Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
142 : 2

۞ سَيَقُولُ ٱلسُّفَهَآءُ مِنَ ٱلنَّاسِ مَا وَلَّىٰهُمۡ عَن قِبۡلَتِهِمُ ٱلَّتِي كَانُواْ عَلَيۡهَاۚ قُل لِّلَّهِ ٱلۡمَشۡرِقُ وَٱلۡمَغۡرِبُۚ يَهۡدِي مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Watasema wajinga na madhaifu wa akili, miongoni mwa Mayahudi na mfano wao, wakiwa katika hali ya kufanya maskhara na kupinga, «Ni kitu gani kilichowageuza hawa Waislamu kuacha kibla chao ambacho walikuwa wakisali kukielekea mwanzo wa Uislamu?»(Nacho ni Baitul Maqdis). Waambie, ewe Mtume, «Upande wa Mashariki na wa Magharibi na katikati yake ni milki ya Mwenyezi Mungu. Hapana upande wowote, miongoni mwa pande zote, ulioko nje ya milki Yake. Yeye Anamuongoza Amtakaye, miongoni mwa waja Wake, kumuelekeza njia ya uongofu iliyo sawa.» Katika hayo, pana ujulishaji kwamba mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu, katika kufuata amri Zake, na kwa hivyo, popote tuelekezwapo tutaelekea. info
التفاسير:

external-link copy
143 : 2

وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَٰكُمۡ أُمَّةٗ وَسَطٗا لِّتَكُونُواْ شُهَدَآءَ عَلَى ٱلنَّاسِ وَيَكُونَ ٱلرَّسُولُ عَلَيۡكُمۡ شَهِيدٗاۗ وَمَا جَعَلۡنَا ٱلۡقِبۡلَةَ ٱلَّتِي كُنتَ عَلَيۡهَآ إِلَّا لِنَعۡلَمَ مَن يَتَّبِعُ ٱلرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيۡهِۚ وَإِن كَانَتۡ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى ٱلَّذِينَ هَدَى ٱللَّهُۗ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَٰنَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِٱلنَّاسِ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٞ

Na kama tulivyowaongoza, enyi Waislamu, kwenye njia sahihi katika Dini, tumewafanya kuwa ni ummah bora ulio muadilifu, ili mue mashahidi juu ya ummah waliopita, kesho Akhera, kwamba Mitume wao waliwafikishia jumbe za Mola wao, na ili Mtume, kesho Akhera, awe vilevile ni shahidi juu yenu, kwamba yeye aliwafikishia ujumbe wa Mola wake. Wala hatukukifanya, ewe Mtume, kile kibla cha Baitul Maqdis ulichokuwa ukikielekea, kisha tukakugeuza tukakuelekeza Alkaba (iliyopo Makkah) isipokuwa ni yapate kuonekana yale tuliyoyajua hapo kale, ujuzi unaofungamana na thawabu na adhabu, ili tumtenganishe yule ambaye atakufuata na kukutii na kuelekea pamoja nawe pale utakapoelekea na yule aliye dhaifu wa imani, awe ni mwenye kubadilika na kuritadi kwa kuacha Dini yake kwa shaka yake na unafiki wake. Hali hii ya kugeuka Muislamu katika Swala yake, kuacha kuelekea Baitul Maqdis na kuelekea Alkaba ni ngumu na nzito, isipokuwa kwa wale walioongozwa na Mwenyezi Mungu na kupewa neema ya Imani na uchajimungu. Na wala hakuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupoteza imani yenu Kwake na kumfuata kwenu Mtume Wake kwa kuzibatilisha Swala zenu mlipokuwa mnaelekea kibla cha zamani. Hakika Yeye Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na upungufu wowote na Aliyetukuka, kwa watu ni Mpole na Mwenye huruma. info
التفاسير:

external-link copy
144 : 2

قَدۡ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجۡهِكَ فِي ٱلسَّمَآءِۖ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبۡلَةٗ تَرۡضَىٰهَاۚ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَحَيۡثُ مَا كُنتُمۡ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ شَطۡرَهُۥۗ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ لَيَعۡلَمُونَ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا يَعۡمَلُونَ

Hakika Tunauona mzunguko wa uso wako upande wa mbinguni mara baada ya mara, huku ukingojea kuteremka Wahyi juu yako kuhusiana na Kibla. Basi hakika Tutakuepusha na Baitul Maqdis Tukuelekeze kwenye kibla unachokipenda na unachokiridhia, nacho ni upande wa Msikiti wa Ḥarām ulioko Makkah. Basi, elekeza uso wako huko. Na popote mtakapokuwa, enyi Waislamu, na mkataka kuswali, elekeeni upande wa Msikiti wa Haram. Na hakika wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa elimu ya Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara wanajua kwamba kugeuzwa kwako kuelekezwa Alkaba ndio haki iliyothibiti katika vitabu vyao. Na wala Mwenyezi Mungu hakuwa ni Mwenye kughafilika juu ya yale wayafanyayo hawa wapinzani wenye shaka, na Atawalipa kwayo. info
التفاسير:

external-link copy
145 : 2

وَلَئِنۡ أَتَيۡتَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ بِكُلِّ ءَايَةٖ مَّا تَبِعُواْ قِبۡلَتَكَۚ وَمَآ أَنتَ بِتَابِعٖ قِبۡلَتَهُمۡۚ وَمَا بَعۡضُهُم بِتَابِعٖ قِبۡلَةَ بَعۡضٖۚ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم مِّنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ إِنَّكَ إِذٗا لَّمِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Na lau utawaletea wale waliopewa Taurati na Injili aina yoyote ya hoja na dalili kwamba kuelekea kwako Alkaba katika swala ndio haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hawangalikifuata kibla chako, kwa inadi na kiburi. Na wala wewe si mwenye kukifuata kibla chao mara nyingine. Wala baadhi yao si wenye kufuata kibla cha baadhi yao. Na lau utafuata matamanio ya nafsi zao kuhusu kibla na mengineyo, baada ya ujuzi uliyoupata kuwa wewe uko kwenye haki na wao wako kwenye batili, wewe wakati huo utakuwa ni miongoni mwa waliozidhulumu nafsi zao. Haya ni maelezo kuambiwa ummah wote, na ni kitisho na kemeo kwa kila afuataye matamanio ya wanaoenda kinyume na Sheria ya Kiislamu. info
التفاسير: