ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
105 : 17

وَبِٱلۡحَقِّ أَنزَلۡنَٰهُ وَبِٱلۡحَقِّ نَزَلَۗ وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا مُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا

Na kwa Haki tumeiteremsha, na kwa Haki imeteremka. Na hatukukutuma ila uwe mbashiri na mwonyaji. info

Na hatukuiteremsha Qur'ani ila kwa kuunga mkono hikima ya Mwenyezi Muungu, iliyo pelekea kuteremshwa kwake. Nayo hiyo Qur'ani kwa dhati yake haikuteremka ila kuwa imekusanya Ukweli wote. Kwani itikadi zake ndizo zilizo sawa, na hukumu zake ndizo zilizo nyooka. Na wewe, ewe Nabii, hatukukutuma ila uwe mbashiri wa kuwabashiria Pepo wenye kuamini, na mwonyaji kuwaonya wanao ukanya Moto. Basi wewe huna jukumu lolote ikiwa wao hawaamini.

التفاسير:

external-link copy
106 : 17

وَقُرۡءَانٗا فَرَقۡنَٰهُ لِتَقۡرَأَهُۥ عَلَى ٱلنَّاسِ عَلَىٰ مُكۡثٖ وَنَزَّلۡنَٰهُ تَنزِيلٗا

Na Qur'ani tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa kituo, na tumeiteremsha kidogo kidogo. info

Na hii Qur'ani tumeigawa na tumeiteremsha kipande kipande kwa muda mrefu, ili uwasomee watu kwa taratibu wapate kuifahamu. Tumeiteremsha kidogo kidogo kwa utulivu bila ya matatanisho.

التفاسير:

external-link copy
107 : 17

قُلۡ ءَامِنُواْ بِهِۦٓ أَوۡ لَا تُؤۡمِنُوٓاْۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ مِن قَبۡلِهِۦٓ إِذَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ يَخِرُّونَۤ لِلۡأَذۡقَانِۤ سُجَّدٗاۤ

Sema: Iaminini au msiiamini. Hakika wale walio pewa ilimu kabla yake, wanapo somewa hii, huanguka kifudifudi wanasujudu. info

Waambie makafiri wa Makka kwa kuwatisha: Jichagulieni nafsi zenu mlitakalo - kuiamini Qur'ani au la! Kwani hakika walio pewa ilimu sawa na fahamu baraabara kabla ya kuteremka kwake, wakisomewa Qur'ani huangukia kwenye nyuso zao kwa kusujudu na kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu.

التفاسير:

external-link copy
108 : 17

وَيَقُولُونَ سُبۡحَٰنَ رَبِّنَآ إِن كَانَ وَعۡدُ رَبِّنَا لَمَفۡعُولٗا

Na wanasema: Subhana Rabbina, Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika ahadi ya Mola wetu Mlezi lazima itimizwe!. info

Na wao husema: Mola wetu Mlezi ametakasika na ila ya kwenda kinyume na ahadi yake ya kuneemesha na kuadhibu alio ahidi. Kwani ahadi yake lazima itimie bila ya shaka yoyote.

التفاسير:

external-link copy
109 : 17

وَيَخِرُّونَ لِلۡأَذۡقَانِ يَبۡكُونَ وَيَزِيدُهُمۡ خُشُوعٗا۩

Na huanguka kifudifudi na huku wanalia, na inawazidisha unyenyekevu. info

Na huangukia tena kwenye nyuso zao mara ya pili wakilia kwa kumkhofu Mwenyezi Mungu, na Qur'ani inawazidisha unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
110 : 17

قُلِ ٱدۡعُواْ ٱللَّهَ أَوِ ٱدۡعُواْ ٱلرَّحۡمَٰنَۖ أَيّٗا مَّا تَدۡعُواْ فَلَهُ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَلَا تَجۡهَرۡ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتۡ بِهَا وَٱبۡتَغِ بَيۡنَ ذَٰلِكَ سَبِيلٗا

Sema: Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri. Wala usitangaze Swala yako kwa sauti kubwa, wala usiifiche kwa sauti ndogo, bali shika njia ya kati na kati ya hizo. info

Waambie hawa washirikina: Mwiteni Mwenyezi Mungu kwa jina la Allah, au jina la Rahman; kwani jina lolote mtalo mwitia ni zuri. Yeye Mtukufu ana majina mengi mazuri mazuri. Wala hamdanganyikiwi kwa kutumia majina mengi kuwa kwa hivyo mwenye kuitwa ni zaidi ya Mmoja. Na unapo soma Qur'ani katika Swala zako, basi usipaze sauti yako wakasikia washirikina wakakusibabi na wakakuudhi. Wala usifanye kwa siri hata Waumini wakawa hawasikii. Kuwa kati kati katika kusoma kwako.

التفاسير:

external-link copy
111 : 17

وَقُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي لَمۡ يَتَّخِذۡ وَلَدٗا وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ شَرِيكٞ فِي ٱلۡمُلۡكِ وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ وَلِيّٞ مِّنَ ٱلذُّلِّۖ وَكَبِّرۡهُ تَكۡبِيرَۢا

Na sema: Alhamdulillah, Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye hana mwana, wala hana mshirika katika ufalme, wala hana rafiki wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa. info

Nasema Alhamdulillah, Himdi zote, yaani sifa na shukrani, ni za Mwenyezi Mungu ambaye hakuzaa mwana, kwani hamhitajii; wala hana mshirika katika ufalme, kwani Yeye peke yake ndiye aliye uanzisha; wala hana msaidizi wa kumtia nguvu kwa udhaifu fulani unao mpata. Na mtukuze Mola wako Mlezi kwa utukufu mkubwa ulio laiki naye.

التفاسير: