ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
8 : 17

عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يَرۡحَمَكُمۡۚ وَإِنۡ عُدتُّمۡ عُدۡنَاۚ وَجَعَلۡنَا جَهَنَّمَ لِلۡكَٰفِرِينَ حَصِيرًا

Huenda Mola wenu Mlezi akakurehemuni. Na mkirudia na Sisi tutarudia. Na tumeifanya Jahannamu kuwa ni gereza kwa ajili ya makafiri. info

Asaa Mola wenu Mlezi akakurehemuni baada ya hiyo mara ya pili pindi mkitubu. Na mkirejea kwenye ufisadi Nasi tutarejea kukuadhibuni. Na tumeifanya Jahannam kuwa ndiyo gereza la kuwafungia makafiri!

التفاسير:

external-link copy
9 : 17

إِنَّ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ يَهۡدِي لِلَّتِي هِيَ أَقۡوَمُ وَيُبَشِّرُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٱلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ أَنَّ لَهُمۡ أَجۡرٗا كَبِيرٗا

Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa. info

Hakika hii Qur'ani inawaongoza watu kwenye njia ambayo ndiyo njia iliyo kaa sawa kabisa kuliko njia zote, na ndiyo njia ya salama kabisa ya kufikilia kwenye furaha ya kweli katika dunia. Na wabashirie wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wenye kuit'ii Haki na wanatenda vitendo vyema, kuwa watapata ujira mkubwa Siku ya Kiyama.

التفاسير:

external-link copy
10 : 17

وَأَنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ أَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا

Na yakwamba wale wasio iamini Akhera tumewaandalia adhabu chungu. info

Na hakika wale ambao hawaiamini Akhera tumewatengenezea adhabu ya machungu makali.

التفاسير:

external-link copy
11 : 17

وَيَدۡعُ ٱلۡإِنسَٰنُ بِٱلشَّرِّ دُعَآءَهُۥ بِٱلۡخَيۡرِۖ وَكَانَ ٱلۡإِنسَٰنُ عَجُولٗا

Na mwanaadamu huomba shari kama vile aombavyo kheri, kwani mwanaadamu ni mwenye pupa. info

Ni katika tabia ya mwanaadamu kufanya haraka katika kuwahukumia watu kwa yanayo wapata, na katika kauli zake na vitendo vyake. Naye hukimbilia kulingania shari kama anavyo lingania kheri. Naye hufanya haraka kumuapiza kwa Mwenyezi Mungu amteremshia shari yule aliye mkasirisha, kama anavyo fanya haraka kuomba kheri.

التفاسير:

external-link copy
12 : 17

وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ ءَايَتَيۡنِۖ فَمَحَوۡنَآ ءَايَةَ ٱلَّيۡلِ وَجَعَلۡنَآ ءَايَةَ ٱلنَّهَارِ مُبۡصِرَةٗ لِّتَبۡتَغُواْ فَضۡلٗا مِّن رَّبِّكُمۡ وَلِتَعۡلَمُواْ عَدَدَ ٱلسِّنِينَ وَٱلۡحِسَابَۚ وَكُلَّ شَيۡءٖ فَصَّلۡنَٰهُ تَفۡصِيلٗا

Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili. Tena tukaifuta ishara ya usiku, na tukaifanya ishara ya mchana ni yenye mwangaza ili mtafute fadhila itokayo kwa Mola wenu Mlezi, na mpate kujua idadi ya miaka na hisabu. Na kila kitu tumekifafanua waziwazi. info

Na Sisi tumejaalia usiku na mchana, kwa namna yao na kupishana kwao, kuwa ni alama zenye kuonyesha Upweke wetu na Uwezo wetu. Tukauondoa mwangaza kwenye usiku, na kisionekane kitu. Na alama yake ni giza liso kuwa na jua. Hiyo ni ishara kubwa. Na mchana tukaufanya wa kuangaza. Hapo laonekana jua, ile ishara kuu, ili mpate kwenda mtakako wakati huo katika kutafuta maisha yenu. Na katika kuja usiku na mchana mpate kujua idadi ya miaka na hisabu za miezi na siku. Na Sisi tumekubainishieni kila kitu kwa uwazi kwa sababu ya maslaha yenu, ili isimame hoja juu yenu baada kutimia neema.

التفاسير:

external-link copy
13 : 17

وَكُلَّ إِنسَٰنٍ أَلۡزَمۡنَٰهُ طَٰٓئِرَهُۥ فِي عُنُقِهِۦۖ وَنُخۡرِجُ لَهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ كِتَٰبٗا يَلۡقَىٰهُ مَنشُورًا

Na kila mtu tumemfungia a'mali yake shingoni mwake. Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu atakacho kikuta kiwazi kimekunjuliwa. info

Na kila mtu tumemfungamanisha na a'mali yake, vitendo vyake, kama koja lilioko shingoni. Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu kilicho andikwa vitendo vyake vyote. Atakiona kitabu hicho kiwazi iwe wepesi kwake kukisoma.

التفاسير:

external-link copy
14 : 17

ٱقۡرَأۡ كِتَٰبَكَ كَفَىٰ بِنَفۡسِكَ ٱلۡيَوۡمَ عَلَيۡكَ حَسِيبٗا

Ataambiwa: Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosha leo kukuhisabu. info

Ataambiwa: Soma kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa duniani alikuwa hajui kusoma. Soma kitabu cha a'mali zako. Hicho leo kinatosha kukuhisabia na kukudhibitia vitendo vyako.

التفاسير:

external-link copy
15 : 17

مَّنِ ٱهۡتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهۡتَدِي لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيۡهَاۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰۗ وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبۡعَثَ رَسُولٗا

Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume. info

Mwenye kufuata njia ya Haki basi anajifaa mwenyewe, na mwenye kuiacha basi anajipoteza mwenyewe. Wala hapana mwenye kubeba dhambi zake akambebea dhambi za mwenginewe. Wala haitufalii kumuadhibu yeyote kwa kutenda kitu kabla hatujampelekea Mtume kutoka kwetu amwonyeshe njia ya Haki na kumkataza maovu.

التفاسير:

external-link copy
16 : 17

وَإِذَآ أَرَدۡنَآ أَن نُّهۡلِكَ قَرۡيَةً أَمَرۡنَا مُتۡرَفِيهَا فَفَسَقُواْ فِيهَا فَحَقَّ عَلَيۡهَا ٱلۡقَوۡلُ فَدَمَّرۡنَٰهَا تَدۡمِيرٗا

Na pindi tukitaka kuuteketeza mji huwaamrisha wale wenye starehe na taanusi, lakini wao huendelea kutenda maovu humo. Basi hapo kauli huthibiti juu ya mji huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa. info

Na pindi tukikadiria tangu azali katika Lauhun-mahfuudh kuwateketeza watu wa mji fulani kwa mujibu wa hikima yetu, basi Sisi huwasalitisha wale walio jidekeza kwa taanusi katika huo mji, wakafanya fisadi zao, wakaacha njia ya Haki, na wakawafuata wenginewe bila ya kutambua, na kwa hivyo huo mji wote tena hapo hustahiki kuangamizwa. Nasi huuangamiza vikubwa mno!

التفاسير:

external-link copy
17 : 17

وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا مِنَ ٱلۡقُرُونِ مِنۢ بَعۡدِ نُوحٖۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ بِذُنُوبِ عِبَادِهِۦ خَبِيرَۢا بَصِيرٗا

Na kaumu ngapi tumeziangamiza baada ya Nuhu! Na Mola wako Mlezi anatosha kabisa kuwa ni Mwenye kuzijua na kuziona dhambi za waja wake. info

Na kaumu nyingi zilizo kuja baada ya Nuhu tuliziangamiza kwa kuwaasi Manabii wao. Na yakutosha kuwa ni ishara ya Mola wako Mlezi kwamba Yeye ni Mjuzi wa kila kitu kama kilivyo, kwa ujuzi wa Mwenye kuona. Naye anazo khabari za dhambi za waja wake, na Mwenye kuziona. Hapana chochote katika vitendo vya waja wake asicho kijua, na Yeye atawalipa kama wanavyo stahiki.

التفاسير: