કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષામાં અનુવાદ - અલી મોહસીન અલ્ બર્વાની

પેજ નંબર:close

external-link copy
283 : 2

۞ وَإِن كُنتُمۡ عَلَىٰ سَفَرٖ وَلَمۡ تَجِدُواْ كَاتِبٗا فَرِهَٰنٞ مَّقۡبُوضَةٞۖ فَإِنۡ أَمِنَ بَعۡضُكُم بَعۡضٗا فَلۡيُؤَدِّ ٱلَّذِي ٱؤۡتُمِنَ أَمَٰنَتَهُۥ وَلۡيَتَّقِ ٱللَّهَ رَبَّهُۥۗ وَلَا تَكۡتُمُواْ ٱلشَّهَٰدَةَۚ وَمَن يَكۡتُمۡهَا فَإِنَّهُۥٓ ءَاثِمٞ قَلۡبُهُۥۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ عَلِيمٞ

Na mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, yatosha kukabidhiwa rahani. Na mmoja wenu akimwekea amana mwenziwe basi aliye aminiwa airudishe amana ya mwenzake, na amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala msifiche ushahidi. Na atakaye ficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mnayo yatenda. info

Ikiwa mko safarini na hamkupata mtu wa kuliandika deni, basi kwa dhamana ya deni wekeni kitu kuwa ni rahani ashike mwenye kukopesha kutokana na mwenye kukopa. Na mtu akipewa dhamana na mwenzie kushika, basi iwe hiyo ni amana ilioko mikononi mwake. Yeye ametegemewa kwa uaminifu wake. Basi inapo takikana amana na aitoe amana ya watu. Na amche Mwenyezi Mungu aliye muumba na kumlea na kumshughulikia kwa uangalifu ili isimkatikie neema ya Mola wake Mlezi duniani na Akhera. Wala msifiche ushahidi unapo takikana. Mwenye kuficha amepata dhambi, na khabithi wa moyo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mnayo yafanya. Atakulipeni kwa mujibu mnavyo stahiki.

التفاسير:

external-link copy
284 : 2

لِّلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَإِن تُبۡدُواْ مَا فِيٓ أَنفُسِكُمۡ أَوۡ تُخۡفُوهُ يُحَاسِبۡكُم بِهِ ٱللَّهُۖ فَيَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Viliomo mbinguni na viliomo duniani ni vya Mwenyezi Mungu. Na mkidhihirisha yaliyomo katika nafsi zenu au mkayaficha, Mwenyezi Mungu atakuhisabuni kwayo. Kisha amsamehe amtakaye na amuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. info

Jueni kuwa vyote viliomo mbinguni na duniani ni vya Mwenyezi Mungu, naye ana makdara navyo vyote na anavijua vyote. Ni sawa sawa ikiwa mtadhihirisha yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkificha, Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa vyote na mwenye kupata khabari za vyote. Naye Siku ya Kiyama atakuhisabuni kwa hayo, na atamghufiria amtakaye na atamuadhibu amtakaye. Yeye ni Muweza wa kila kitu.

التفاسير:

external-link copy
285 : 2

ءَامَنَ ٱلرَّسُولُ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِ مِن رَّبِّهِۦ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَۚ كُلٌّ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَمَلَٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّن رُّسُلِهِۦۚ وَقَالُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۖ غُفۡرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيۡكَ ٱلۡمَصِيرُ

Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako. info

Hakika aliyo teremshiwa Mtume Muhammad s.a.w. ni Haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Naye amemuamini Mwenyezi Mungu, na pamoja naye wameamini pia Waumini, wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake. Wao wanawaamini Mitume wote wa Mwenyezi Mungu sawa sawa, na wanawatukuza sawa, huku wakisema: Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake. Na wametilia mkazo Imani yao ya moyoni kwa kauli yao ya ulimini huku wakimuelekea Mwenyezi Mungu kumwambia: Mola Mlezi wetu! Tumesikia uliyo yateremsha yenye hikima, na tumeyapokea yaliyo amrishwa. Ewe Mola wetu Mlezi! Tupe maghfira yako. Na kwako Wewe tu pekee ndio tunako kwendea na ndio marejeo.

التفاسير:

external-link copy
286 : 2

لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَاۚ لَهَا مَا كَسَبَتۡ وَعَلَيۡهَا مَا ٱكۡتَسَبَتۡۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذۡنَآ إِن نَّسِينَآ أَوۡ أَخۡطَأۡنَاۚ رَبَّنَا وَلَا تَحۡمِلۡ عَلَيۡنَآ إِصۡرٗا كَمَا حَمَلۡتَهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِنَاۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلۡنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِۦۖ وَٱعۡفُ عَنَّا وَٱغۡفِرۡ لَنَا وَٱرۡحَمۡنَآۚ أَنتَ مَوۡلَىٰنَا فَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyho. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. (Ombeni:)Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri. info

Hakika Mwenyezi Mungu hawakalifishi waja wake ila kwa kadiri wanavyo weza kuyafanya na kuyafuata. Kwa hivyo kila mwenye kukalifishwa atalipwa kwa vitendo vyake - akitenda kheri atapata malipo ya kheri, akitenda shari atapata shari. Basi enyi Waumini! Nyenyekeeni kwa Mwenyezi Mungu mkimuomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Usituadhibu pindi tukiporonyoka tukasahau ulio tuamrisha, au yakatupata ya kutusabibisha kutumbukia makosani. Mola Mlezi wetu! Usituchukulie kwa shida ukatupa sharia nzito nzito kama ulivyo wafanyia Mayahudi kwa sababu ya inda yao na udhalimu wao. Wala usitukalifishe mambo tusiyo yaweza, na utusamehe kwa ukarimu wako, na tughufirie kwa fadhila yako, na uturehemu kwa rehema yako yenye wasaa. Hakika Wewe ni Mola Mlezi wetu. Tunusuru ewe Mola Mlezi, kwa ajili ya kutukuza Neno lako na kuitangaza Dini yako - tuwashinde kaumu ya wapingaji.

التفاسير: