Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
89 : 2

وَلَمَّا جَآءَهُمۡ كِتَٰبٞ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِ مُصَدِّقٞ لِّمَا مَعَهُمۡ وَكَانُواْ مِن قَبۡلُ يَسۡتَفۡتِحُونَ عَلَى ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَلَمَّا جَآءَهُم مَّا عَرَفُواْ كَفَرُواْ بِهِۦۚ فَلَعۡنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na ilipowajia Qur’ani inayotoka kwa Mwenyezi Mungu, ikisadikisha yale ambayo waliokuwa nayo kwenye Taurati, waliikanusha na kuukataa utume wa Muhammad, rehema na mani zimshukie. Na walikuwa, kabla ya kutumilizwa kwake, wakitumai kusaidiwa na yeye dhidhi ya washirikina wa Kiarabu, na walikuwa wakisema, “Umekaribia wakati wa kutumilizwa Mtume wa zama za mwisho ambaye sisi tutamfuata na tutapigana na nyinyi tukiwa pamoja na yeye.” Alipowajia huyo Mtume, ambaye walizijua sifa zake na ukweli wake, walimkataa na walimkanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu imshukie kila aliyemkanusha Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad, rehema na amani zimshukie, na kukanusha Kitabu chake ambacho Mwenyezi Mungu alimletea kwa njia ya Wahyi. info
التفاسير:

external-link copy
90 : 2

بِئۡسَمَا ٱشۡتَرَوۡاْ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمۡ أَن يَكۡفُرُواْ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بَغۡيًا أَن يُنَزِّلَ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ فَبَآءُو بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٖۚ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٞ مُّهِينٞ

Ni baya chaguo la Wana wa Isrāīl walilojichagulia. Kwani walibadilisha imani kwa ukafiri, (kwa kuacha imani na kuchukua ukafiri) kwa dhulma na uhasidi kwa kuwa Mwenyezi Mungu, kwa fadhila ZAke, Alimteremshia Nabii Wake na Mtume Wake Muhammad, rehema na amani zimshukie. Basi wakarudi na hali ya kuwa Mwenyezi Mungu Ana ghadhabu juu yao kwa kumkanusha kwao Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, baada ya kuwa na ghadhabu juu yao kwa kuipotoa Taurati. Na wenye kukanusha unabii wa Muhammad, rehema na amani zimshukie, wana adhabu yenye kuwabadilisha na kuwafanya wanyonge. info
التفاسير:

external-link copy
91 : 2

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ ءَامِنُواْ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُواْ نُؤۡمِنُ بِمَآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا وَيَكۡفُرُونَ بِمَا وَرَآءَهُۥ وَهُوَ ٱلۡحَقُّ مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَهُمۡۗ قُلۡ فَلِمَ تَقۡتُلُونَ أَنۢبِيَآءَ ٱللَّهِ مِن قَبۡلُ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na baadhi ya Waislamu wanaposema kuwaambia Mayahudi, “Aminini Qur’ani,” wanasema, “Sisi tunaviamini vilivyoteremshwa kwa Mitume wetu.” Na wao wanakanusha vilivyoteremshwa na Mwenyezi Mungu baada yake, pamoja na kuwa ndio haki inayosadikisha vile walivyonavyo. Lau wao walikuwa wanaviamini vitabu vyao kikweli, wangaliiamini Qur’ani iliyozisadikisha. Waambie, ewe Mtume, “Iwapo nyinyi mnayamini yale mliyoteremshiwa na Mwenyezi Mungu kwenu, kwa nini mliwaua Manabii wa Mwenyezi Mungu wakati wa nyuma?” info
التفاسير:

external-link copy
92 : 2

۞ وَلَقَدۡ جَآءَكُم مُّوسَىٰ بِٱلۡبَيِّنَٰتِ ثُمَّ ٱتَّخَذۡتُمُ ٱلۡعِجۡلَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَنتُمۡ ظَٰلِمُونَ

Hakika Nabii wa Mwenyezi Mungu, Mūsā, aliwajia nyinyi na miujiza iliyo wazi yenye dalili ya ukweli wake, kama mafuriko, nzige, chawa, vyura na mengineyo katika yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu katika Qur’ani tukufu. Pamoja na hivyo, mumemchukuwa ndama mkamfanya ni muabudiwa, baada ya Mūsā kuondoka kuenda kukutana na Mola wake. Na nyinyi kwa kufanya hivyo mnavuka mipaka ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
93 : 2

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَكُمۡ وَرَفَعۡنَا فَوۡقَكُمُ ٱلطُّورَ خُذُواْ مَآ ءَاتَيۡنَٰكُم بِقُوَّةٖ وَٱسۡمَعُواْۖ قَالُواْ سَمِعۡنَا وَعَصَيۡنَا وَأُشۡرِبُواْ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلۡعِجۡلَ بِكُفۡرِهِمۡۚ قُلۡ بِئۡسَمَا يَأۡمُرُكُم بِهِۦٓ إِيمَٰنُكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na Kumbukeni, wakati tulipochukua kwenu ahadi yenye mkazo ya kuikubali Taurati aliyokuja nayo Mūsā, mkavunja ahadi, tukaliinua jabali la Tūr juu ya vichwa vyenu na tukasema, “Tuchukueni tulichowapa kwa bidii, na msikie na mtii, au tutaliangusha jabali juu yenu.” Mkasema, “Tumesikia kauli yako na tumeasi amri yako,” kwa kuwa ibada ya ndama imetangamana na nyoyo zenu kwa sababu ya kuendelea kwenu sana kwenye ukafiri. Waambie, ewe Mtume, Ni mbaya iliyoje hiyo njia ya ukafiri na upotevu ambayo imani yenu imewapeleka, iwapo nyinyi mnayasadiki yale yaliyoteremshwa kwenu. info
التفاسير: