Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
191 : 2

وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ ثَقِفۡتُمُوهُمۡ وَأَخۡرِجُوهُم مِّنۡ حَيۡثُ أَخۡرَجُوكُمۡۚ وَٱلۡفِتۡنَةُ أَشَدُّ مِنَ ٱلۡقَتۡلِۚ وَلَا تُقَٰتِلُوهُمۡ عِندَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَٰتِلُوكُمۡ فِيهِۖ فَإِن قَٰتَلُوكُمۡ فَٱقۡتُلُوهُمۡۗ كَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na waueni wale wanaopigana na nyinyi miongoni mwa Washirikina popote mtakapowakuta, na muwtoe kutoka pahali walipowatoa, napo ni Maka. Na fitina, ambayo ni ukafiri na ushirikina na kuwazuia watu na Uislamu, ni mbaya zaidi kuliko nyinyi kuwaua wao. Wala msiwaanzie vita katika Msikiti wa Haramu, kwa kuheshimu sehemu zake tukufu, mpaka wao wawaanzie vita humo. Na iwapo watawapiga vita katika Msikiti wa Haramu, basi waueni hapo. Mfano wa malipo hayo ya kutisha yatakuwa ndiyo malipo ya Makafiri. info
التفاسير:

external-link copy
192 : 2

فَإِنِ ٱنتَهَوۡاْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na iwapo watayaacha yale walionayo ya ukafiri na ya kuwapigeni vita kwenye Msikiti wa Haramu na wakaingia katika Imani, kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwasamehe waja Wake, ni Mwenye huruma na wao. info
التفاسير:

external-link copy
193 : 2

وَقَٰتِلُوهُمۡ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتۡنَةٞ وَيَكُونَ ٱلدِّينُ لِلَّهِۖ فَإِنِ ٱنتَهَوۡاْ فَلَا عُدۡوَٰنَ إِلَّا عَلَى ٱلظَّٰلِمِينَ

Na endeleeni, enyi Waumini, kuwapiga vita washirikina wafanyao uadui mpaka kusiweko tena kuwafitini Waislamu na dini yao wala kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na ibakie dini kuwa ni ya Mwenyezi Mungu Peke Yake, hali ya kuwa safi, haabudiwi yoyote pamoja na Yeye. Na iwapo watakomeka na ukafiri na vita, basi komekeni nao.Kwani mateso hayawi ela kwa wale wanaoendelea na ukafiri wao na uadui wao. info
التفاسير:

external-link copy
194 : 2

ٱلشَّهۡرُ ٱلۡحَرَامُ بِٱلشَّهۡرِ ٱلۡحَرَامِ وَٱلۡحُرُمَٰتُ قِصَاصٞۚ فَمَنِ ٱعۡتَدَىٰ عَلَيۡكُمۡ فَٱعۡتَدُواْ عَلَيۡهِ بِمِثۡلِ مَا ٱعۡتَدَىٰ عَلَيۡكُمۡۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُتَّقِينَ

Kuwapiga kwenu vita, enyi Waumini, hao washirikina, katika mwezi ambao Mwenyezi Mungu Ameharamisha vita, ni malipo ya wao kuwapiga nyinyi vita mwezi mtukufu.Na yule anayekeuka yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu ya pahali na zama, atapewa mateso yanayofanana na kitendo chake na yanayotokana na jinsi ya kosa alilolifanya. Basi atakayewafanyia uadui kwa vita au chinginecho, wapeni adhabu ifananayo na uovu wao, wala pasiwe na dhiki kwenu kuhusu hilo. kwa sababu wao ndio wenye kuanza uadui. Na muogopeni Mwenyezi Mungu na msipitishe kipimo cha kufanana kuadhibu. Na juenu kuwa Mwenyezi Mungu Yuko pamoja na wale wamchao na wanaomtii kwa kutekeleza Aliyoyafanya faradhi na kuyaepuka Aliyoyafanya haramu. info
التفاسير:

external-link copy
195 : 2

وَأَنفِقُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا تُلۡقُواْ بِأَيۡدِيكُمۡ إِلَى ٱلتَّهۡلُكَةِ وَأَحۡسِنُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na endeleeni, enyi Waumini, kutoa mali kwa kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kupigana jihadi katika njia yake. Wala msiziingize nafsi zenu kwenye maangamivu kwa kuacha jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuacha kutoa katika njia Yake. Na fanyeni wema katika kutoa na kutii, na mzifanye amali zenu zote ni zenye kutakasika kwa kukusudiwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Kwa hakika Mwenyezi Mungu Anawapenda watu wenye kutakasa nia na kufanya wema. info
التفاسير:

external-link copy
196 : 2

وَأَتِمُّواْ ٱلۡحَجَّ وَٱلۡعُمۡرَةَ لِلَّهِۚ فَإِنۡ أُحۡصِرۡتُمۡ فَمَا ٱسۡتَيۡسَرَ مِنَ ٱلۡهَدۡيِۖ وَلَا تَحۡلِقُواْ رُءُوسَكُمۡ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ ٱلۡهَدۡيُ مَحِلَّهُۥۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوۡ بِهِۦٓ أَذٗى مِّن رَّأۡسِهِۦ فَفِدۡيَةٞ مِّن صِيَامٍ أَوۡ صَدَقَةٍ أَوۡ نُسُكٖۚ فَإِذَآ أَمِنتُمۡ فَمَن تَمَتَّعَ بِٱلۡعُمۡرَةِ إِلَى ٱلۡحَجِّ فَمَا ٱسۡتَيۡسَرَ مِنَ ٱلۡهَدۡيِۚ فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ ثَلَٰثَةِ أَيَّامٖ فِي ٱلۡحَجِّ وَسَبۡعَةٍ إِذَا رَجَعۡتُمۡۗ تِلۡكَ عَشَرَةٞ كَامِلَةٞۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمۡ يَكُنۡ أَهۡلُهُۥ حَاضِرِي ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Na tekelezeni Hija na Umra ziwe zimekamilika, zimetakasika na kukusudiwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.Na iwapo kitwazuia, kwenda kuzikamilisha baada ya kuzihirimia, kizuizi chochote, kama adui na ugonjwa, lililo wajibu kwenu ni kuchinja kitakacho kuwa chepesi kwenu miongoni mwa ngamia, ng’ombe, mbuzi au kondoo, hali ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, ili mpate kutoka katika ihramu zenu kwa kunyoa nywele za kichwa au kuzipunguza.Wala msinyoe vichwa vyenu, mkiwa mumezuiwa, mpaka mwenye kuzuiwa amchinje mnyama wake pale pahali alipozuiwa kisha ajitoe kwenye ihramu yake kama alivyochinja Mtume(S.A.W) hapo Hudaibiya kisha akanyoa kichwa chake. Na asiyekuw yule aliyezuiwa, hatachinja mnyama wake mpaka afike ndani ya eneo la tukufu la Maka, ambapo ndipo pahali pake, sku ya idi ambayo ni siku ya kumi na siku zifuatazo za Tashrīq. Na ambaye kati yenu atakuwa mngonjwa au ana udhia katika kichwa chake akawa anahitajia kunyoa, naye yuko kwenye ihramu, basi atanyoa na ni juu yake atoe fidya: afunge siku tatu au awape sadaka masikini sita, kila mmoja nusu pishi ya chakula, au achinje mbudi au kondoo awape mafukara wa eneo tukufu la Maka. Na pindi mtakapo kuwa kwenye hali ya amani na afya, basi atakaye kujistarehesha kwa kufanya Umra ndani ya Hija, nako ni kuihalalishia mambo alioharamhshiwa kwa sababu ya ihramu baada ya kumaliza Umra yake, inampasa kuchinja kiwezekanacho katika wanyama. Na yule aliyekosa mnyama wa kuchinja, itamlazimu afunge siku tatu ndani ya miezi ya Hija na siku saba mtakapo kumaliza amali za Hija na mkarudi kwenu; hizo ni siku kumi kamili, hapana budi kuzifunga.Mnyama huyo wa kuchinjwa, na yale yaliyopasa juu yake ya kufunga, ni kwa yule ambaye watu wake si wakazi wa ardhi tukufu ya Haram. Na muogopeni Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na mujilazimishe kuzitekeleza amri Zake na kujiepusha na Makatazo Yake, na mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni mkali wa mateso kwa yule aendaye kinyume na amri Zake na na kufanya Aliyoyakemea. info
التفاسير: