Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik: Alija Muhsin el-Bervani.

Broj stranice:close

external-link copy
68 : 7

أُبَلِّغُكُمۡ رِسَٰلَٰتِ رَبِّي وَأَنَا۠ لَكُمۡ نَاصِحٌ أَمِينٌ

Nakufikishieni ujumbe wa Mola wangu Mlezi. Na mimi kwenu ni mwenye kukunasihini, muaminifu. info

Katika haya ninayo kwambieni mimi nafikisha amri na makatazo ya Mola Mlezi wangu, na hayo ndio Ujumbe wake kwenu. Na mimi nakupeni nasaha ya dhati, kwa niya safi kabisa. Na mimi ni muaminifu katika ninayo kwambieni, wala mimi si miongoni ya watu waongo.

التفاسير:

external-link copy
69 : 7

أَوَعَجِبۡتُمۡ أَن جَآءَكُمۡ ذِكۡرٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَلَىٰ رَجُلٖ مِّنكُمۡ لِيُنذِرَكُمۡۚ وَٱذۡكُرُوٓاْ إِذۡ جَعَلَكُمۡ خُلَفَآءَ مِنۢ بَعۡدِ قَوۡمِ نُوحٖ وَزَادَكُمۡ فِي ٱلۡخَلۡقِ بَصۜۡطَةٗۖ فَٱذۡكُرُوٓاْ ءَالَآءَ ٱللَّهِ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Mnaona ajabu kukufikieni mawaidha yanayo toka kwa Mola wenu Mlezi kwa mtu aliye mmoja wenu nyinyi ili akuonyeni? Na kumbukeni alivyo kufanyeni mshike pahala pa kaumu ya Nuhu, na akakuzidisheni katika umbo. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa. info

Tena Hud akawaambia: Hivyo mmestaajabu mno, na mkaona mageni kukujieni ukumbusho wa Haki kwa ulimi wa mtu aliye mmoja wenu, kukuonyeni? Mkiendelea na haya mliyo nayo matokeo yake yatakuwa ni mabaya mno. Na hakika jambo hilo si la kustaajabiwa. Kisha Huud akawatajia yaliyo wasibu walio kanusha katika watu walio watangulia, na akawakumbusha neema za Mwenyezi Mungu juu yao. Akasema: Kumbukeni Mwenyezi Mungu alivyo kufanyeni ndio warithi wa nchi baada ya kaumu ya Nuhu alio waangamiza kwa kumkadhibisha Nuhu, na Mwenyezi Mungu akakuzidishieni nyinyi nguvu za mwili na nguvu za utawala. Na neema hizo zinatakikana zilete Imani. Basi zikumbukeni neema zake ili mpate kufuzu.

التفاسير:

external-link copy
70 : 7

قَالُوٓاْ أَجِئۡتَنَا لِنَعۡبُدَ ٱللَّهَ وَحۡدَهُۥ وَنَذَرَ مَا كَانَ يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَا فَأۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Wakasema: Je! Umetujia ili tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na tuyaache waliyo kuwa wakiyaabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayo tuahidi, ukiwa miongoni mwa wasemao kweli. info

Lakini wao juu ya wito mzuri huu walisema kwa kuona mageni: Hivyo wewe umetujia kututaka tumuabudu Mwenyezi Mungu mmoja peke yake, na tuache masanamu waliyo kuwa wakiyaabudu baba zetu? Na hapana shaka sisi hatutofanya hayo, nawe tuletee hiyo adhabu unayo tutishia, kama wewe kweli ni katika wasema kweli!

التفاسير:

external-link copy
71 : 7

قَالَ قَدۡ وَقَعَ عَلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡ رِجۡسٞ وَغَضَبٌۖ أَتُجَٰدِلُونَنِي فِيٓ أَسۡمَآءٖ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّا نَزَّلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٖۚ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ

Akasema: Bila ya shaka adhabu na ghadhabu zimekwisha kukuangukieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Mnabishana nami kwa ajili ya majina tu mliyo yaita nyinyi na baba zenu ambayo kwayo Mwenyezi Mungu hakuteremsha uthibitisho? Basi ngojeni, mimi pia ni pamoja nanyi katika wanao ngoja. info

Hakika kwa hii inadi yenu mmestahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu ikuteremkieni, na ghadhabu yake ikufikieni! Nyinyi mnabisha kwa ajili ya masanamu ambayo mliyo yaita kuwa ni miungu nyinyi na baba zenu, na wala si chochote ila ni majina tu walio pewa, na wala Mwenyezi Mungu hakuleta hoja ya kuonyesha ungu wao. Hayo hayana nguvu za muumbaji inayo kuruhusuni kuyaabudu! Na ikiwa mtashikilia ukaidi huu basi ingojeeni adhabu ya Mwenyezi Mungu, nami pamoja nanyi, sote tungoje nini kitakushukieni.

التفاسير:

external-link copy
72 : 7

فَأَنجَيۡنَٰهُ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَقَطَعۡنَا دَابِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۖ وَمَا كَانُواْ مُؤۡمِنِينَ

Basi tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukakata mizizi ya wale walio zikanusha Ishara zetu, na hawakuwa wenye kuamini. info

Basi Sisi tukamwokoa A'ad na walio amini pamoja naye kwa rehema yetu, na tukawateremshia makafiri cha kuwateketeza, na hapana chao kilicho bakia wala hapana athari yao, na wala hawakuingia katika kundi la Waumini.

التفاسير:

external-link copy
73 : 7

وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمۡ صَٰلِحٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ قَدۡ جَآءَتۡكُم بَيِّنَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡۖ هَٰذِهِۦ نَاقَةُ ٱللَّهِ لَكُمۡ ءَايَةٗۖ فَذَرُوهَا تَأۡكُلۡ فِيٓ أَرۡضِ ٱللَّهِۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٖ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Na kwa Thamud tulimpeleka ndugu yao, Swaleh. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika imekwisha kukufikieni Ishara iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu aliye ni Ishara kwenu. Basi mwachieni ale kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimdhuru, isije kukushukieni adhabu chungu. info

Na tuliwapelekea kina Thamud ndugu yao Swaleh, ambaye ni mwenzi wao kwa nasaba na uwananchi. Na wito wake ulikuwa kama wito wa Mitume walio kuwa kabla yake na baada yake. Akawaambia: Msafishieni ibada Mwenyezi Mungu peke yake, na wala hapana Mungu isipo kuwa Yeye. Na hoja ya Utume wangu imekwisha kukujilieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Nayo ni huyo ngamia mwenye sifa za pekee. Katika huyo ngamia pana hoja. Yeye ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, muacheni ale atakapo katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimdhuru isije kukupateni adhabu chungu. Thamud ni kabila ya Kiarabu iliyo kuwa Al Hijr, baina ya Hijaz na Sham karibu na Wadi Alquraa.

التفاسير: