કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષામાં અનુવાદ - અલી મોહસીન અલ્ બર્વાની

પેજ નંબર:close

external-link copy
146 : 2

ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَعۡرِفُونَهُۥ كَمَا يَعۡرِفُونَ أَبۡنَآءَهُمۡۖ وَإِنَّ فَرِيقٗا مِّنۡهُمۡ لَيَكۡتُمُونَ ٱلۡحَقَّ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ

Wale tulio wapa Kitabu wanayajua haya kama wanavyo wajua watoto wao; na kuna kikundi katika wao huificha haki na hali wanajua. info

Na hakika Watu wa Kitabu wanajua kuwa huku kugeuza Kibla ni jambo la haki, na wanakutambua kuwa wewe ndiye Nabii aliye sifiwa katika vitabu vyao, na miongoni mwa sifa hizo kuwa atasali kuelekea Alkaaba. Na kujua kwao Unabii wako na kukijua Kibla chako ni sawa sawa wanavyo wajua watoto wao kwa uwazi kabisa. Lakini baadhi yao wanaificha kweli hii juu ya kuwa wanajua, kwa kufuata pumbao na chuki zao za upotovu kuwania mila zao kwa ajili ya kulinda madaraka yao, na wanatafuta hila za kukupotoeni nyie.

التفاسير:

external-link copy
147 : 2

ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ

Haki inatoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanao fanya shaka. info

Na hakika Haki ni anayo kutolea Mwenyezi Mungu Mtukufu sio wanayo kupotoshelea watu wa Kitabu. Basi kuweni na yakini nayo, msiwe watu wenye kutia shaka shaka na kubabaika. Na katika hiyo Haki ni hii amri ya Kibla, basi endeleeni nayo wala msiwabali (musiwajali) wapinzani.

التفاسير:

external-link copy
148 : 2

وَلِكُلّٖ وِجۡهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَاۖ فَٱسۡتَبِقُواْ ٱلۡخَيۡرَٰتِۚ أَيۡنَ مَا تَكُونُواْ يَأۡتِ بِكُمُ ٱللَّهُ جَمِيعًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Na kila mmoja anao upande anao elekea. Basi shindanieni mema. Popote mlipo Mwenyezi Mungu atakuleteni nyote pamoja. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. info

Hakika Kibla hicho tulicho kuelekeza ndicho Kibla chako na Kibla cha Umma wako. Na hali kadhaalika kila umma una kibla chake unako elekea katika swala yao kwa mujibu wa sharia zilizo kwisha pita. Wala katika haya hapana kupikuana kwa ubora, na ama kupikuana kwa ubora ni kwa kutenda vitendo vya ut'iifu na a'mali za kheri. Basi kimbilieni kwenye kheri na mshindane kwa hayo. Mwenyezi Mungu atakuhisabuni kwa hayo, kwani Yeye atakukusanyeni nyote Siku ya Kiyama kutoka kokote mtapo kuwako. Wala hatamchopoka hata mmoja. Kila kitu kimo mkononi mwake, na katika hivyo ni amana, kuhuisha, kufufua na kukusanya.

التفاسير:

external-link copy
149 : 2

وَمِنۡ حَيۡثُ خَرَجۡتَ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۖ وَإِنَّهُۥ لَلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na hiyo ndiyo Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yatenda. info

Basi katika Swala zako popote pale ulipo uelekee Msikiti Mtakatifu, ukiwa upo mjini au umo safarini, popote wendapo. Na hakika haya bila ya shaka ndiyo ya Haki yanayo wafikiana na hikima ya Mola wako Mlezi aliye pamoja nawe. Basi wewe na umma wako yatamanini haya. Kwani Mwenyezi Mungu atakulipeni malipo mema kabisa. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye ujuzi wala hapana katika vitendo vyenu vilivyo fichikana naye.

التفاسير:

external-link copy
150 : 2

وَمِنۡ حَيۡثُ خَرَجۡتَ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَحَيۡثُ مَا كُنتُمۡ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ شَطۡرَهُۥ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيۡكُمۡ حُجَّةٌ إِلَّا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِي وَلِأُتِمَّ نِعۡمَتِي عَلَيۡكُمۡ وَلَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ

Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo ili watu wasiwe na hoja juu yenu, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao Basi msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi - na ili nikutimizieni neema yangu, na ili mpate kuongoka. info

Jilazimishe kuifuata amri ya Mwenyezi Mungu katika mambo ya kuelekea Kibla, na kuwa na pupa nayo wewe na umma wako. Na uelekeze uso wako uelekee upande wa Msikiti Mtakatifu popote wendapo katika safari zako. Na elekeeni huko popote mtapo kuwapo pande zote za dunia, mkiwa mko safarini au mpo mjini, ili ukatike ule ushindani wa hoja za hao walio khalifu na wanao jadiliana nanyi ikiwa hamkufuata amri hii ya kugeuza Kibla. Mayahudi watasema: Vipi Muhammad anapo sali anaelekea Beitul Muqaddas, na Nabii alielezwa katika vitabu vyetu ni kuwa moja katika sifa zake anaelekea Alkaaba? Na washirikina wa Kiarabu watasema: Vipi anadai kuwa mila yake ni mila ya Ibrahim, naye hafuati Kibla chake? Juu ya vyote hakika hao walio dhulumu walio potoka wakaiacha Haki kutoka pande zote mbili hawatoacha majadiliano yao na upotovu wao, bali watasema: Hakugeuka kuelekea Alkaaba ila kuwa anafuata ile ile dini ya kishirikina ya kaumu yake, na kuupenda ule mji wake. Basi nyinyi msiwabali hao, kwani uchochezi wao hauto kudhuruni. Nanyi niogopeni Mimi, msiikhalifu amri yangu. Kwa amri hii tumetaka kuitimiza neema juu yenu, na Kibla hichi tulicho kuelekezeni ndicho kipelekee kuthibiti kwenu katika uwongofu na kupata tawfiki.

التفاسير:

external-link copy
151 : 2

كَمَآ أَرۡسَلۡنَا فِيكُمۡ رَسُولٗا مِّنكُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِنَا وَيُزَكِّيكُمۡ وَيُعَلِّمُكُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمۡ تَكُونُواْ تَعۡلَمُونَ

Kama tulivyo mtuma Mtume kwenu anaye tokana na nyinyi, anakusomeeni Aya zetu na kukutakaseni na kukufundisheni Kitabu na hikima na kukufundisheni mliyo kuwa hamyajui. info

Na hivi kukuelekezeni kwenye Msikiti Mtakatifu na kwa kuwa tumekutumieni Mtume aliye tokana nanyi, akikusomeeni Aya ni katika kukutimizieni neema yetu, kama tulivyo kutimizieni ile neema - nayo ni Qur'ani - na akusafishieni nafsi zenu zitoke uchafu wa ushirikina na tabia na ada mbovu mbovu, na anakusemezeni kwa njia ya kukufunzeni maarifa ya Qur'ani na ilimu zenye nafuu, na kukufunzeni mambo ambayo mlikuwa hamyajui. Kwani mlikuwa katika ujinga na upotovu ulio mpofu wa kijahilia.

التفاسير:

external-link copy
152 : 2

فَٱذۡكُرُونِيٓ أَذۡكُرۡكُمۡ وَٱشۡكُرُواْ لِي وَلَا تَكۡفُرُونِ

Basi nikumbukeni nitakukumbukeni, na nishukuruni wala msinikufuru. info

Basi enyi Waumini! Nikumbukeni kwa kunit'ii, na Mimi nitakukumbukeni kwa kukupeni thawabu. Na nishukuruni kwa neema nilizo kuvikeni, wala msizipinge neema hizi kwa kuyaasi yale niliyo kuamrisheni.

التفاسير:

external-link copy
153 : 2

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱلصَّبۡرِ وَٱلصَّلَوٰةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Enyi mlio amini! Takeni msaada kwa subira na Swala. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri. info

Na tafuteni kujisaidia, enyi Waumini, katika kila linalo kupateni, kwa kusubiri na kushika Swala. Swala ndio msingi wa ibada zote. Hakika Mwenyezi Mungu kwa uwezo wake wenye nguvu yu pamoja na wanao subiri. Yeye ndiye mlinzi wao, na Yeye ndiye anaye wanusuru daima.

التفاسير: