Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
17 : 2

مَثَلُهُمۡ كَمَثَلِ ٱلَّذِي ٱسۡتَوۡقَدَ نَارٗا فَلَمَّآ أَضَآءَتۡ مَا حَوۡلَهُۥ ذَهَبَ ٱللَّهُ بِنُورِهِمۡ وَتَرَكَهُمۡ فِي ظُلُمَٰتٖ لَّا يُبۡصِرُونَ

Hali ya wanafiki ambao wameuamini, kidhahiri sio kindani, utume wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie yeye, kisha wakakanusha, wakawa wanaenda huku na kule kwenye giza la upotevu wao bila kujua wanapoenda wala kuwa na matarajio ya kutoka kwenye giza hilo, inafanana na hali ya kikundi cha watu, kwenye usiku wa giza, ambapo mmoja wao aliwasha moto mkubwa ili wapate joto na mwangaza. Moto ulipowaka na kung’arisha pambizo zake, ulizimika na giza likaenea. Wakawa watu hao wako kwenye giza, hawaoni chochote wala hawaongoki kupajua penye njia ya kujua matoko. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 2

صُمُّۢ بُكۡمٌ عُمۡيٞ فَهُمۡ لَا يَرۡجِعُونَ

Wao ni viziwi, hawaisikii haki kwa kuizingatia, ni mabubu, hawaitamki haki, ni vipofu, hawauoni mwangaza wa uongofu. Kwa hivyo, hawawezi kurudi kwenye Imani ambayo waliiacha na kuchukuwa upotevu badali yake. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 2

أَوۡ كَصَيِّبٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فِيهِ ظُلُمَٰتٞ وَرَعۡدٞ وَبَرۡقٞ يَجۡعَلُونَ أَصَٰبِعَهُمۡ فِيٓ ءَاذَانِهِم مِّنَ ٱلصَّوَٰعِقِ حَذَرَ ٱلۡمَوۡتِۚ وَٱللَّهُ مُحِيطُۢ بِٱلۡكَٰفِرِينَ

Au hali yao inafanana na hali ya kikundi kingine cha wanafiki ambao haki inawadhihirikia wakati mwengine, na huwa na shaka nayo wakati mwengine. Hali yao ni ile ya watu wanaotembea jangwani, wakanyeshewa na mvua nyingi, iliyofuatana na giza lingi lililopandana, mpigo wa radi pamoja na mng’aro wa pepe na vimondo vyenye kuchoma. Hivyo vinawafanya wao, kwa vituko vyake, kuweka vidole vyao kwenye masikio yao, kwa kuogopa kufa. Na Mwenyezi Mungu Amewazunguka makafiri, hawamponyoki wala hawamshindi. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 2

يَكَادُ ٱلۡبَرۡقُ يَخۡطَفُ أَبۡصَٰرَهُمۡۖ كُلَّمَآ أَضَآءَ لَهُم مَّشَوۡاْ فِيهِ وَإِذَآ أَظۡلَمَ عَلَيۡهِمۡ قَامُواْۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَذَهَبَ بِسَمۡعِهِمۡ وَأَبۡصَٰرِهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Hizo pepe, kwa mng’aro wake, zinakaribia kuwatoa macho yao. Pamoja na hivyo, kila pepe ikiwang’arishia njia, wanatembea kwenye mwangaza wake, na ikiondoka, njia huwa na giza ikawabidi wasimame pale waliopo. Lau si Mwenyezi Mungu kuwapa muda, Angewaondolea masikizi yao ya kusikia na macho yao ya kuonea. Na Yeye ni mwenye uweza wa kufanya hilo wakati wowote. Yeye ni Muweza wa kila kitu. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 2

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱعۡبُدُواْ رَبَّكُمُ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ

Mwito utokao kwa Mwenyezi Mungu kwa binadamu wote: Muabuduni Mwenyezi Mungu Ambaye Amewalea kwa neema zake, na mumuogope wala msiende kinyume na dini Yake. Kwani yeye ndiye Aliyewaumba kutoka kwenye hali ya kutokuwako, na Akawaumba waliokuwa kabla yenu, ili muwe ni miongoni mwa wenye kumcha Mwenyezi Mungu ambao Yeye Ameridhika nao na wao wameridhika na Yeye. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 2

ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ فِرَٰشٗا وَٱلسَّمَآءَ بِنَآءٗ وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجَ بِهِۦ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ رِزۡقٗا لَّكُمۡۖ فَلَا تَجۡعَلُواْ لِلَّهِ أَندَادٗا وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Mola wenu ni Yule Aliyewafanyia ardhi iwe ni tandiko, ili maisha yenu yawe mepesi juu yake, na mbingu ziwe zimejengeka madhubuti, na Akateremsha mvua kutoka kwenye mawingu, Akatoa kwa mvua hiyo matunda na mimea aina mbalimbali ili iwe ni riziki kwenu. Basi, msimuwekee Mwenyezi Mungu washirika katika ibada, hali nyinyi mnajua kuwa Mwenyezi Mungu Amepwekeka katika kuumba, kuruzuku na kustahiki kuabudiwa. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 2

وَإِن كُنتُمۡ فِي رَيۡبٖ مِّمَّا نَزَّلۡنَا عَلَىٰ عَبۡدِنَا فَأۡتُواْ بِسُورَةٖ مِّن مِّثۡلِهِۦ وَٱدۡعُواْ شُهَدَآءَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na mkiwa, enyi makafiri, muna shaka juu ya Qurani tuliyomteremshia mja wetu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukie, na mkadai kuwa haitoki kwa Mwenyezi Mungu, basi leteni sura moja inayofanana na sura ya Qurani, na takeni msaada kutoka kwa yoyote mnayemuweza ili awasaidie, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 2

فَإِن لَّمۡ تَفۡعَلُواْ وَلَن تَفۡعَلُواْ فَٱتَّقُواْ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلۡحِجَارَةُۖ أُعِدَّتۡ لِلۡكَٰفِرِينَ

Mkiwa hamuwezi sasa, na hamtaweza wakati unaokuja kabisa, basi uogopeni Moto, kwa kumuamini Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kumtii Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu na Mitume Wake. info
التفاسير: