ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
50 : 17

۞ قُلۡ كُونُواْ حِجَارَةً أَوۡ حَدِيدًا

Sema: Kuweni hata mawe na chuma. info

Ewe Nabii! Waambie: Hata mkiwa mawe yasiyo na uhai, au chuma, ambacho ni kigumu kuliko jiwe,

التفاسير:

external-link copy
51 : 17

أَوۡ خَلۡقٗا مِّمَّا يَكۡبُرُ فِي صُدُورِكُمۡۚ فَسَيَقُولُونَ مَن يُعِيدُنَاۖ قُلِ ٱلَّذِي فَطَرَكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةٖۚ فَسَيُنۡغِضُونَ إِلَيۡكَ رُءُوسَهُمۡ وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَۖ قُلۡ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَرِيبٗا

Au umbo lolote mnalo liona kubwa katika vifua vyenu. Watasema: Nani atakaye turudisha tena? Sema: Yule yule aliye kuumbeni mara ya kwanza! Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu! info

Au umbo jingenelo lolote ambalo mnaona kwa mawazo yenu haliwezi kuwa hai, basi hapana shaka yoyote mtafufuliwa! Watasema kwa kuona ni muhali: Nani atakaye turejesha hivyo? Waambie: Atakurjesheeni Mwenyezi Mungu, yule yule aliye kuumbeni mara ya kwanza. Watakutikisia vichwa vyao kwa mastaajabu, nao wakisema kwa kejeli: Huko kufufuliwa unako tuahidi kutakuwa lini? Waambie: Nataraji kutakuwa karibu!

التفاسير:

external-link copy
52 : 17

يَوۡمَ يَدۡعُوكُمۡ فَتَسۡتَجِيبُونَ بِحَمۡدِهِۦ وَتَظُنُّونَ إِن لَّبِثۡتُمۡ إِلَّا قَلِيلٗا

iku atakapo kuiteni, na nyinyi mkamuitikia kwa kumshukuru, na mkadhani kuwa hamkukaa ila muda mdogo tu. info

Na siku atapo kufufueni Mwenyezi Mungu kutoka makaburini kwenu, mtafufuliwa nanyi mkimshukuru na kumsifu Mola wenu Mlezi kwa ukamilifu wa uwezo wake. Na mtadhani kuwa hamkukaa makaburni kwenu ila muda mchache tu. Mtaona muda ni mfupi kwa mnasaba ya hayo mnayo yaendea.

التفاسير:

external-link copy
53 : 17

وَقُل لِّعِبَادِي يَقُولُواْ ٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُۚ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ يَنزَغُ بَيۡنَهُمۡۚ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ كَانَ لِلۡإِنسَٰنِ عَدُوّٗا مُّبِينٗا

Waambie waja wangu waseme maneno mazuri, maana Shet'ani huchochea ugomvi baina yao. Hakika Shet'ani ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu. info

Ewe Nabii! Waambie waja wangu Waumini wanapo pambana na washirikina waseme maneno yaliyo bora ya kukinaisha, na waachilie mbali kutumia maneno makali makali yanayo sabibisha shari na uharibifu. Kwani Shetani huleta fisadi baina ya Waumini na makafiri, kwa kuwa yeye ni adui aliye wazi wa binaadamu.

التفاسير:

external-link copy
54 : 17

رَّبُّكُمۡ أَعۡلَمُ بِكُمۡۖ إِن يَشَأۡ يَرۡحَمۡكُمۡ أَوۡ إِن يَشَأۡ يُعَذِّبۡكُمۡۚ وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ وَكِيلٗا

Mola wenu Mlezi anakujueni vilivyo. Akipenda atakurehemuni, na akipenda atakuadhibuni. Na hatukukutuma ili uwe mlinzi juu yao. info

Mola wenu Mlezi ndiye anaye jua vyema mwisho wa mambo yenu. Akipenda atakurehemuni kwa kukupeni tawfiki ya Imani, (uwezo wa kuamini) au akipenda atakupeni adhabu kwa kuikosa hiyo Imani. Wala Sisi hatukukupeleka wewe uwe ni mwakilishi wao kwa mambo yao, hata uwalazimishe kuamini. Bali tumekutuma uwe ni mbashiri kuwapa khabari njema wenye kusadiki, na mwonyaji kuwaonya wanao kanusha. Waachilie mbali, na waamrishe sahaba zako wawastahamilie.

التفاسير:

external-link copy
55 : 17

وَرَبُّكَ أَعۡلَمُ بِمَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَلَقَدۡ فَضَّلۡنَا بَعۡضَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ عَلَىٰ بَعۡضٖۖ وَءَاتَيۡنَا دَاوُۥدَ زَبُورٗا

Na Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi. Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine; na Daudi tulimpa Zaburi. info

Na Mola wako Mlezi anajua vilivyo vyote viliomo mbinguni na ardhini, na anajua hali zao. Basi anawakhiari miongoni mwao kwa kuwapa Unabii awatakao. Naye amekukhiari wewe kwa kukupa Utume wake. Basi haiwafalii wao kuudhika na Unabii wako. Na hao Manabii si wote sawa sawa kwa daraja mbele yake Aliye tukuka shani yake. Bali baadhi yao ni bora kuliko wenginewe. Naye amewatukuza baadhi ya Manabii juu ya wengine kwa miujiza, na wingi wa wafwasi, si kwa ufalme. Basi alitukuzwa Daudi kwa kuwa kapewa Zaburi, si kwa kuwa kapewa ufalme. Basi hapana ajabu kuwa wewe, Muhammad, ukapata fadhila kubwa kabisa kwa kuwa umepewa Qur'ani.

التفاسير:

external-link copy
56 : 17

قُلِ ٱدۡعُواْ ٱلَّذِينَ زَعَمۡتُم مِّن دُونِهِۦ فَلَا يَمۡلِكُونَ كَشۡفَ ٱلضُّرِّ عَنكُمۡ وَلَا تَحۡوِيلًا

Sema: Waombeni hao mnao wadaia badala yake Yeye. Hawawezi kukuondoleeni madhara, wala kuyaweka pengine. info

Waambie hawa wanao abudu viumbe na wanadai kuwa hao ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu: Waombeni hao mnao waabudu inapo kuteremkieni shida, au mkakhofu kuwa itakushukieni. Hamtopata kwao chochote cha kukuondoleeni madhara yenu, wala kuyahamisha akapewa mwinginewe.

التفاسير:

external-link copy
57 : 17

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ يَبۡتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ ٱلۡوَسِيلَةَ أَيُّهُمۡ أَقۡرَبُ وَيَرۡجُونَ رَحۡمَتَهُۥ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُۥٓۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحۡذُورٗا

Hao wanao waomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi - hata miongoni mwao walio karibu mno - na wanataraji rehema zake na wanaikhofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhari nayo. info

Na hakika hawa viumbe wanao waomba wale wanao waabudu, wao wenyewe wanamuabudu Mwenyezi Mungu, na wanaomba wapate daraja na cheo kwake kwa ut'iifu, na wana pupa ya kutaka wawe karibu zaidi na Mwenyezi Mungu, na wanatumaini kupata kwake rehema, na wanaikhofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mwenyezi Mungu inatakikana kutahadhari nayo na kuiogopa!

التفاسير:

external-link copy
58 : 17

وَإِن مِّن قَرۡيَةٍ إِلَّا نَحۡنُ مُهۡلِكُوهَا قَبۡلَ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَوۡ مُعَذِّبُوهَا عَذَابٗا شَدِيدٗاۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي ٱلۡكِتَٰبِ مَسۡطُورٗا

Na hapana mji wowote ila Sisi tutauteketeza kabla ya Siku ya Kiyama, au tutaupa adhabu kali. Haya yamekwisha andikwa katika Kitabu. info

Na ni mazoea yetu kuuteketeza kila mji na watu wake unapo dhulumu mji huo. Au huwapa adhabu kali watu wake kwa mauwaji au vyenginevyo. Basi watu wako watahadhari, kwani hukumu yetu imekwisha hukumiwa, na imekwisha andikwa katika Kitabu chetu.

التفاسير: