Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
146 : 2

ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَعۡرِفُونَهُۥ كَمَا يَعۡرِفُونَ أَبۡنَآءَهُمۡۖ وَإِنَّ فَرِيقٗا مِّنۡهُمۡ لَيَكۡتُمُونَ ٱلۡحَقَّ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ

Wale Tuliowapa Taurati na Injili miongoni mwa wanavyuoni wa Kiyahudi na wajuzi wa Kinaswara wanajua ya kwamba Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa sifa zake zilizotajwa katika vitabu vyao, kama vile wanavyowajuwa wana wao. Na hakika kuna kundi kati yao wanaificha haki na wao wanaujuwa ukweli wake na kuwa sifa zake zimethibiti. info
التفاسير:

external-link copy
147 : 2

ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ

Yale yaliyoteremshwa kwako, ewe Nabii, ndiyo haki kutoka kwa Mola wako. Kwa hivyo, usiwe ni kati ya wale wanaoyatilia shaka. Maneno haya, ingawa anambiwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, yanaelekezwa kwa ummah wote. info
التفاسير:

external-link copy
148 : 2

وَلِكُلّٖ وِجۡهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَاۖ فَٱسۡتَبِقُواْ ٱلۡخَيۡرَٰتِۚ أَيۡنَ مَا تَكُونُواْ يَأۡتِ بِكُمُ ٱللَّهُ جَمِيعًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Kila ummah, miongoni mwa ummah wa kila aina, una kibla chake anachokielekea kila mmoja katika wao kwenye swala yake. Basi kimbilieni, enyi Waumini, hali ya kushindana katika kutenda vitendo vyema ambavyo Ameviwajibisha kwenu Mwenyezi Mungu katika Dini ya Kiislamu. Mwenyezi Mungu Atawakusanya nyote Siku ya Kiyama kutoka popote mtakapokuwa. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. info
التفاسير:

external-link copy
149 : 2

وَمِنۡ حَيۡثُ خَرَجۡتَ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۖ وَإِنَّهُۥ لَلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Na mahali popote ulipotoka, ewe Nabii, ukiwa msafiri au ukitaka kuswali, elekeza uso wako upande wa Msikiti wa Haram. Kuelekea kwako huko ndio haki iliyothibiti kutoka kwa Mola wako. Na Mwenyezi Mungu hakuwa ni Mwenye kughafilika juu ya yale mnayoyatenda na Atawalipa kwa hayo. info
التفاسير:

external-link copy
150 : 2

وَمِنۡ حَيۡثُ خَرَجۡتَ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَحَيۡثُ مَا كُنتُمۡ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ شَطۡرَهُۥ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيۡكُمۡ حُجَّةٌ إِلَّا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِي وَلِأُتِمَّ نِعۡمَتِي عَلَيۡكُمۡ وَلَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ

Na mahali popote utokapo, ewe Nabii, elekea Msikiti wa Haram. Na popote mnapokuwa, enyi Waislamu, katika nchi yoyote miongoni mwa nchi za ardhi, elekezeni nyuso zenu upande wa Msikiti wa Haram, ili watu wapinzani wasiwe na hoja yoyote kwenu kwa njia ya ugomvi na mjadala, baada ya kuelekea huko, isipokuwa wale madhalimu na wenye ukaidi kati yao. Hao watabakia kwenye mjadala wao. Basi, msiwaogope wao, niogopeni Mimi kwa kufuata amri Yangu na kujiepusha na katazo Langu na ili nikamilishe neema Zangu kwenu kuwachagulia sheria zilizokamilika zaidi, na ili mpate kuongoka kufuata haki na usawa. info
التفاسير:

external-link copy
151 : 2

كَمَآ أَرۡسَلۡنَا فِيكُمۡ رَسُولٗا مِّنكُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِنَا وَيُزَكِّيكُمۡ وَيُعَلِّمُكُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمۡ تَكُونُواْ تَعۡلَمُونَ

Kama Tulivyowaneemesha kwa kuelekea Alkaba, Tumewaletea mjumbe anayetokana na nyinyi, anawasomea aya zibainishazo haki kuitenga na batili, kuwasafisha na uchafu wa ushirikina na tabia mbaya, kuwafundisha Kitabu, Sunna na hukumu za Sheria na kuwafundisha habari za Mitume na visa vya ummah waliopita, mambo ambayo mlikuwa hamyajui. info
التفاسير:

external-link copy
152 : 2

فَٱذۡكُرُونِيٓ أَذۡكُرۡكُمۡ وَٱشۡكُرُواْ لِي وَلَا تَكۡفُرُونِ

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amewaamrisha Waumini wamtaje Yeye na Akatoa ahadi kwa hilo malipo bora zaidi, nayo ni kumsifu yule anayemtaja Yeye mbele ya viumbe walioko juu. Pia Amewaamrisha Waumini wamshukuru Yeye Peke Yake kwa maneno na vitendo na wasizikanushe neema Zake juu yao. info
التفاسير:

external-link copy
153 : 2

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱلصَّبۡرِ وَٱلصَّلَوٰةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Enyi Waumini, takeni msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yenu yote, kwa kusubiri juu ya mikasa na misiba, na kuacha maasia na madhambi na kusubiri juu ya kufanya mambo ya utiifu na yale yanayomkurubisha mtu kwa Mola wake, na kwa Swala ambayo kwayo nafsi inapata utulivu na ambayo inakataza machafu na maovu. Hakika Mwenyezi Mungu Yuko pamoja na wenye kusubiri kwa msaada Wake, taufiki Yake na muelekezo Wake. Katika hii Aya kuna kuthibitisha kuwa Mwenyezi Mungu Yuko pamoja na Waumini kimahsusi, upamoja unaolazimiana na yaliyotangulia kutajwa. Ama kuwa Mwenyezi Mungu yuko pamoja na viumbe kijumla kunakolazimiana na elimu Yake na kuwa ujuzi Wake umezunguka kila kitu, basi upamoja huo ni wa viumbe vyote. info
التفاسير: