Jambo hili lilimtisha Firauni na ikafoka ghadhabu yake, akasema: Hivyo nyinyi mmemuamini na kumsadiki Mola Mlezi wa Musa na Haarun kabla sijakupeni ruhusa mimi? Hakika hapa pana kijambo mmekizua nyinyi na Musa na Haarun kwa kuwafikiana. Na haya si chochote ila ni vitimbi mlivyo vipanga katika mji wa Misri mpate kuwatoa wenyewe kwa hila yenu. Basi ngojeni, mtaiona adhabu itayo kushukieni kuwa ndio jaza yenu kwa kumfuata Musa na Haarun, na ndio adabu yenu kwa hivi vitimbi vyenu na khadaa!