Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
38 : 2

قُلۡنَا ٱهۡبِطُواْ مِنۡهَا جَمِيعٗاۖ فَإِمَّا يَأۡتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدٗى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Tulisema, “Shukeni kutoka Peponi nyote! Na utawajia, nyinyi na vizazi vyenu vinavyofuatia, ujumbe wenye mambo ya kuwaongoza kwenye haki. Wenye kuufuata huo kwa vitendo, hawatakuwa na hofu kuhusu mustakbala wao wa Akhera, wala hawatakuwa na huzuni juu ya vitu walivyovikosa vya ulimwenguni. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 2

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Na wenye kukataa na kukanusha aya zetu zinazosomwa na dalili za Umoja Wetu, basi hao ndio ambao watasalia Motoni, wakiwa humo milele: hawatatoka humo.” info
التفاسير:

external-link copy
40 : 2

يَٰبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتِيَ ٱلَّتِيٓ أَنۡعَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ وَأَوۡفُواْ بِعَهۡدِيٓ أُوفِ بِعَهۡدِكُمۡ وَإِيَّٰيَ فَٱرۡهَبُونِ

Enyi kizazi cha Ya’qūb, tajeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo nyingi kwenu, nishukuruni na timizeni wasia Wangu kwenu kuwa muviamini Vitabu Vyangu na Mitume Wangu Wote, mfuate Sheria Zangu kivitendo. Mkifanya hivyo, nitawatimizia niliyowaahidi ya kuwarehemu katika ulimwengu na kuwaokoa kesho Akhera. Na Mimi, Peke Yangu, niogopeni na muwe na hadhari na mateso Yangu ikiwa mtavunja ahadi na kunikanusha. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 2

وَءَامِنُواْ بِمَآ أَنزَلۡتُ مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَكُمۡ وَلَا تَكُونُوٓاْ أَوَّلَ كَافِرِۭ بِهِۦۖ وَلَا تَشۡتَرُواْ بِـَٔايَٰتِي ثَمَنٗا قَلِيلٗا وَإِيَّٰيَ فَٱتَّقُونِ

Na iaminini Qur,ani, enyi wana wa Isrāīl, ambayo niliiteremsha kwa Muhammad, aliye Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie yeye, ambayo inalingana na yale mnayoyajua yaliyo sahihi katika Taurati. Na msiwe ni kundi la mwanzo la Watu wa Kitabu (ahl al-kitāb) kuikanusha. Na wala msizibadilishe aya zangu kwa thamani chache ya taka za dunia zenye kuondoka. Na Kwangu Mimi, Peke Yangu, fanyeni vitendo vya kunitii na acheni kuniasi. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 2

وَلَا تَلۡبِسُواْ ٱلۡحَقَّ بِٱلۡبَٰطِلِ وَتَكۡتُمُواْ ٱلۡحَقَّ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Wala msichanganye haki niliyowafafanulia, na batili mliyoizusha. Na jihadharini kuificha haki iliyo wazi ya sifa za Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ambazo zimo ndani ya vitabu vyenu. Na nyinyi mnazipata hizo zimeandikwa kwenu, katika vitabu mnavyovijua vilivyoko mikononi mwenu. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 2

وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱرۡكَعُواْ مَعَ ٱلرَّٰكِعِينَ

Na ingieni kwenye dini ya Uislamu: Msimamishe Swala kwa njia sahihi kama alivyokuja nayo Nabii wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, mtekeleze Zaka za lazima kwa namna iliyowekwa na Sheria, na mue pamoja na wanaorukuu katika ummah wake, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 2

۞ أَتَأۡمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلۡبِرِّ وَتَنسَوۡنَ أَنفُسَكُمۡ وَأَنتُمۡ تَتۡلُونَ ٱلۡكِتَٰبَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Ni ubaya ulioje wa hali yenu na hali ya wasomi wenu, mnapoamrisha watu kufanya mambo ya kheri na kuziacha nafsi zenu, hamziamrishi ziingie kwenye hiyo kheri kubwa, nayo ni Uislamu, na hali nyinyi mnaisoma Taurati ambayo ndani yake muna sifa za Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na ulazima wa kumfuata! Kwani hamzitumii akili zenu kisawa? info
التفاسير:

external-link copy
45 : 2

وَٱسۡتَعِينُواْ بِٱلصَّبۡرِ وَٱلصَّلَوٰةِۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى ٱلۡخَٰشِعِينَ

Jisaidieni, katika mambo yenu, kwa subira za kila aina, na pia kwa Swala ambayo ni ngumu isipokuwa kwa wanyenyekevu. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 2

ٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَٰقُواْ رَبِّهِمۡ وَأَنَّهُمۡ إِلَيۡهِ رَٰجِعُونَ

Wenye kumcha Mwenyezi Mungu na kutaraji Malipo yaliyoko Kwake, wenye kuamini kwa yakini kuwa wao ni wenye kukutana na Mola wao, Aliyetukuka na kushinda, baada ya kufa, na kuwa wao ni wenye kurejea Kwake Siku ya Kiama kwa kuhesabiwa na kulipwa. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 2

يَٰبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتِيَ ٱلَّتِيٓ أَنۡعَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ وَأَنِّي فَضَّلۡتُكُمۡ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

Enyi kizazi cha Ya’qūb! Kumbukeni neema zangu nyingi juu yenu, mnishukuru kwa neema hizo na mkumbuke kuwa Mimi nimewatukuza nyinyi juu ya watu wa zama zenu, kwa wingi wa Mitume na Vitabu vilivyoteremshwa kama Taurati na Injili. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 2

وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا لَّا تَجۡزِي نَفۡسٌ عَن نَّفۡسٖ شَيۡـٔٗا وَلَا يُقۡبَلُ مِنۡهَا شَفَٰعَةٞ وَلَا يُؤۡخَذُ مِنۡهَا عَدۡلٞ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Iogopeni Siku ya Kiama, Siku ambayo hakuna mtu wa kumfaa mwengine kitu chochote, wala Mwenyezi Mungu hatakubali maombezi kwa Makafiri na wala hatakubali kutoka kwao kitu chochote cha kuwakomboa, hata kama kilikuwa ni mali yote yaliyoko ardhini, na hakuna yoyote atakayeweza kujitokeza kuwanusuru wao na kuwaokoa na adhabu. info
التفاسير: