Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
187 : 2

أُحِلَّ لَكُمۡ لَيۡلَةَ ٱلصِّيَامِ ٱلرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَآئِكُمۡۚ هُنَّ لِبَاسٞ لَّكُمۡ وَأَنتُمۡ لِبَاسٞ لَّهُنَّۗ عَلِمَ ٱللَّهُ أَنَّكُمۡ كُنتُمۡ تَخۡتَانُونَ أَنفُسَكُمۡ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡ وَعَفَا عَنكُمۡۖ فَٱلۡـَٰٔنَ بَٰشِرُوهُنَّ وَٱبۡتَغُواْ مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَكُمۡۚ وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ ٱلۡخَيۡطُ ٱلۡأَبۡيَضُ مِنَ ٱلۡخَيۡطِ ٱلۡأَسۡوَدِ مِنَ ٱلۡفَجۡرِۖ ثُمَّ أَتِمُّواْ ٱلصِّيَامَ إِلَى ٱلَّيۡلِۚ وَلَا تُبَٰشِرُوهُنَّ وَأَنتُمۡ عَٰكِفُونَ فِي ٱلۡمَسَٰجِدِۗ تِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِ فَلَا تَقۡرَبُوهَاۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ ءَايَٰتِهِۦ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ

Amewahalalishia Mwenyezi Mungu masiku ya mwezi wa Ramadhani kuwaingilia wake zenu. Wao ni sitara na hifadhi kwenu, na nyinyi ni sitara na hifadhi kwao. Anajua Mwenyezi Mungu kwamba nyinyi mulikuwa mkizidhiki nafsi zenu kwa kuenda kinyume na yale ambayo Mwenyezi Mungu Aliyaharimisha kwenu ya kuwaingilia wanawake baada ya Isha katika masiku ya kufunga- hilo lilikuwa mwanzo wa Uislamu-, Mwenyezi Mungu Alikubali toba yenu na Akawatolea nafasi kwa hili jambo. Basi sasa waingilieni na mtafute kile Alichowakadiria Mwenyezi Mungu, miongoni mwa watoto, na kuleni na kunyweni mpaka ujitokeze kwenu mwangaza wa asubuhi utengane na weusi wa usiku kwa kujitokeza alfajiri ya kweli. Kisha kamilisheni kufunga kwa kujizuia na venye kutangua mpaka kuingia usiku kwa kutwa jua. Wala musiwaingilie wake zenu, au kufanya kitu cha kusababisha kuwaingilia, iwapo muko kwenye itikafu misikitini, sababu hilo laharibu itikafu- nako ni kukaa msikitini kwa muda maalumu kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka-. Hukumu hizo, ambazo mwenyezi Mungu Amezifanya ni Sheria kwenu, ndiyo mipaka Yake itenganishayo kati ya halali na haramu. Basi msiikaribie, ili msije mkaingia katika haramu. Kwa mfano wa ubainifu huu ulio wazi, Mwenyezi Mungu Anazifafanua aya Zake na hukumu Zake kwa watu, ili wamche na kumuogopa. info
التفاسير:

external-link copy
188 : 2

وَلَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَكُم بَيۡنَكُم بِٱلۡبَٰطِلِ وَتُدۡلُواْ بِهَآ إِلَى ٱلۡحُكَّامِ لِتَأۡكُلُواْ فَرِيقٗا مِّنۡ أَمۡوَٰلِ ٱلنَّاسِ بِٱلۡإِثۡمِ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Na wasile baadhi yenu mali ya wengine kwa njia ya batili, kama kuapa yamini la urongo, kunyang’anya, kuiba, kuhonga, kula riba na mfano wa hayo.Wala msipeleke kwa mahakimu hoja potofu ili mpate kula kwa njia ya utesi mali ya kikundi cha watu wengine kwa njia ya batili, hali ya kuwa nyinyi mnajua uharamu wa hilo juu yenu. info
التفاسير:

external-link copy
189 : 2

۞ يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡأَهِلَّةِۖ قُلۡ هِيَ مَوَٰقِيتُ لِلنَّاسِ وَٱلۡحَجِّۗ وَلَيۡسَ ٱلۡبِرُّ بِأَن تَأۡتُواْ ٱلۡبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَٰكِنَّ ٱلۡبِرَّ مَنِ ٱتَّقَىٰۗ وَأۡتُواْ ٱلۡبُيُوتَ مِنۡ أَبۡوَٰبِهَاۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Wanakuuliza watu wako, ewe Nabii, kuhusu miezi michanga na kubadilika hali zake. Waambie, Mwenyezi Mungu Ameifanya miezi kuwa ni alama za watu kujua nyakati za ibada zao zilizowekewa wakati, mfano wa Saumu na Hija, na nyakati za kuamiliana kwao. Kheri haiko katika mambo mliyoyazowea wakati wa ujahilia na mwanzo wa Uislamu ya kuingia majumbani kupitia kwa nyuma, wakati mnapotia nia ya Hija au ya Umra, mkidhani kwamba huko ndiko kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Lakini kheri ni kile kitendo cha mwenye kumcha Mwenyezi Mungu na akajiepusha na maasia. Na ingieni majumbani kupitia kwenye milango yake wakati mnapohirimia Hija au Umra. Na muogopeni Mwenyezi Mungu katika mambo yenu yote ili mupate kufaulu kuyapata yote mnayoyapenda ya kheri ya dunia na ya Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
190 : 2

وَقَٰتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ يُقَٰتِلُونَكُمۡ وَلَا تَعۡتَدُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُعۡتَدِينَ

Na piganeni, enyi Waumini, ili kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu, na wale wanaopigana na nyinyi, wala msifanye yaliyokatazwa ya kukatakata viungo, kufanya hiyana (ya kuchukua kitu katika ngawira kabla ya kugawanywa), kumuua asiyefaa kuuawa miongoni mwa wanawake, watoto, wazee na wanaoingia kwenye hukumu yao. Hakika Mwenyezi Mungu Hawapendi wale wanaokiuka mipaka Yake na kuyahalalisha yalioharamishwa na Mewnyezi Mungu na Mtume Wake. info
التفاسير: