Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany

external-link copy
127 : 7

وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوۡمَهُۥ لِيُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَيَذَرَكَ وَءَالِهَتَكَۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبۡنَآءَهُمۡ وَنَسۡتَحۡيِۦ نِسَآءَهُمۡ وَإِنَّا فَوۡقَهُمۡ قَٰهِرُونَ

Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Unamuacha Musa na watu wake walete uharibifu katika nchi na wakuache wewe na miungu yako? Akasema: Tutawauwa wavulana wao, na tutawaacha hai wanawake wao. Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu juu yao. info

Baada ya Firauni na watu wake kuona waliyo yaona, katika vile kudhihiri mambo ya Musa na nguvu za ushindi wake, na wachawi wakamuamini, walisema wakuu wa kaumu yake: Unamuacha Musa na watu wake wawe huru katika amani, ili mwisho wao wawafisidi kaumu yako dhidi yako katika nchi ya Misri kwa kuwatia katika dini yao, na wakuache wewe na miungu yako bila ya wao kujali? Hapo watu wa Misri watakuona wewe na hiyo miungu kuwa mmeshindwa. Firauni akasema kuwajibu: Tutawawauwa watoto wao wa kiume wa watu hawa, kila anaye zaliwa; na tutawabakisha wa kike wawe hai, ili wasiwe na nguvu, kama tulivyo fanya zamani. Na sisi tuko juu yao kwa kuwashinda na kwa utawala, na kuwafanyia kahari.

التفاسير: