Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany

Numero di pagina:close

external-link copy
121 : 7

قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa viumbe vyote. info

Huku wakisema hao wachawi walio tubia: Tumemuamini Muumba wa viumbe vyote, Mwenye kumiliki na kuendesha mambo yao yote.

التفاسير:

external-link copy
122 : 7

رَبِّ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ

Mola Mlezi wa Musa na Haarun. info

Hakika huyo ndiye Mungu anaye itakidiwa na kuaminiwa na Musa na Haarun.

التفاسير:

external-link copy
123 : 7

قَالَ فِرۡعَوۡنُ ءَامَنتُم بِهِۦ قَبۡلَ أَنۡ ءَاذَنَ لَكُمۡۖ إِنَّ هَٰذَا لَمَكۡرٞ مَّكَرۡتُمُوهُ فِي ٱلۡمَدِينَةِ لِتُخۡرِجُواْ مِنۡهَآ أَهۡلَهَاۖ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Akasema Firauni: Mmemuamini kabla sijakupeni idhini? Hizi ni njama mlizo panga mjini mpate kuwatoa wenyewe. Lakini karibu mtajua! info

Jambo hili lilimtisha Firauni na ikafoka ghadhabu yake, akasema: Hivyo nyinyi mmemuamini na kumsadiki Mola Mlezi wa Musa na Haarun kabla sijakupeni ruhusa mimi? Hakika hapa pana kijambo mmekizua nyinyi na Musa na Haarun kwa kuwafikiana. Na haya si chochote ila ni vitimbi mlivyo vipanga katika mji wa Misri mpate kuwatoa wenyewe kwa hila yenu. Basi ngojeni, mtaiona adhabu itayo kushukieni kuwa ndio jaza yenu kwa kumfuata Musa na Haarun, na ndio adabu yenu kwa hivi vitimbi vyenu na khadaa!

التفاسير:

external-link copy
124 : 7

لَأُقَطِّعَنَّ أَيۡدِيَكُمۡ وَأَرۡجُلَكُم مِّنۡ خِلَٰفٖ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمۡ أَجۡمَعِينَ

Lazima nitaikata mikono yenu na miguu yenu mbali mbali. Kisha nitakutundikeni misalabani. info

Na ninakuapieni kuwa nitakuteseni vikali, na nitakukateni mikono yenu na miguu yenu mbali mbali, nitakata mkono wa upande mmoja na mguu wa upande wa pili, kisha nitakutundikeni misalabani, kila mmoja wenu, nanyi mmo katika hali hiyo, ili muwe ni zingatio kwa anaye jifikiria kutufanyia vitimbi, au kutaka kuufanyia uasi utawala wetu!

التفاسير:

external-link copy
125 : 7

قَالُوٓاْ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ

Wakasema: Sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. info

Nao hawakuibali kauli yake wala vitisho vyake, kwa kuwa Imani ilikwisha saki ndani ya nyoyo zao. Wakamwambia: Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. Kwa hivyo tunaneemeka katika rehema yake na bora ya malipo yake.

التفاسير:

external-link copy
126 : 7

وَمَا تَنقِمُ مِنَّآ إِلَّآ أَنۡ ءَامَنَّا بِـَٔايَٰتِ رَبِّنَا لَمَّا جَآءَتۡنَاۚ رَبَّنَآ أَفۡرِغۡ عَلَيۡنَا صَبۡرٗا وَتَوَفَّنَا مُسۡلِمِينَ

Nawe hukuudhika nasi ila kwa kuwa tumeziamini Ishara za Mola Mlezi wetu zilipo tujia. Ewe Mola Mlezi wetu! Tumiminie uvumilivu na utufishe hali ni Waislamu. info

Na wewe hutuchukii na kutuadhibu ila kwa kuwa tumemsadiki Musa, na tumezikubali zilipo tujia Ishara za Mola wetu Mlezi zilio wazi, zenye kuonyesha Haki! Kisha wakamuelekea Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu, wakisema: Ewe Mola Mlezi wetu! Tumiminie subira kubwa, itupe nguvu kuhimili shida zote; na utufishe katika Uislamu bila ya kuteseka kwa anayo tuahidi Firauni.

التفاسير:

external-link copy
127 : 7

وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوۡمَهُۥ لِيُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَيَذَرَكَ وَءَالِهَتَكَۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبۡنَآءَهُمۡ وَنَسۡتَحۡيِۦ نِسَآءَهُمۡ وَإِنَّا فَوۡقَهُمۡ قَٰهِرُونَ

Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Unamuacha Musa na watu wake walete uharibifu katika nchi na wakuache wewe na miungu yako? Akasema: Tutawauwa wavulana wao, na tutawaacha hai wanawake wao. Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu juu yao. info

Baada ya Firauni na watu wake kuona waliyo yaona, katika vile kudhihiri mambo ya Musa na nguvu za ushindi wake, na wachawi wakamuamini, walisema wakuu wa kaumu yake: Unamuacha Musa na watu wake wawe huru katika amani, ili mwisho wao wawafisidi kaumu yako dhidi yako katika nchi ya Misri kwa kuwatia katika dini yao, na wakuache wewe na miungu yako bila ya wao kujali? Hapo watu wa Misri watakuona wewe na hiyo miungu kuwa mmeshindwa. Firauni akasema kuwajibu: Tutawawauwa watoto wao wa kiume wa watu hawa, kila anaye zaliwa; na tutawabakisha wa kike wawe hai, ili wasiwe na nguvu, kama tulivyo fanya zamani. Na sisi tuko juu yao kwa kuwashinda na kwa utawala, na kuwafanyia kahari.

التفاسير:

external-link copy
128 : 7

قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱللَّهِ وَٱصۡبِرُوٓاْۖ إِنَّ ٱلۡأَرۡضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلۡمُتَّقِينَ

Musa akawaambia watu wake: Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu, na subirini. Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu. Naye humrithisha amtakaye katika waja wake. Na mwisho ni wa wachamngu. info

Na hapo Musa aliona kama dalili za huzuni katika watu wake, basi akawatia nguvu katika azma yao. Akawambia: Mtakeni Mwenyezi Mungu msaada na kukuungeni mkono. Na kuweni imara, wala msifazaike. Kwani ardhi yote imo katika nguvu za uwezo wa Mwenyezi Mungu na ufalme wake. Humrithisha amtakaye katika waja wake, wala si ya Firauni. Na mwisho mwema wataupata wale wanao mcha Mwenyezi Mungu kwa kushikamana naye na kuzikamata hukumu zake.

التفاسير:

external-link copy
129 : 7

قَالُوٓاْ أُوذِينَا مِن قَبۡلِ أَن تَأۡتِيَنَا وَمِنۢ بَعۡدِ مَا جِئۡتَنَاۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يُهۡلِكَ عَدُوَّكُمۡ وَيَسۡتَخۡلِفَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرَ كَيۡفَ تَعۡمَلُونَ

Wakasema: Tumeudhiwa kabla hujatufikia, na baada ya wewe kutujia! Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamhiliki adui wenu, na akakufanyeni nyinyi ndio wa kufuatia kushika nchi, ili atazame mtavyo kuja tenda nyinyi. info

Wakasema wale watu kwa huzuni na unyonge: Sisi tulipata maudhi zamani kutoka kwa Firauni kabla hujatujia, na hivi sasa tena baada ya kuja kwako. Musa akawafungulia mlango wa matarajio mema kwa kuwaambia: Hakika linalo tarajiwa kwa fadhila za Mola wenu Mlezi ni kumteketeza adui yenu, aliye kufanyeni watumwa na akakuteseni kwa dhulma yake, na akujaalieni nyinyi ndio wa kuimiliki ardhi aliyo kuahidini. Yeye Subhanahu, Aliye takasika, anayajua mnayo yatenda baada ya kukuwekeni huku. Je, mtaishukuru neema au mtaikufuru? Na mtatenda mema katika nchi au mtafanya fisadi? Hayo ili apate kukulipeni duniani na Akhera kwa mujibu wa mtendayo.

التفاسير:

external-link copy
130 : 7

وَلَقَدۡ أَخَذۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ بِٱلسِّنِينَ وَنَقۡصٖ مِّنَ ٱلثَّمَرَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَذَّكَّرُونَ

Na hakika tuliwaadhibu watu wa Firauni kwa miyaka (ya ukame) na kwa upungufu wa mazao, ili wapate kukumbuka. info

Na hakika Sisi tuliwaadhibu Firauni na watu wake kwa ukame, na dhiki ya maisha, na upungufu wa matunda na mazao na miti, kwa kutaraji kuwa watazindukana wautambue unyonge wao, na kushindwa ufalme wao wa jeuri mbele ya nguvu za Mwenyezi Mungu, wapate kuwaidhika na waache kuwadhulumu Wana wa Israili, na wauitikie wito wa Musa a.s. Kwani mtindo wa shida ni kuzuia kujidanganya, na kutengeza tabia, na kuzielekeza nafsi ziikubali Haki, na kumridhi Mola Mlezi wa viumbe vyote, na kumnyenyekea Yeye tu, si mwenginewe.

التفاسير: