Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
265 : 2

وَمَثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمُ ٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِ ٱللَّهِ وَتَثۡبِيتٗا مِّنۡ أَنفُسِهِمۡ كَمَثَلِ جَنَّةِۭ بِرَبۡوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٞ فَـَٔاتَتۡ أُكُلَهَا ضِعۡفَيۡنِ فَإِن لَّمۡ يُصِبۡهَا وَابِلٞ فَطَلّٞۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ

Na mfano wa wale ambao wanatoa mali yao kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kwa kuwa na itikadi iliyojikita ya kuwa ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli, ni kama mfano wa bustani kubwa iliyoko kwenye ardhi ya juu iliyo nzuri iliyonyeshewa na mvua nyingi, yakaongezeka kwa wingi matunda yake. Na hata kama haingalinyeshewa na mvua nyingi, rasharasha la mvua lingalitosha kuifanya itoe ongezeko lingi la matunda. Basi hivyo ndivyo ulivyo utoaji wa watu wenye ikhlasi; amali zao zinakubaliwa mbele ya Mwenyezi Mungu na kuongezwa, ziwe ni chache au ni nyingi. Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kuchungulia siri, Ndiye Mwenye kuyaona ya nje na ya ndani, Anampa thawabu kila mtu kulingana na ikhlasi yake. info
التفاسير:

external-link copy
266 : 2

أَيَوَدُّ أَحَدُكُمۡ أَن تَكُونَ لَهُۥ جَنَّةٞ مِّن نَّخِيلٖ وَأَعۡنَابٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ لَهُۥ فِيهَا مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ وَأَصَابَهُ ٱلۡكِبَرُ وَلَهُۥ ذُرِّيَّةٞ ضُعَفَآءُ فَأَصَابَهَآ إِعۡصَارٞ فِيهِ نَارٞ فَٱحۡتَرَقَتۡۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُمۡ تَتَفَكَّرُونَ

Je anapendelea mmoja wenu awe na bustani yenye mitende na mizabibu, ambayo inapita chini ya miti yake maji tamu, na ndani yake ana kila aina ya matunda, na amefikia hali ya ukongwe ya kutoweza kupanda mimea kama hii, na ana watoto wadogo wanaohitaji bustani hii, na katika hali hii ukavuma upepo mkali uchomao, ukaja ukaiteketeza? Hivi ndivyo hali ya wasio na ikhlasi kataka utoaji wao; watakuja Siku ya Kiyama na hawana jema lolote lao. Kwa ufafanuzi huu, Mwenyezi Mungu Anawabainishia mambo yanayowafaa nyinyi, ili mtaamali na kumtakasia Mwenyezi Mungu utoaji wenu. info
التفاسير:

external-link copy
267 : 2

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَنفِقُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا كَسَبۡتُمۡ وَمِمَّآ أَخۡرَجۡنَا لَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِۖ وَلَا تَيَمَّمُواْ ٱلۡخَبِيثَ مِنۡهُ تُنفِقُونَ وَلَسۡتُم بِـَٔاخِذِيهِ إِلَّآ أَن تُغۡمِضُواْ فِيهِۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ

Enyi mlioniamini na mkawafuata Mitume wangu, toeni miongoni mwa halali mliyoichuma na ile tuliyowatolea kutoka kwenye ardhi. Na wala msikusudie kutoa kibaya, katika hiyo halali, kuwapa mafukara, ambacho lau nyinyi mngalipewa, hamngalikipokea isipokuwa mkiwa mtapuuza ubaya na upungufu ulionacho. Ni vipi nyinyi mnaridhika kumpa Mwenyezi Mungu kitu ambacho hamridhiki nacho mkipewa? Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu Aliyewaruzuku Anajitosha kutohitajia sadaka zenu, ni Mstahiki wa kusifiwa na Mhimidiwa kwa kila hali. info
التفاسير:

external-link copy
268 : 2

ٱلشَّيۡطَٰنُ يَعِدُكُمُ ٱلۡفَقۡرَ وَيَأۡمُرُكُم بِٱلۡفَحۡشَآءِۖ وَٱللَّهُ يَعِدُكُم مَّغۡفِرَةٗ مِّنۡهُ وَفَضۡلٗاۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ

Uchoyo huu na kuchagua kibaya kukitoa sadaka yatokana na Shetani ambaye anawaogopesha nyinyi ufukara na kuwahimiza uchoyo, na anawaamrisha nyiyi maasia na kumfanyia kinyume Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na kutukuka, Anawaahidi nyinyi, kwa kutoa kwenu, msamaha wa madhambi yenu na riziki kundufu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nyongeza zenye kuenea, ni Mjuzi wa nia na vitendo. info
التفاسير:

external-link copy
269 : 2

يُؤۡتِي ٱلۡحِكۡمَةَ مَن يَشَآءُۚ وَمَن يُؤۡتَ ٱلۡحِكۡمَةَ فَقَدۡ أُوتِيَ خَيۡرٗا كَثِيرٗاۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّآ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ

Mwenyezi Mungu Anampa taufiki ya usawa katika kunena na kutenda Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na yoyote ambaye Mwenyezi Mungu Amemneemesha kwa hilo, Hua Amempa kheri nyingi. Na hatakumbuka hilo na kunufaika nalo isipokuwa wenye akili zenye kung’ara kwa nuru ya Mwenyezi Mungu na uongofu Wake. info
التفاسير: