Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
253 : 2

۞ تِلۡكَ ٱلرُّسُلُ فَضَّلۡنَا بَعۡضَهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖۘ مِّنۡهُم مَّن كَلَّمَ ٱللَّهُۖ وَرَفَعَ بَعۡضَهُمۡ دَرَجَٰتٖۚ وَءَاتَيۡنَا عِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَأَيَّدۡنَٰهُ بِرُوحِ ٱلۡقُدُسِۗ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقۡتَتَلَ ٱلَّذِينَ مِنۢ بَعۡدِهِم مِّنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ وَلَٰكِنِ ٱخۡتَلَفُواْ فَمِنۡهُم مَّنۡ ءَامَنَ وَمِنۡهُم مَّن كَفَرَۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقۡتَتَلُواْ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَفۡعَلُ مَا يُرِيدُ

Mitume hawa watukufu, Mwenyezi Mungu Amewatukuza baadhi yao juu ya wengine, kulingana na neema za Mwenyezi Mungu juu yao. Miongoni mwao kuna ambao Mwenyezi Mungu Amesema nao, kama Mūsā na Muhammad, rehema na amani ziwashukie. Katika hili pana kuthibitisha sifa ya kusema kwa Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka, kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake. Na miongoni mwao kuna ambao Mwenyezi Mungu Aliwainua daraja nyingi za juu, kama Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa kuenea ujumbe wake, kutia kikomo cha unabii kwake, kwa kuwatukuza ummah wake juu ya ummah wengine na yasiyokuwa hayo. Na Mwenyezi Mungu Alimpa 'Īsā mwana wa Maryam, amani imshukie, hoja zilizo wazi, ambazo ni miujiza yenye kushinda, kama kumponya aliyezaliwa kipofu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na kumponya mwenye barasi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kama kuhuisha kwake waliokufa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu Alimpa nguvu kwa Jibrili, amani imshukie. Na lau Mwenyezi Mungu Alitaka wasipigane hao waliokuja baada ya hawa Mitume, baada ya kuwafunukia wao hoja zilizo wazi, hawangalipigana. Lakini ilitokea tafauti baina yao: katika wao kuna aliyejikita kwenye Imani yake, na katika wao kuna aliyeshikilia kukanusha. Na lau Mwenyezi Mungu Alitaka, baada ya hizo tafauti zilizotokea zilizopelekea kupigana, hawangalipigana, lakini Mwenyezi Mungu Anampa taufik ya kumtii Yeye na kumuamini Anayemtaka, na Anamuondolea taufiki Yake Anayemtaka akamuasi na kumkanusha, Kwani Yeye Anafanya na kuchagua Analolitaka. info
التفاسير:

external-link copy
254 : 2

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَنفِقُواْ مِمَّا رَزَقۡنَٰكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ يَوۡمٞ لَّا بَيۡعٞ فِيهِ وَلَا خُلَّةٞ وَلَا شَفَٰعَةٞۗ وَٱلۡكَٰفِرُونَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na kumsadiki Mtume Wake na kufanya amali zinazoambatana na uongofu Wake! Toeni Zaka zilizofaradhiwa na mtoe sadaka ya vitu mlivyopewa na Mwenyezi Mungu kabla haijaja Siku ya Kiyama, wakati ambapo hakuna kuuziana ikapatikana faida, wala mali ambayo nyinyi mtajikomboa nayo nafsi zenu kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala urafiki wa rafiki wenye kuwaokoa, wala muombezi anayemiliki kuwafanya mpunguziwe adhabu. Na makafiri ndio madhalimu na wakeukaji mipaka ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
255 : 2

ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَيُّ ٱلۡقَيُّومُۚ لَا تَأۡخُذُهُۥ سِنَةٞ وَلَا نَوۡمٞۚ لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ مَن ذَا ٱلَّذِي يَشۡفَعُ عِندَهُۥٓ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيۡءٖ مِّنۡ عِلۡمِهِۦٓ إِلَّا بِمَا شَآءَۚ وَسِعَ كُرۡسِيُّهُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَۖ وَلَا يَـُٔودُهُۥ حِفۡظُهُمَاۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِيُّ ٱلۡعَظِيمُ

Mwenyezi Mungu Ndiye Ambaye hakuna yoyote anayestahiki uungu na kuabudiwa isipokua Yeye. Ndiye Aliye hai Ambaye Amekusanya maana yote ya uhai mkamilifu unaolingana na utukufu Wake. Ndiye Msimamizi wa kila kitu. Kusinzia hakumshiki wala kulala. Kila kilichoko kwenye mbingu na kilichoko kwenye ardhi ni milki Yake. Na hatajasiri mtu yoyote kuombea mbele Yake isipokuwa kwa ruhusa Yake. Ujuzi Wake umevizunguka vitu vyote vilivyopita, vilivyoko na vitakavyo kuja. Anajua yaliyo mbele ya viumbe katika mambo ambayo yatakuja na yaliyo nyuma yao katika mambo yaliyopita. Na hakuna yoyote, katika viumbe, mwenye kuchungulia chochote katika elimu Yake isipokuwa kadiri ile ambayo Menyezi Mungu Amemjulisha na kumuonesha. Kursiy Yake imeenea kwenye mbingu na ardhi. Kursiy ni mahali pa nyayo za Mola, uliyo mkubwa utukufu Wake, na hakuna ajuwae namna ilivyo isipokuwa ni Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Wala hakumlemei Mwenyezi Mungu Aliyetakata kuzitunza. (hizo mbingu na ardhi).Yeye Ndiye Aliye juu ya viumbe Vyake vyote, kwa dhati Yake na sifa Zake, Aliyekusanya sifa za utukufu na kiburi. Aya hii ni aya tukufu zaidi katika Qur’ani, na inaitwa Āyah al- Kursīy. info
التفاسير:

external-link copy
256 : 2

لَآ إِكۡرَاهَ فِي ٱلدِّينِۖ قَد تَّبَيَّنَ ٱلرُّشۡدُ مِنَ ٱلۡغَيِّۚ فَمَن يَكۡفُرۡ بِٱلطَّٰغُوتِ وَيُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱسۡتَمۡسَكَ بِٱلۡعُرۡوَةِ ٱلۡوُثۡقَىٰ لَا ٱنفِصَامَ لَهَاۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Kwa kuwa Dini hii imekamilika na hoja zake ziko wazi, haihitajii ilazimishwe kwa watu ambao jizya (jizyah) inapokewa kutoka kwao. Kwani dalili ziko wazi ambazo kwa dalili hizo inabainika haki, ikawa kando na batili, na uongofu, ukawa kando na upotevu. Basi mwenye kukanusha vyote vinavyoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu na akamuamini Mwenyezi Mungu, huwa amethibiti na kulingana kwenye njia bora na ameshikamana na kamba imara ya Dini isiyokatika. Na Mwenyezi Mungu ni Msikizi wa maneno ya waja Wake, ni Mjuzi wa nia zao na vitendo vyao na Atawalipa kwa hayo. info
التفاسير: