Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
135 : 2

وَقَالُواْ كُونُواْ هُودًا أَوۡ نَصَٰرَىٰ تَهۡتَدُواْۗ قُلۡ بَلۡ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِـۧمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Na Mayahudi walisema kuwaambia ummah wa Mtume Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie yeye, “Ingieni kwenye dini ya Kiyahudi mtapata uongofu. Na Wanaswara waliwaambia kama hayo. Waambie, ewe Mtume, “Uongofu ni kuwa sote tufuate Mila ya Ibrāhīm ambaye alijiepusha na kila dini ya ubatilifu na kufuata Dini ya haki, na hakuwa ni miongoni mwa waliomshirikisha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.” info
التفاسير:

external-link copy
136 : 2

قُولُوٓاْ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡنَا وَمَآ أُنزِلَ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَمَآ أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَآ أُوتِيَ ٱلنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمۡ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّنۡهُمۡ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ

Semeni, enyi Waumini, kuwaambia Mayahudi na Wanaswara, “Tumemuamini Mwenyezi Mungu, Aliye Mmoja, Anayeabudiwa kwa haki; na tumeiamini Qur’ani tuliyoteremshiwa ambayo Mwenyezi Mungu alimletea Wahyi Nabii wake na Mtume Wake Muhammad, rehema na amani zimshukie; na tumeziamini Kurasa alizoteremshiwa Ibrāhīm na watoto wake wawili: Ismāīl na Is’ḥāq, na alizoteremshiwa Ya’qūb na Asbāṭ - Manabii wanaotokana na watoto wa Ya’qūb waliokuwa katika makabila kumi na mbili ya Wana wa Isrāīl-; na tumeiamini Taurati aliyopewa Mūsā na Injil aliyopewa Īsā na Wahyi ulioteremshwa kwa Mitume wote. Hatumbagui yoyote miongoni mwao katika kuamini. Na sisi ni wenye kumdhalilikia Mwenyezi Mungu kwa kumtii na kumuabudu.” info
التفاسير:

external-link copy
137 : 2

فَإِنۡ ءَامَنُواْ بِمِثۡلِ مَآ ءَامَنتُم بِهِۦ فَقَدِ ٱهۡتَدَواْۖ وَّإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا هُمۡ فِي شِقَاقٖۖ فَسَيَكۡفِيكَهُمُ ٱللَّهُۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Wakiyaamini Makafiri, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara na wengineo, kama yale milyoyaamini nyinyi katika yale aliyokuja nayo Mtume, basi wameongoka kwenye haki; na wakikataa, basi wao wako kwenye upinzani mkubwa. Mwenyezi Mungu Atakutosheleza, ewe Mtume, shari lao na Atakupa ushindi juu yao. Yeye Ndiye Msikizi wa maneno yenu, Ndiye Mjuzi wa hali zenu. info
التفاسير:

external-link copy
138 : 2

صِبۡغَةَ ٱللَّهِ وَمَنۡ أَحۡسَنُ مِنَ ٱللَّهِ صِبۡغَةٗۖ وَنَحۡنُ لَهُۥ عَٰبِدُونَ

Jilazimisheni na Dini ya Mwenyezi Mungu ambayo Ameifanya inasibiane na maumbile yenu. Kwani hakuna maumbile mazuri kuliko yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewaumbia watu. Jilazimisheni nayo na mseme, “Sisi ni wenye kuiandama, ni watiifu kwa Mola wetu katika kufuata kwetu mila ya Ibrāhīm.” info
التفاسير:

external-link copy
139 : 2

قُلۡ أَتُحَآجُّونَنَا فِي ٱللَّهِ وَهُوَ رَبُّنَا وَرَبُّكُمۡ وَلَنَآ أَعۡمَٰلُنَا وَلَكُمۡ أَعۡمَٰلُكُمۡ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُخۡلِصُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia Watu wa Kitabu, “Je mnajadiliana na sisi juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasa, hali ya kuwa Yeye ni Mola wa viumbe wote, hahusiki na watu fulani tu bila ya wengine? Sisi tuna amali zetu, na nyinyi muna zenu. Na sisi tunamtakasia Mwenyezi Mungu ibada na utiifu; hatumshirikishi kitu chochote na hatumuabudu yoyote isipokuwa Yeye.” info
التفاسير:

external-link copy
140 : 2

أَمۡ تَقُولُونَ إِنَّ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطَ كَانُواْ هُودًا أَوۡ نَصَٰرَىٰۗ قُلۡ ءَأَنتُمۡ أَعۡلَمُ أَمِ ٱللَّهُۗ وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن كَتَمَ شَهَٰدَةً عِندَهُۥ مِنَ ٱللَّهِۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Au je, Mnasema, kwa njia ya kujadili kuhusu Mwenyezi Mungu kwamba Ibrāhīm na Ismā'īl na Is’ḥāq na Ya’qūb na Asbāṭ - Manabii waliokuwa katika makabila kumi na mbili ya Wana wa Isrāīl wanaotokana na wana wa Ya’qūb - walikuwa katika dini ya Kiyahudi au ya Kinaswara? Huu ni urongo. Kwani hao walitumilizwa na kufa kabla ya Taurati na Injili. Waambie, ewe Mtume, “Kwani ni nyinyi mnaoijua zaidi dini yao au ni Mwenyezi Mungu Aliyetukuka?” Na Mwenyezi Mungu Ameshaeleza katika Qur’ani kwamba wao walikuwa Waislamu wenye msimamo uliolingana sawa. Na hakuna yoyote dhalimu zaidi kuliko nyinyi mnapouficha ushahidi uliothibiti kwenu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kudai kinyume chake kwa kumzulia Mwenyezi Mungu urongo. Na Mwenyezi Mungu si Mwenye kughafilika na chochote katika vitendo vyenu. Yeye ni Mwenye kuvidhibiti na ni Mwenye kuwalipa kwavyo. info
التفاسير:

external-link copy
141 : 2

تِلۡكَ أُمَّةٞ قَدۡ خَلَتۡۖ لَهَا مَا كَسَبَتۡ وَلَكُم مَّا كَسَبۡتُمۡۖ وَلَا تُسۡـَٔلُونَ عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Hao ni ummah waliopita miongoni mwa wale waliowatangulia nyinyi. Wao wana amali zao, na nyinyi muna amali zenu. Wala nyinyi hamtaulizwa kuhusu amali zao. Na wao hawataulizwa kuhusu amali zenu. Katika aya hii pana kukata njia ya kujifungamanisha na viumbe kwa kujiamabatisha nao, kutoghurika kwa kunasibiana na wao, kwa kuwa linalozingatiwa ni kumuamini Mwenyezi Mungu na kumuabudu Peke Yake na kuwafuata Mitume Wake, na kwamba mwenye kumkanusha Mtume yoyote katika wao, huwa amewakanusha Mitume wote. info
التفاسير: