Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Vertimas į suahilių k. - Abdullah Muchamed ir Nasir Khamis

Puslapio numeris:close

external-link copy
24 : 4

۞ وَٱلۡمُحۡصَنَٰتُ مِنَ ٱلنِّسَآءِ إِلَّا مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡۖ كِتَٰبَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَآءَ ذَٰلِكُمۡ أَن تَبۡتَغُواْ بِأَمۡوَٰلِكُم مُّحۡصِنِينَ غَيۡرَ مُسَٰفِحِينَۚ فَمَا ٱسۡتَمۡتَعۡتُم بِهِۦ مِنۡهُنَّ فَـَٔاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةٗۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِيمَا تَرَٰضَيۡتُم بِهِۦ مِنۢ بَعۡدِ ٱلۡفَرِيضَةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Na ni haramu kwenu kuwaoa wanawake walioolewa, isipokuwa wale mliowateka katika jihadi. Hao ni halali kwenu kuwaoa baada ya kutakasika vizazi vyao kwa kipindi kimoja cha hedhi. Mwenyezi Mungu Amewaandikia uharamu wa kuwaoa hao, na Amewaruhusu kuwaoa wangineo, miongoni mwa wale Aliowahalalishia kuwataka kwa ndoa mkitumia pesa zenu kujihifadhi msitende haramu. Basi wale mliostarehe nao, miongoni mwao, kwa ndoa sahihi, wapeni mahari yao ambayo ni haki yao iliyolazimishwa na Mwenyezi Mungu juu yenu. Na si makosa kwenu, kwa makubaliano yaliyofikiwa baina yenu kwa kuridhiana, kupunguza au kuongeza kiwango cha mahari baada ya kuamuliwa kiwango chake. Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo ya waja Wake, ni Mwenye hekima katika hukumu zake na uendeshaji Wake. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 4

وَمَن لَّمۡ يَسۡتَطِعۡ مِنكُمۡ طَوۡلًا أَن يَنكِحَ ٱلۡمُحۡصَنَٰتِ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ فَمِن مَّا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُم مِّن فَتَيَٰتِكُمُ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۚ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِإِيمَٰنِكُمۚ بَعۡضُكُم مِّنۢ بَعۡضٖۚ فَٱنكِحُوهُنَّ بِإِذۡنِ أَهۡلِهِنَّ وَءَاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِ مُحۡصَنَٰتٍ غَيۡرَ مُسَٰفِحَٰتٖ وَلَا مُتَّخِذَٰتِ أَخۡدَانٖۚ فَإِذَآ أُحۡصِنَّ فَإِنۡ أَتَيۡنَ بِفَٰحِشَةٖ فَعَلَيۡهِنَّ نِصۡفُ مَا عَلَى ٱلۡمُحۡصَنَٰتِ مِنَ ٱلۡعَذَابِۚ ذَٰلِكَ لِمَنۡ خَشِيَ ٱلۡعَنَتَ مِنكُمۡۚ وَأَن تَصۡبِرُواْ خَيۡرٞ لَّكُمۡۗ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na asiyeweza kujimudu mahari ya Waumini waungwana, basi ni hiyari yake aoe wengineo miongoni mwa wanawake wenu waumini waliomilikiwa. Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ndiye Mjuzi wa ukweli wa Imani yenu. Baadhi yenu mnatokana na wengine katika nyinyi. Basi waoeni kwa ruhusa ya watu wao, na wapeni mahari yao mliokubaliana nayo kwa moyo wenu safi, na wawe ni wenye kujiepusha na haramu, si wenye kudhihirisha zina, wala si wenye kuzini kwa siri kwa kufanya urafiki na wanaume. Wakiolewa na wakafanya kitendo kichafu cha kuzini, adhabu yao ni kadiri ya nusu ya adhabu ya walio huru. Huyo aliyeruhusiwa kuoa wajakazi wenye sifa zilizotajwa, ameruhusiwa iwapo anachelea kuingia kwenye uzinifu na ikawa ni uzito kwake kuvumilia kutoundama. Na kuvumilia kutooa wajakazi pamoja na kujihifadhi ni aula na bora zaidi. Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni Mwingi wa msamaha kwenu, ni Mwenye kuwahurumia sana kwa kuwaruhusu muwaoe wao(hao wajakazi) mkishindwa kuwaoa waungwana. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 4

يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمۡ وَيَهۡدِيَكُمۡ سُنَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَيَتُوبَ عَلَيۡكُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Katika kuwaekea Sheria hizi, Mwenyezi Mungu Anataka kuwafunulia wazi alama za dini Yake iliyolingana na hukumu Zake zenye hekima, kuwaonesha njia za Mitume na watu wema waliokuwa kabla yenu katika halali na haramu na kuwakubalia toba zenu kwa kuwarudisha kwenye kumtii Mwenyezi Mungu. Na Yeye, Aliyetakasika na sifa pungufu, ni Mjuzi wa yale yenye kutengeneza mambo ya waja Wake, ni Mwenye hekima katika sheria Zake Alizowaekea. info
التفاسير: