Na wewe hutuchukii na kutuadhibu ila kwa kuwa tumemsadiki Musa, na tumezikubali zilipo tujia Ishara za Mola wetu Mlezi zilio wazi, zenye kuonyesha Haki! Kisha wakamuelekea Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu, wakisema: Ewe Mola Mlezi wetu! Tumiminie subira kubwa, itupe nguvu kuhimili shida zote; na utufishe katika Uislamu bila ya kuteseka kwa anayo tuahidi Firauni.