Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
164 : 2

إِنَّ فِي خَلۡقِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱخۡتِلَٰفِ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ وَٱلۡفُلۡكِ ٱلَّتِي تَجۡرِي فِي ٱلۡبَحۡرِ بِمَا يَنفَعُ ٱلنَّاسَ وَمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مِن مَّآءٖ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَآبَّةٖ وَتَصۡرِيفِ ٱلرِّيَٰحِ وَٱلسَّحَابِ ٱلۡمُسَخَّرِ بَيۡنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ

Hakika, katika kuumba mbingu kwa kuzifanya ziinuke juu na ziwe kunjufu, na ardhi kwa majabali yake, mabonde yake na bahari zake, na katika kutafautiana usiku na mchana kwa urefu na ufupi, giza na muangaza, na kuandamana kwao kwa kila mmoja kukaa pahali pa mwingine, na katika majahazi yanayopita baharini, yanayobeba vitu vinavyowanufaisha watu, na katika maji ya mvua Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, Akaipa uhai ardhi kwa maji hayo ikawa rangi ya kijani yenye kupendeza baada ya kuwa kavu isiyokuwa na mimea, na vile Alivyoeneza Mwenyezi Mungu humo kila kitambaacho juu ya ardhi hiyo, na katika yale Aliyowaneemesha kwayo ya kuugeuza upepo na kuuelekeza, na katika mawingu yanayopelekwa baina ya mbingu na ardhi, hakika, katika dalili zote hizo zilizopita, pana alama za upweke wa Mwenyezi Mungu na ukubwa wa neema Zake kwa watu wanaoelewa sehemu za hoja na wanaozifahamu dalili za Mwenyezi Mungu Aliyetukuka juu ya upweke Wake na kustahiki Kwake Peke Yake kuabudiwa. info
التفاسير:

external-link copy
165 : 2

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَندَادٗا يُحِبُّونَهُمۡ كَحُبِّ ٱللَّهِۖ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَشَدُّ حُبّٗا لِّلَّهِۗ وَلَوۡ يَرَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ إِذۡ يَرَوۡنَ ٱلۡعَذَابَ أَنَّ ٱلۡقُوَّةَ لِلَّهِ جَمِيعٗا وَأَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعَذَابِ

Pamoja na hizi hoja za kukata, kinatoka kikundi cha watu wakichukua, badala ya Mwenyezi Mungu, masanamu na wategemewa wakiwafanya ni kama Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kuwapa mapenzi, heshima na twaa, Mambo yasiyostahiki kufanyiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na Waumini, mapenzi yao kwa Mwenyezi Mungu ni makubwa zaidi kuliko mapenzi ya hawa makafiri kwa Mwenyezi Mungu na kwa waungu wao. Sababu Waumini wamemtakasia Mwenyezi Mungu mapenzi yao yote. Na hao makafiri wamemshirikisha Mwenyezi Mungu katika mapenzi. Na lau wangalijua wale waliojidhulumu nafsi zao kwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika maisha ya kidunia, pindi watakapoiona adhabu ya Akhera, kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Peke Yake Mwenye nguvu zote na kwamba Mwenyezi Mungu ni mkali wa adhabu, hawangaliwafanya wasiokuwa Mwenyezi Mungu kuwa ni waungu wakawa wanawaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, na kujikurubisha nao Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
166 : 2

إِذۡ تَبَرَّأَ ٱلَّذِينَ ٱتُّبِعُواْ مِنَ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُواْ وَرَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَ وَتَقَطَّعَتۡ بِهِمُ ٱلۡأَسۡبَابُ

Watakapoiyona adhabu ya Akhera, watajitenga wale viongozi waliofuatwa kujiepusha na wale waliowafuata katika ushirikina na zitawakatikia wao aina zote za mawasiliano waliyojifungamanisha nayo duniani: ya ujamaa, ufuasi, dini na mengineyo yasiyokuwa hayo. info
التفاسير:

external-link copy
167 : 2

وَقَالَ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُواْ لَوۡ أَنَّ لَنَا كَرَّةٗ فَنَتَبَرَّأَ مِنۡهُمۡ كَمَا تَبَرَّءُواْ مِنَّاۗ كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ ٱللَّهُ أَعۡمَٰلَهُمۡ حَسَرَٰتٍ عَلَيۡهِمۡۖ وَمَا هُم بِخَٰرِجِينَ مِنَ ٱلنَّارِ

Na wale wafuasi watasema, «Twatamani tuwe na marejeo ya duniani, ili tutangaze kujitenga kwetu na hawa viongozi kama walivyotangaza kujitenga kwao na sisi.» Na kama Alivyowaonesha Mwenyezi Mungu ukali wa adhabu Yake, Siku ya Kiyama, Atawaonesha vitendo vyao viovu kuwa ni majuto kwao. Na hawatakuwa ni wenye kutoka Motoni kabisa. info
التفاسير:

external-link copy
168 : 2

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ كُلُواْ مِمَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ حَلَٰلٗا طَيِّبٗا وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٌ

Enyi watu, kuleni katika riziki ya Mwenyezi Mungu, iliyoko kwenye ardhi, ile ambayo Amewahalalishia nyinyi, nayo ni iliyo tohara isiyokuwa najisi, inayonufaisha isiyodhuru wala msifuate njia za Shetani katika kuhalalisha, kuharamisha, uzushi na maasia. Hakika Yeye ni adui yenu mwenye uadui uliyo wazi. info
التفاسير:

external-link copy
169 : 2

إِنَّمَا يَأۡمُرُكُم بِٱلسُّوٓءِ وَٱلۡفَحۡشَآءِ وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Hakika Shetani anawaamuru mfanye kila sampuli ya dhambi baya linalowatia uovuni, na kila maasia yenye upeo wa uchafu, na mumzulie Mwenyezi Mungu urongo, kama kuharamisha halali na mangineyo, pasi na ujuzi wowote info
التفاسير: