Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
106 : 2

۞ مَا نَنسَخۡ مِنۡ ءَايَةٍ أَوۡ نُنسِهَا نَأۡتِ بِخَيۡرٖ مِّنۡهَآ أَوۡ مِثۡلِهَآۗ أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Tunaipoibadilisha aya au kuiondoa kutoka nyoyoni na akilini, tunaileta yenye manufaa zaidi kwenu kuliko hiyo au tunaileta iliyo mfano wake katika utekelelezaji na thawabu. Na kila mojawapo ya aya hizo ina hekima yake. Kwani hujui, ewe Nabii, kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza, hakuna kitu kinachomshinda? info
التفاسير:

external-link copy
107 : 2

أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ

Kwani hukujua, ewe Nabii, wewe na ummah wako, kwamba Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ndiye Mwenye kumiliki, Ndiye Mwenye kuendesha mambo ya mbinguni na ardhini? Anafanya Analolitaka na Anatoa uamuzi Anaotaka. Anawaamrisha waja Wake na kuwakataza Anavyotaka, na ni juu yao kutii na kukubali. Na wajue wenye kumuasi Yeye kuwa hakuna rafiki mwenye kuwasaidia wala muokozi mwenye kuzuia adhabu ya Mwenyezi Mungu isiwapate. info
التفاسير:

external-link copy
108 : 2

أَمۡ تُرِيدُونَ أَن تَسۡـَٔلُواْ رَسُولَكُمۡ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبۡلُۗ وَمَن يَتَبَدَّلِ ٱلۡكُفۡرَ بِٱلۡإِيمَٰنِ فَقَدۡ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ

Bali nyinyi mnataka, enyi watu, kumuuliza Mtume wenu Muhammad, rehema na amani zimshukie, awapatie mambo, kwa njia ya ukaidi na ujeuri, kama yalivyotakwa, mfano wa hayo, kutoka kwa Mua. Na jueni kwamba mwenye kuchagua ukafiri na kuacha Imani, ashatoka nje ya njia ya Mwenyezi Mungu iliyolingana sawa na ameingia kwenye ujinga na upotevu. info
التفاسير:

external-link copy
109 : 2

وَدَّ كَثِيرٞ مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَوۡ يَرُدُّونَكُم مِّنۢ بَعۡدِ إِيمَٰنِكُمۡ كُفَّارًا حَسَدٗا مِّنۡ عِندِ أَنفُسِهِم مِّنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلۡحَقُّۖ فَٱعۡفُواْ وَٱصۡفَحُواْ حَتَّىٰ يَأۡتِيَ ٱللَّهُ بِأَمۡرِهِۦٓۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Wengi wa Watu wa Kitabu watamani kuwarudisha nyinyi, baada ya kuamini kwenu, muwe makafiri kama mlivyokuwa kabla mkiabudu masanamu. Haya ni kwa sababu ya chuki zilizojaa kwenye nafsi zao, baada ya kuwabainikia ukweli wa Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad, rehema na amani zimshukiye, katika yale aliyokuja nayo. Basi lipuzeni lolote la ubaya au makosa lililotoka kwao. Na sameheni ujahili wao mpaka Mwenyezi Mungu Alete hukumu Yake ya kupigana na wao (na hili lilikuwa), na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu; hakuna kitu chochote kimshindacho. info
التفاسير:

external-link copy
110 : 2

وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Jishughulisheni, enyi Waumini, kutekeleza Swala kwa namna sahihi ipasavyo na kutoa Zaka zilizofaradhiwa. Na mjue kwamaba kila kheri mnayoitangulizia nafsi zenu, mtapata thawabu zake Akhera mbele ya Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye Aliyetukuka ni Mwenye kuyaona matendo yenu na Atawalipa kwayo. info
التفاسير:

external-link copy
111 : 2

وَقَالُواْ لَن يَدۡخُلَ ٱلۡجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوۡ نَصَٰرَىٰۗ تِلۡكَ أَمَانِيُّهُمۡۗ قُلۡ هَاتُواْ بُرۡهَٰنَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Mayahudi na Wanaswara, kila mmoja katika wao anadai kuwa Pepo itaingiwa na pote lake peke yake, hataingia asiyekuwa katika pote hilo. Hayo ni mawazo yao maovu. Waambie, ewe Mtume, “Leteni dalili yenu juu ya ushahidi wa hilo mnalolidai iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu.” info
التفاسير:

external-link copy
112 : 2

بَلَىٰۚ مَنۡ أَسۡلَمَ وَجۡهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحۡسِنٞ فَلَهُۥٓ أَجۡرُهُۥ عِندَ رَبِّهِۦ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Mambo si kama walivyodhania kuwa Pepo ni ya pote fulani tu, si ya pote lingine. Hakika ataingia Peponi mwenye kumtakasa Mwenyezi Mungu Peke Yake Asiye na mshirika na akawa ni mwenye kumfuata Mtume Muhammad, rehema na amani zimshukie, katika maneno yake yote na vitendo vyake vyote. Basi mwenye kufanya hayo atakuwa na thawabu ya matendo yake mbele ya Mola wake huko Akhera, nayo ni kuingia Peponi, hali ya kuwa wao, hao wenye kuingia Peponi, hawaogopi mambo ya Akhera yanayowakabili mbele yao, wala hawahuzuniki juu ya hadhi za ulimwengu zilizowapita. info
التفاسير: