Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Vertimas į suahilių k. - Abdullah Muchamed ir Nasir Khamis

Puslapio numeris:close

external-link copy
15 : 4

وَٱلَّٰتِي يَأۡتِينَ ٱلۡفَٰحِشَةَ مِن نِّسَآئِكُمۡ فَٱسۡتَشۡهِدُواْ عَلَيۡهِنَّ أَرۡبَعَةٗ مِّنكُمۡۖ فَإِن شَهِدُواْ فَأَمۡسِكُوهُنَّ فِي ٱلۡبُيُوتِ حَتَّىٰ يَتَوَفَّىٰهُنَّ ٱلۡمَوۡتُ أَوۡ يَجۡعَلَ ٱللَّهُ لَهُنَّ سَبِيلٗا

Na wale wanaozini katika wanawake wenu, washuhudisheni kwao, enyi viongozi na makadhi, wanaume wanne waadilifu miongoni mwa Waislamu, Na iwapo watatoa ushahidi juu yao kwa hilo, wazuieni, wanawake hao, majumbani mpaka yamalizike maisha yao kwa kufa au Mwenyezi Mungu awape njia ya kuwaokoa na hilo. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 4

وَٱلَّذَانِ يَأۡتِيَٰنِهَا مِنكُمۡ فَـَٔاذُوهُمَاۖ فَإِن تَابَا وَأَصۡلَحَا فَأَعۡرِضُواْ عَنۡهُمَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ تَوَّابٗا رَّحِيمًا

Na wawili wenye kujiingiza kwenye kitendo cha uzinifu basi waudhini kwa kuwapiga, kuwahama na kuwaaibisha. Wakitubia na kitendo walichokifanya na wakajirekebisha kwa kufanya mambo mema, wasameheni na kuacha kuwaudhi. Faida inayotokana na aya hii na ile kabla yake ni kwamba wanaume wakifanya kitendo cha uzinifu wataudhiwa., ama wanawake watafungwa na kuudhiwa. Kifungo, kikomo chake ni kifo. Na udhia, kikomo chake ni toba na kutengea. Hii ilikuwako mwanzo wa Uislamu, kisha ikaondolewa kwa Sheria iliowekwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, nayo ni kupigwa mawe mpaka kufa, kwa yule ambaye ashaoa au ashaolewa, wakiwa wote wawili ni watu huru, waliobaleghe, wenye akili na ambao wameingilia au kuingiliwa katika ndoa sahihi. Ama wasiokuwa hao, adhabu yao ni kupigwa mbati mia na kuhamishwa mwaka mzima. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzikubali toba za waja Wake wanaotubia, ni Mwenye huruma kwao. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 4

إِنَّمَا ٱلتَّوۡبَةُ عَلَى ٱللَّهِ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٖ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Kwa kweli, Mwenyezi Mungu Anaikubali toba itokayo kwa wale wanaofanya maasia na madhambi kwa ujinga wao wa kutojua ubaya wake na kwamba yanasababisha hasira za Mwenyezi Mungu.- Kwa hivyo, kila anayemuasi Mwenyezi Mungu, kwa kukosea au kwa kusudi, yeye ni mjinga kwa kuzingatia maana haya, hata kama anajua kuwa ni haramu.- kisha, hao wanaokubaliwa toba zao, wakarudi kwa Mola wao kwa majuto na kutii kabla ya kukabiliwa na mauti. Basi hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu Anaikubali toba yao. Na Mwenyezi Mungu daima ni Mjuzi kwa viumbe Wake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake mambo na makadirio Yake. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 4

وَلَيۡسَتِ ٱلتَّوۡبَةُ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ حَتَّىٰٓ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ ٱلۡمَوۡتُ قَالَ إِنِّي تُبۡتُ ٱلۡـَٰٔنَ وَلَا ٱلَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمۡ كُفَّارٌۚ أُوْلَٰٓئِكَ أَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا

Kukubaliwa toba si kwa wale wanaoendelea kufanya maasia bila ya kurudi kwa Mola wao mpaka wakafikiwa na shida ya mauti, hapo mmoja wao aseme, «Mimi sasa nimetubia.» Kama ambavyo haikubaliwi toba ya wale wanaokufa na hali wao ni wenye kukanusha, ni wenye kupinga upweke wa Mwenyezi Mungu na ujumbe wa Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Hao wenye kuendeleza maasia hadi kufa kwao, na wakanushaji ambao wanakufa na huku ni makafiri, tumewatayarishia adhabu iumizayo. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 4

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا يَحِلُّ لَكُمۡ أَن تَرِثُواْ ٱلنِّسَآءَ كَرۡهٗاۖ وَلَا تَعۡضُلُوهُنَّ لِتَذۡهَبُواْ بِبَعۡضِ مَآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ إِلَّآ أَن يَأۡتِينَ بِفَٰحِشَةٖ مُّبَيِّنَةٖۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ فَإِن كَرِهۡتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰٓ أَن تَكۡرَهُواْ شَيۡـٔٗا وَيَجۡعَلَ ٱللَّهُ فِيهِ خَيۡرٗا كَثِيرٗا

Enyi mlioamini, haifai kwenu kuwafanya wake wa baba zenu ni miongoni mwa mali yalioachwa kurithiwa, mkawa mnafanya mtakavyo kwao: kwa kuwaoa, kuwakataza wasiolewe au kuwaoza waume wengine, hali ya kuwa wao hawayataki hayo yote. Na pia haifai kwenu kuwadhuru wake zenu kwa kuwa mnawachukia, ili wapate kusamehe baadhi ya mlivyowapa, mahari au vinginevyo. Isipokuwa wakiwa wamefanya jambo ovu, kama uzinifu, hapo mnayo nafasi ya kuwazuia mpaka mkitwae mlichowapa. Na kule kukaa kwenu na wake zenu yatakikana kuwe ni juu ya misingi ya heshima na mapenzi na kuwatekelezea haki zao. Na iwapo mtawachukia kwa sababu yoyote katika sababu za kidunia, basi kuweni na subira. Kwani huenda mkachukia jambo, miongoni mwa mambo, na ikawa ndani yake muna kheri nyingi. info
التفاسير: