wakweli kwamba nyinyi mnastahiki zaidi uimarishaji wa ardhi kuliko wao.” info
التفاسير:

external-link copy
32 : 2

قَالُواْ سُبۡحَٰنَكَ لَا عِلۡمَ لَنَآ إِلَّا مَا عَلَّمۡتَنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ

Malaika walisema, “Tunakuepusha na kila sifa pungufu, ewe Mola wetu! Sisi hatuna ujuzi isipokuwa ule uliyotufundisha. Wewe, Peke Yako, Ndiye Mjuzi wa mambo ya viumbe vyako, Ndiye Mwenye Hekima katika uendeshaji Wako.” info
التفاسير:

external-link copy
33 : 2

قَالَ يَٰٓـَٔادَمُ أَنۢبِئۡهُم بِأَسۡمَآئِهِمۡۖ فَلَمَّآ أَنۢبَأَهُم بِأَسۡمَآئِهِمۡ قَالَ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ إِنِّيٓ أَعۡلَمُ غَيۡبَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَأَعۡلَمُ مَا تُبۡدُونَ وَمَا كُنتُمۡ تَكۡتُمُونَ

Mwenyezi Mungu Alisema, “Ewe Ādam! Waambie majina ya vitu hivi ambayo walishindwa kuyajua.” Ādam alipowaambia hayo majina, Mwenyezi Mungu Alisema kuwaambia Malaika, “Niliwaambia kuwa Mimi ninayajua yaliyofichika kwenu, ya mbinguni na ardhini, na ninayajua mnayoyafanya kwa dhahiri na mnayoyafanya kwa siri.” info
التفاسير:

external-link copy
34 : 2

وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰ وَٱسۡتَكۡبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na taja kwa watu, ewe Mtume, takrima ya Mwenyezi Mungu kwa Ādam Aliposema Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kuwaambia Malaika, “Msujudieni Ādam kwa njia ya kumheshimu na kuonyesha fadhila zake.” Wote walitii amri, isipokuwa Iblisi alikataa kusujudu kwa sababu ya kiburi na uhasidi, akawa ni miongoni mwa wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu, wenye kuasi amri Yake. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 2

وَقُلۡنَا يَٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ وَكُلَا مِنۡهَا رَغَدًا حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Mwenyezi Mungu Akasema, “Ewe Ādam! Kaa wewe na mkeo Ḥawwā’ kwenye pepo na stareheni kwa matunda yake kwa furaha na ukunjufu popote pale mnapotaka humo, na tahadharini na mti huu, msije mkaingia katika maasia mkawa ni wenye kukiuka amri ya Mwenyezi Mungu.” info
التفاسير:

external-link copy
36 : 2

فَأَزَلَّهُمَا ٱلشَّيۡطَٰنُ عَنۡهَا فَأَخۡرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِۖ وَقُلۡنَا ٱهۡبِطُواْ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ وَلَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُسۡتَقَرّٞ وَمَتَٰعٌ إِلَىٰ حِينٖ

Shetani akawaingiza makosani, kwa kuwashawishi mpaka wakala katika ule mti, ikasababisha kutolewa kwao kwenye Pepo na starehe zake. Na Mwenyezi Mungu Aliwaambia, “Shukeni ardhini, mkiteta nyinyi kwa nyinyi- yaani: Ādam, Ḥawwā’ na Shetani-, na nyinyi katika hiyo ardhi muna utulivu na makao na kunufaika kwa vilivyomo mpaka muda wa maisha yenu ukome.” info
التفاسير:

external-link copy
37 : 2

فَتَلَقَّىٰٓ ءَادَمُ مِن رَّبِّهِۦ كَلِمَٰتٖ فَتَابَ عَلَيۡهِۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Ādam alipokea matamko ya kuomba ili akubaliwe, aliyoletewa na Mwenyezi Mungu, kwa njia ya ilham (ilham), yaliyokusanya toba na kutaka msamaha, nayo ni neno Lake Aliyetukuka, “Ewe Mola wetu! Tumejidhulumu nafsi zetu. Na Usipotusamehe na Kuturehemu, hakika tutakuwa ni miongoni mwa waliyopata hasara.” (7:23). Mwenyezi Mungu Alikubali toba yake na Akamsamehe. Kwani Yeye, Aliyetukuka, ni Mwingi wa kukubali toba ya Mwenye kutubia miongoni mwa waja Wake na ni Mwenye Kuwarehemu. info
التفاسير: