કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષામાં અનુવાદ - અલી મોહસીન અલ્ બર્વાની

પેજ નંબર:close

external-link copy
253 : 2

۞ تِلۡكَ ٱلرُّسُلُ فَضَّلۡنَا بَعۡضَهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖۘ مِّنۡهُم مَّن كَلَّمَ ٱللَّهُۖ وَرَفَعَ بَعۡضَهُمۡ دَرَجَٰتٖۚ وَءَاتَيۡنَا عِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَأَيَّدۡنَٰهُ بِرُوحِ ٱلۡقُدُسِۗ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقۡتَتَلَ ٱلَّذِينَ مِنۢ بَعۡدِهِم مِّنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ وَلَٰكِنِ ٱخۡتَلَفُواْ فَمِنۡهُم مَّنۡ ءَامَنَ وَمِنۡهُم مَّن كَفَرَۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقۡتَتَلُواْ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَفۡعَلُ مَا يُرِيدُ

MITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu ya wengineo. Katika wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na wengine akawapandisha vyeo. Na tukampa Isa mwana wa Mariyam hoja zilizo wazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana walio kuwa baada yao baada ya kuwajia hoja zilizo wazi. Lakini walikhitalifiana. Basi wapo kati yao walio amini, na wengine kati yao walio kufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana. Lakini Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo. info

Hao ni Mitume ambao baadhi yao tumewataja, wengine tumewatukuza kuliko wenginewe. Wamo kati yao walio semezwa na Mwenyezi Mungu ana kwa ana, kama Musa. Na wengine kati yao Mwenyezi Mungu amewanyanyua kushinda vyeo vya wote, kama Muhammad ambaye akamkhusisha kumpa Ujumbe kwa ulimwengu wote, na kukamilisha Sharia, na kuwa ni Mtume wa mwisho. Na miongoni mwao ni Isa bin Maryam, ambaye Mwenyezi Mungu alimtia nguvu kwa kumpa miujiza kama kufufua wafu, na kuponyesha upofu na ukoma, na akamletea Jibril, Roho Mtakatifu, ili kumtia nguvu. Na Mitume hawa wameleta Uwongofu, na Dini ya Haki, na Ushahidi ulio wazi wenye kuongoa. Kwa haya imewajibikia watu wote wawaamini, wala wasikhitalifiane, wala wasipigane. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasipigane hao watu baada ya kuletewa Mitume na ishara zilizo wazi zenye kuonyesha Haki, pasingetokea kupigana wala kukhitalifiana. Lakini Mwenyezi Mungu hakutaka hayo. Kwa hivyo wakakhitalifiana. Basi kati yao wakawapo walio amini, na wengine walio kufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli uwana wala wasingeli khitalifiana. Bali wangeli kuwa wote katika Haki. Lakini Mwenyezi Mungu hutenda apendalo.

التفاسير:

external-link copy
254 : 2

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَنفِقُواْ مِمَّا رَزَقۡنَٰكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ يَوۡمٞ لَّا بَيۡعٞ فِيهِ وَلَا خُلَّةٞ وَلَا شَفَٰعَةٞۗ وَٱلۡكَٰفِرُونَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Enyi mlio amini! Toeni katika tulivyo kupeni kabla haijafika Siku ambayo hapatakuwapo biashara, wala urafiki, wala uombezi. Na makafiri ndio madhaalimu. info

Enyi mlio muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho! Toeni baadhi ya tuliyo kuruzukuni kwa ajili ya mambo ya kheri. Fanyeni haraka kwa hayo kabla haijafika Siku ya Kiyama ambayo itayo kuwa yote ni ya kheri, wala hazipatikani sababu za kuzozana. Siku hiyo hamwezi kuyadiriki yaliyo kwisha kupiteni duniani, na hapo haitakufaeni biashara, wala urafiki, wala uombezi wa mtu yeyote bila ya idhini ya Mwenyezi Mungu. Na siku hiyo dhulma za makafiri zitadhihiri kwa kuwa hawakuitikia Wito wa Haki.

التفاسير:

external-link copy
255 : 2

ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَيُّ ٱلۡقَيُّومُۚ لَا تَأۡخُذُهُۥ سِنَةٞ وَلَا نَوۡمٞۚ لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ مَن ذَا ٱلَّذِي يَشۡفَعُ عِندَهُۥٓ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيۡءٖ مِّنۡ عِلۡمِهِۦٓ إِلَّا بِمَا شَآءَۚ وَسِعَ كُرۡسِيُّهُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَۖ وَلَا يَـُٔودُهُۥ حِفۡظُهُمَاۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِيُّ ٱلۡعَظِيمُ

Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu. info

Mwenyezi Mungu ndiye anaye stahiki kuabudiwa pekee. Yeye ndiye Mwenye kubaki, Mwenye kuyasimamia mambo ya viumbe daima. Haghafiliki kabisa, wala hanyong'onyei, wala halali wala yanayo fanana na hayo, kwani Yeye hasifiki na upungufu wa chochote. Yeye pekee ndiye Mwenye kumiliki mbingu na ardhi, wala hana mshirika yeyote katika hayo. Kwa hivyo hapana kiumbe anaye weza kumwombea mwenginewe ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Yeye Subhanahu wa Taa'la anajua kila kitu. Anayajua yaliyo kuwa na yatayo kuwa. Hapana mtu anaye weza kujua kitu katika ilimu ya Mwenyezi Mungu ila atakavyo Yeye ajue na aridhie. Utawala wake umeenea mbinguni na ardhini. Hayamhangaishi Yeye kuyadabiri hayo, kwani Yeye ametukuka, hana upungufu wala kushindwa na jambo, Muadhamu katika utukufu wake na utawala wake. Katika haya upo ushahidi wa kuonyesha ujuzi wa Mwenyezi Mungu wa daima, na Kusimamia kwake kusio koma kwa yote ya mbinguni na duniani. Pia pana ishara ya kuwa Mwenyezi Mungu hapitikiwi na vituko vinavyo zuka.Ilimu ya Sayansi imethibitisha kuwa kulala ni katika sifa ya wanyama na mimea iliyo hai. Ikiwa Mwenyezi Mungu halali basi Yeye ni hai kwa uhai ulio elekeana na dhati yake, lakini sio kama vilivyo hai vinginevyo.

التفاسير:

external-link copy
256 : 2

لَآ إِكۡرَاهَ فِي ٱلدِّينِۖ قَد تَّبَيَّنَ ٱلرُّشۡدُ مِنَ ٱلۡغَيِّۚ فَمَن يَكۡفُرۡ بِٱلطَّٰغُوتِ وَيُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱسۡتَمۡسَكَ بِٱلۡعُرۡوَةِ ٱلۡوُثۡقَىٰ لَا ٱنفِصَامَ لَهَاۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. info

Hapana ruhusa kumlazimisha yeyote kuingia katika Dini. Kwa Aya na Ishara zilio zagaa Njia ya Haki imewekwa wazi kutokana na njia ya upotovu. Basi aliye ongoka akafuata Imani na akakataa kufuata chochote kisicho ingia akilini, na kinacho mpelekea kuacha Haki, basi huyo ameshika njia madhbuti kabisa ya kumkinga asiingie katika upotovu, kama yule mwenye kukamata kishikio imara kilicho fungika baraabara kitacho mlinda asitumbukie shimoni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyasikia mnayo yasema, ni Mwenye kuyajua mnayo yatenda, na ni Mwenye kukulipeni kwa vitendo vyenu.

التفاسير: