Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
249 : 2

فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِٱلۡجُنُودِ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ مُبۡتَلِيكُم بِنَهَرٖ فَمَن شَرِبَ مِنۡهُ فَلَيۡسَ مِنِّي وَمَن لَّمۡ يَطۡعَمۡهُ فَإِنَّهُۥ مِنِّيٓ إِلَّا مَنِ ٱغۡتَرَفَ غُرۡفَةَۢ بِيَدِهِۦۚ فَشَرِبُواْ مِنۡهُ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُۥ هُوَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ قَالُواْ لَا طَاقَةَ لَنَا ٱلۡيَوۡمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦۚ قَالَ ٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَٰقُواْ ٱللَّهِ كَم مِّن فِئَةٖ قَلِيلَةٍ غَلَبَتۡ فِئَةٗ كَثِيرَةَۢ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Alipotoka Twalut na askari wake kwenda kupigana na watu majabari, aliwaambia, «Mwenyezi Mungu Atawapa mtihani wa subira kwa mto uliyo mbele yenu mtakaouvuka, ili abainike mwenye Imani na aliye mnafiki. Yoyote kati yenu atakaye kunywa maji ya mto huo, si katika mimi, wala hafai kuwa na mimi kwenye jihadi. Na yule ambaye hatayaonja maji hayo, yeye ni katika mimi, kwa kutii amri yangu, na anafaa kwa jihadi. Isipokuwa aliyeruhusiwa na akateka mteko mmoja kwa mkono wake, huyo hana lawama. Basi walipofika mtoni, waliyaangukia maji na waliyanywa sana isipokuwa idadi ya watu wachache kati yao, walisubiri juu ya kiu na joto na wakatosheka na mteko wa mkono. Wakati huo wale walioasi amri, walirudi nyuma. Tālūt pamoja na wale Waumini wachache walipouvuka mto - walikuwa watu zaidi ya mia tatu na kumi- kwa ajili ya kupambana na maadui zao na wakaona wingi wa maadui zao na wingi wa silaha walionazo, walisema, «Hatuna uwezo leo wa kupigana na Jālūt na askari wake wenye nguvu. Hapo, wale wliokuwa na yakini ya kukutana na Mola Wao walijibu wakiwakumbusha ndugu zao juu ya Mwenyezi Mungu na uwezo Wake, «Nivikundi vingapi vichache, venye imani na subira, viliyashinda, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, makundi yaliyokuwa na watu wengi makafiri wenye kuasi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Yupo pamoja na wenye subira kwa taufiki Yake na nusra Yake na malipo Yake mema. info
التفاسير:

external-link copy
250 : 2

وَلَمَّا بَرَزُواْ لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦ قَالُواْ رَبَّنَآ أَفۡرِغۡ عَلَيۡنَا صَبۡرٗا وَثَبِّتۡ أَقۡدَامَنَا وَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na walipojitokeza kwa Jālūt na askari wake na wakaiona hatari kwa macho yao, walifazaika na kumuelekea kwa Mwenyezi Mungu kwa maombi na kunyenyekea huku wakisema, «EweMola wetu! Tumiminie subira nyingi kwenye nyoyo zetu, Uzithibitishe nyayo zetu ziwe thabiti muda wa kupigana na adui, zisiwe na uoga wa kukimbia vita, na Utunusuru kwa msaada wako juu ya watu makafiri. info
التفاسير:

external-link copy
251 : 2

فَهَزَمُوهُم بِإِذۡنِ ٱللَّهِ وَقَتَلَ دَاوُۥدُ جَالُوتَ وَءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ٱلۡمُلۡكَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَعَلَّمَهُۥ مِمَّا يَشَآءُۗ وَلَوۡلَا دَفۡعُ ٱللَّهِ ٱلنَّاسَ بَعۡضَهُم بِبَعۡضٖ لَّفَسَدَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ ذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

Hapo waliwashinda kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na Dāwūd, Amani imshukiye, alimuua Jālūt, kiongozi wa majabari. Na Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka, baada ya hapo, Akampa Dāwūd ufalme na utume katika Wana wa Isrāīl, na Alimfundisha Aliyoyataka miongoni mwa elimu. Na lau kama si himaya ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwatumia baadhi ya watu- nao ni wale watiifu Kwake na wanaomuamini- kuwazuia wengine- nao ni wanaomuasi Mwenyezi Mungu na kumshirikisha-, basi ardhi ingaliharibika kwa ushindi wa ukafiri na kupata nguvu uharibifu na wenye kufanya maasia. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kwa viumbe wote. info
التفاسير:

external-link copy
252 : 2

تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ نَتۡلُوهَا عَلَيۡكَ بِٱلۡحَقِّۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Hizo ni hoja za Mwenyezi Mungu na dalili Zake tunakusimulia wewe, ewe Nabii, kwa kweli, na hakika wewe ni miongoni mwa Mitume walio wakweli. info
التفاسير: