Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
120 : 2

وَلَن تَرۡضَىٰ عَنكَ ٱلۡيَهُودُ وَلَا ٱلنَّصَٰرَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمۡۗ قُلۡ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلۡهُدَىٰۗ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم بَعۡدَ ٱلَّذِي جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ

Na hawataridhika nawe, ewe Mtume, Mayahudi wala Wanaswara isipokuwa ikiwa utaacha Dini yako na ukafuata Dini yao. Waambie, “Dini ya Uislamu ndiyo Dinii sahihi” Na ukifuata matamanio ya hao, baada ya wahyi uliokujia, hutakuwa na rafiki wa kukunufaisha kwa Mwenyezi Mungu wala msaidizi wa kukunusuru. Maneno haya ingawa anaambiwa Mtume, yanalekezwa kwa ummah wote. info
التفاسير:

external-link copy
121 : 2

ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَتۡلُونَهُۥ حَقَّ تِلَاوَتِهِۦٓ أُوْلَٰٓئِكَ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۗ وَمَن يَكۡفُرۡ بِهِۦ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Wale Mayahudi na Wanaswara tuliowapa Kitabu, wanakisoma kisomo cha sawasawa, wanakifiuata kipasavyo kufuatwa na wanayaamini yaliyomo ndani yake ya kuwaamini Mitume wa Mwenyezi Mungu, ambao miongoni mwao ni wa mwisho wao, Nabii wetu na Mtume wetu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,. Na hawayapotoi wala hawayabadilishi yaliyokuja ndani yake. Hawa ndio waliomuamini Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na aliyoteremshiwa. Ama wale waliogeuza sehemu ya Kitabu na wakaficha baadhi yake, hao ndio waliomkanusha Nabii wa Mwenyezi Mungu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na yale aliyoteremshiwa. Na wenye kumkanusha, hao watakuwa ni wetu wenye hasara kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
122 : 2

يَٰبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتِيَ ٱلَّتِيٓ أَنۡعَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ وَأَنِّي فَضَّلۡتُكُمۡ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

Enyi kizazi cha Ya’qūb, tajeni neema zangu kubwa kwenu na mkumbuke kuwa niliwatukuza juu ya watu wa zama zenu kwa wingi wa Manabii wenu na kwa Vitabu walivyoteremshiwa. info
التفاسير:

external-link copy
123 : 2

وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا لَّا تَجۡزِي نَفۡسٌ عَن نَّفۡسٖ شَيۡـٔٗا وَلَا يُقۡبَلُ مِنۡهَا عَدۡلٞ وَلَا تَنفَعُهَا شَفَٰعَةٞ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Na ogopeni vitisho vya Siku ya Hesabu. Kwani hapo, hakuna nafsi itakayoifaa kitu chochote nafsi nyingine, wala Mwenyezi Mungu Hatakubali fidia, kutoka kwa hiyo nafsi, ya kuiyokoa na adhabu, wala hainufaiki kwa kuombewa na hakuna yoyote wa kuinusuru. info
التفاسير:

external-link copy
124 : 2

۞ وَإِذِ ٱبۡتَلَىٰٓ إِبۡرَٰهِـۧمَ رَبُّهُۥ بِكَلِمَٰتٖ فَأَتَمَّهُنَّۖ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامٗاۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِيۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهۡدِي ٱلظَّٰلِمِينَ

Na Kumbuka, ewe Nabii, wakati Mwenyezi Mungu Alipomfanyia mtihani Ibrāhīm kwa amri Alizomkalifisha nazo, akazitekeleza na kusimama nazo kwa njia nzuri. Mwenyezi Mungu Akamwambia, “Mimi nimekufanya wewe ni kiigizo kwa watu.” Ibrāhīm akasema, “Ewe Mola wajaalie baadhi ya watu wa kizazi chake ni viongozi kwa ukarimu Zako.” Mwenyezi Mungu Akamjibu kwamba madhalimu hawatapata uongozi wa kidini. info
التفاسير:

external-link copy
125 : 2

وَإِذۡ جَعَلۡنَا ٱلۡبَيۡتَ مَثَابَةٗ لِّلنَّاسِ وَأَمۡنٗا وَٱتَّخِذُواْ مِن مَّقَامِ إِبۡرَٰهِـۧمَ مُصَلّٗىۖ وَعَهِدۡنَآ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيۡتِيَ لِلطَّآئِفِينَ وَٱلۡعَٰكِفِينَ وَٱلرُّكَّعِ ٱلسُّجُودِ

Na Kumbuka, ewe Nabii, wakati tulipoifanya Alkaba ni marejeo ya watu; wanakuja kuikusudia, kisha wanarudi makwao kwa watu wao, kisha wanairudia tena, ni makusanyiko yao katika Hija, Umra, kutufu na kuswali, na pia ni amani kwao: hakuna adui anayewashambulia wakiwa hapo na tukasema, “Pafanyeni hapo Maqām Ibrāhīm ni mahali pa kuswali. Maqām Ibrāhīn ni jiwe ambalo Ibrāhīm alisimama juu yake alipokuwa akijenga Alkaba. Na tulimletea Wahyi Ibrahīm na mtoto wake Ismāīl kwa kuwaambia, «Isafisheni Nyumba Yangu na kila najisi na uchafu kwa ajili ya wenye kuabudu kwa kutufu pambizoni mwa Alkaba au kuketi Itikafu (I’tikāf) Msikitini na kuswali hapo.” info
التفاسير:

external-link copy
126 : 2

وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِـۧمُ رَبِّ ٱجۡعَلۡ هَٰذَا بَلَدًا ءَامِنٗا وَٱرۡزُقۡ أَهۡلَهُۥ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ مَنۡ ءَامَنَ مِنۡهُم بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ قَالَ وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُۥ قَلِيلٗا ثُمَّ أَضۡطَرُّهُۥٓ إِلَىٰ عَذَابِ ٱلنَّارِۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Na Kumbuka, ewe Nabii, wakati Aliposema Ibrāhīm akiwa katika maombi, “Ewe Mola wangu! ijaalie Makkah ni mji wenye amani usiokuwa na kitisho, uwaruzuku watu wake aina ya matunda na uwahusu kwa riziki hii wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.” Mwenyezi Mungu Alisema, “Na mwenye kukufuru katika wao nitamruzuku ulimwenguni na kumstarehesha starehe chache, kasha nitamlazimisha kwa nguvu kwenda Motoni. Ubaya wa marejeo na makao ni mwisho huu.” info
التفاسير: