Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
70 : 2

قَالُواْ ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ إِنَّ ٱلۡبَقَرَ تَشَٰبَهَ عَلَيۡنَا وَإِنَّآ إِن شَآءَ ٱللَّهُ لَمُهۡتَدُونَ

Wana wa Isrāīl walimwambia Mūsā, “Tuombee Mola wako Atufafanulie sifa zake nyingine zisizokuwa zilizotangulia. Sababu ng’ombe wenye sifa hizi ni wengi. Kwa hivyo, tumechanganyikiwa hatujui tuchague yupi. Na sisi, Mwenyezi Mungu Anapotaka, tutaongokea kumjua ng’ombe ambaye ilitolewa amri achinjwe.” info
التفاسير:

external-link copy
71 : 2

قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٞ لَّا ذَلُولٞ تُثِيرُ ٱلۡأَرۡضَ وَلَا تَسۡقِي ٱلۡحَرۡثَ مُسَلَّمَةٞ لَّا شِيَةَ فِيهَاۚ قَالُواْ ٱلۡـَٰٔنَ جِئۡتَ بِٱلۡحَقِّۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُواْ يَفۡعَلُونَ

Mūsā aliwaambia, “Mwenyezi Mungu Anasema kwamba huyo ni ng’ombe asiyetumiwa kwa kazi ya kulima ardhi ya kilimo, hakutayarishwa kutia maji, hana kasoro yoyote na hana alama yoyote ya rangi isiyokuwa rangi ya ngozi yake.” Wakasema, “Sasa umekuja na ukweli wa sifa ya ng’ombe.” Wakalazimika kumchinja baada ya muda mrefu wa mbinu za kuchelewesha. Na walikuwa karibu kutofanya hilo kwa ushindani wao. Hivi ndivyo walivyojitilia mkazo, ndipo Mwenyezi Mungu Akawafanyia mkazo. info
التفاسير:

external-link copy
72 : 2

وَإِذۡ قَتَلۡتُمۡ نَفۡسٗا فَٱدَّٰرَٰءۡتُمۡ فِيهَاۖ وَٱللَّهُ مُخۡرِجٞ مَّا كُنتُمۡ تَكۡتُمُونَ

Na Kumbukeni, mlipomuua mtu, mkabishana kuhusu yeye, akawa kila mmoja ajiepushia nafsi yake tuhuma ya kuua na hali Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyafichua yale ambayo mlikuwa mkiyaficha kuhusu kifo cha yule aliyeuawa. info
التفاسير:

external-link copy
73 : 2

فَقُلۡنَا ٱضۡرِبُوهُ بِبَعۡضِهَاۚ كَذَٰلِكَ يُحۡيِ ٱللَّهُ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَيُرِيكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Tukasema, “Mpigeni aliyeuliwa kwa sehemu ya yule ng’ombe aliyechinjwa, Mwenyezi Mungu atamfufua akiwa hai na atawaambia muuaji wake ni nani.” Basi wakampiga kwa ile sehemu ya ng’ombe, Mwenyezi Mungu Akamhuisha na akamtaja muuaji wake. Hivyo ndivyo Anavyohuisha Mwenyezi Mungu wafu Siku ya Kiyama na kuwaonyesha nyinyi, Wana wa Isrāīl, miujiza Yake yenye dalili ya ukamilifu wa uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, ili mfikiri kwa akili zenu mpate kujiepusha na vitendo vya kumuasi. info
التفاسير:

external-link copy
74 : 2

ثُمَّ قَسَتۡ قُلُوبُكُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَٱلۡحِجَارَةِ أَوۡ أَشَدُّ قَسۡوَةٗۚ وَإِنَّ مِنَ ٱلۡحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنۡهُ ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ وَإِنَّ مِنۡهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخۡرُجُ مِنۡهُ ٱلۡمَآءُۚ وَإِنَّ مِنۡهَا لَمَا يَهۡبِطُ مِنۡ خَشۡيَةِ ٱللَّهِۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Lakini nyinyi hamkufaidika na hilo. Kwani baada ya miujiza yote hii yenye kupita mipaka ya uwezo wa kiumbe, nyoyo zenu zilikuwa ngumu na shupavu kwa namna ambayo hakuna kheri iliopenyeza ndani, na hazikulainika mbele ya miujiza yenye kushinda niliyowaonesha, mpaka nyoyo zenu zikafikia hadi ya kuwa ni kama jiwe gumu, bali zililishinda jiwe kwa ugumu wake. Kwani miongoni mwa mawe kuna yanayopanuka na kutoboka na maji yakabubujika kwa wingi kutoka humo mpaka yakawa ni mito yenye kupata. Na miongoni mwayo kuna yanayofanya nyufa, yakapasuka na kuchimbuka maji ya chemchemi na mikondo. Na miongoni mwayo kuna yanayoanguka kutoka juu ya milima kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kumuadhimisha. Na Mwenyezi Mungu Hakuwa ni Mwenye kughafilika kwa mnayoyafanya. info
التفاسير:

external-link copy
75 : 2

۞ أَفَتَطۡمَعُونَ أَن يُؤۡمِنُواْ لَكُمۡ وَقَدۡ كَانَ فَرِيقٞ مِّنۡهُمۡ يَسۡمَعُونَ كَلَٰمَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُۥ مِنۢ بَعۡدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ

Enyi waislamu! Kwani mumesahau vitendo vya Wana wa Isrāīl, ndipo nafsi zenu zikawa na tamaa kuwa Mayahudi wataiamini dini yenu? Wanavyuoni wao walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu ya Taurati, kisha wakiyapotoa kwa kuyageuza na kuyapa maana yasiyo sahihi baada ya kuyafahamu maana yake ya kweli, au kwa kuyageuza matamshi yake, hali wanajua kuwa wao wanayapotoa maneno ya Mwenyezi Mungu kwa kusudi na urongo. info
التفاسير:

external-link copy
76 : 2

وَإِذَا لَقُواْ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٖ قَالُوٓاْ أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ ٱللَّهُ عَلَيۡكُمۡ لِيُحَآجُّوكُم بِهِۦ عِندَ رَبِّكُمۡۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Hawa Mayahudi, wakikutana na Waumina, wanasema kwa ndimi zao, “Tumeamini dini yenu na Mtume wenu aliyebashiriwa katika Taurati.” Na wakiwa faragha, wao kwa wao, hawa wanafiki wa kiyahudi, huwa wakiambiana kwa njia ya kukemeana, “Vipi nyinyi mnawahadithia Waumini yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewabainishia katika Taurati kuhusu Muhammad, mkawapa hoja juu yenu mbele ya Mola wenu Siku ya Kiyama? Kwani hamfahamu mkajihadhari?” info
التفاسير: