Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
260 : 2

وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِـۧمُ رَبِّ أَرِنِي كَيۡفَ تُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰۖ قَالَ أَوَلَمۡ تُؤۡمِنۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَٰكِن لِّيَطۡمَئِنَّ قَلۡبِيۖ قَالَ فَخُذۡ أَرۡبَعَةٗ مِّنَ ٱلطَّيۡرِ فَصُرۡهُنَّ إِلَيۡكَ ثُمَّ ٱجۡعَلۡ عَلَىٰ كُلِّ جَبَلٖ مِّنۡهُنَّ جُزۡءٗا ثُمَّ ٱدۡعُهُنَّ يَأۡتِينَكَ سَعۡيٗاۚ وَٱعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Na Kumbuka, ewe Mtume, maombi ya Ibrahim kwa Mola wake Amuoneshe namna ya Ufufuzi. Mwenyezi Mungu Alimwambia, «Kwani huamini?» Akasema, «La! Nakuamini. Lakini nataka hilo ili nipate yakini zaidi juu ya yakini niliyonayo.» Akasema, «Chukua ndege wanne, uwe nao, uwachinje na uwakatekate kisha weka sehemu ya hao ndege juu ya kila jabali. Kisha waite, watakujia kwa haraka.» Ibrahim, amani imshukie, akawita. Papo hapo kila sehemu ikarudi mahali pake, na papo hapo wakamjia kwa haraka. Na ujue kuwa Mwenyezi Mungu ni Mshindi, hakuna kimshindacho, ni Mwenye hekima katika maneno Yake, vitendo Vyake, sheria Yake na makadirio Yake. info
التفاسير:

external-link copy
261 : 2

مَّثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنۢبَتَتۡ سَبۡعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنۢبُلَةٖ مِّاْئَةُ حَبَّةٖۗ وَٱللَّهُ يُضَٰعِفُ لِمَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ

Na miongoni mwa vitu bora zaidi vinavyowanufaisha Waumini ni kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na mfano wa Waumini wenye kutoa mali yao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa mbegu iliyopandwa kwenye ardhi nzuri, muda si muda ikatoa mte wenye sehemu saba. Kila sehemu ikatoa suke moja na kila suke likawa na mbegu mia. Na Mwenyezi Mungu Anamuongezea thawabu anayemtaka, kulingana na kadiri ya Imani aliyonayo yule mtoaji na ikhlasi yake iliyo timamu.Na fadhila za Mwenyezi Mungu zimeenea, na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, ni Mjuzi wa yule anayestahiki kuzipata, ni Mwenye kuchungulia nia za waja Wake. info
التفاسير:

external-link copy
262 : 2

ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ لَا يُتۡبِعُونَ مَآ أَنفَقُواْ مَنّٗا وَلَآ أَذٗى لَّهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Wale ambao wanatoa mali yao katika jihadi na aina mbali-mbali za kheri, kisha wasifuatishe, yale waliyoyatoa ya kheri, kwa kumsumbulia waliyempa wala kumkera, kwa neno au kitendo, kwa kumhisisha kuwa wamemfadhili, watapata thawabu kubwa mbele ya Mola wao na hawatakuwa na kicho kuhusu mustakbala wao wa Akhera wala hawatahuzunika juu ya kitu chochote kilichowapita wasikipate katika ulimwengu. info
التفاسير:

external-link copy
263 : 2

۞ قَوۡلٞ مَّعۡرُوفٞ وَمَغۡفِرَةٌ خَيۡرٞ مِّن صَدَقَةٖ يَتۡبَعُهَآ أَذٗىۗ وَٱللَّهُ غَنِيٌّ حَلِيمٞ

Maneno mazuri kujibiwa muombaji na kusamehe utiriri wake katika kuomba, ni bora kuliko sadaka inayofuatiwa na kero na ubaya kutoka kwa mtoaji sadaka. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Hana haja ya sadaka za waja, ni Mpole Hana haraka nao ya kuwatesa. info
التفاسير:

external-link copy
264 : 2

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُبۡطِلُواْ صَدَقَٰتِكُم بِٱلۡمَنِّ وَٱلۡأَذَىٰ كَٱلَّذِي يُنفِقُ مَالَهُۥ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۖ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ صَفۡوَانٍ عَلَيۡهِ تُرَابٞ فَأَصَابَهُۥ وَابِلٞ فَتَرَكَهُۥ صَلۡدٗاۖ لَّا يَقۡدِرُونَ عَلَىٰ شَيۡءٖ مِّمَّا كَسَبُواْۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, msiziondoe thawabu za vitu vile mlivyovitoa sadaka kwa usumbulizi na kero. Kwani huyu, mwenye kufanya haya, anafanana na mtu atowaye mali yake ili watu wamuone na wamsifu ilhali yeye hamuamini Mwenyezi Mungu wala hana yakini na Siku ya Akhera. Mfano wa huyo ni mfano wa jiwe laini lenye mchanga juu yake, lililonyeshewa na mvua nyingi, ikaondoa ule mchanga, ikaliacha tupu halina kitu juu yake. Basi hawa wenye kufanya ria ndivo walivyo, amali zao zinapotea mbele ya Mwenyezi Mungu na hawapati chochote cha thawabu kwa utoaji wao. Na Mwenyezi Mungu hawaafikii makafiri kuifikia haki katika vitu wanvyovitoa na mengineyo. info
التفاسير: