Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Vertimas į suahilių k. - Abdullah Muchamed ir Nasir Khamis

Puslapio numeris:close

external-link copy
114 : 4

۞ لَّا خَيۡرَ فِي كَثِيرٖ مِّن نَّجۡوَىٰهُمۡ إِلَّا مَنۡ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوۡ مَعۡرُوفٍ أَوۡ إِصۡلَٰحِۭ بَيۡنَ ٱلنَّاسِۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ ٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِ ٱللَّهِ فَسَوۡفَ نُؤۡتِيهِ أَجۡرًا عَظِيمٗا

Hakuna manufaa katika mengi ya maneno ya watu ya siri baina yao, isipokuwa yawapo ni mazungumzo yenye kuita kwenye kufanya mema ya utoaji sadaka au maneno mazuri au kuleta upatanishi baina ya watu. Na mwenye kuyafanya mambo hayo, kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, akitarajia thawabu Zake, tutampa thawabu nyingi zilizo kunjufu. info
التفاسير:

external-link copy
115 : 4

وَمَن يُشَاقِقِ ٱلرَّسُولَ مِنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ ٱلۡهُدَىٰ وَيَتَّبِعۡ غَيۡرَ سَبِيلِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ نُوَلِّهِۦ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصۡلِهِۦ جَهَنَّمَۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرًا

Na mwenye kuenda kinyume na Mtume , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye baada ya kubainikiwa na haki na akafuata njia isiyokuwa njia ya Waumini na haki ambayo wako nayo, basi tutamuacha na muelekeo wake, hatutamuongoza kwenye heri na tutamtia ndani ya Moto wa Jahanamu, akiteseka kwa joto lake. Ni mabaya yaliyoje marejeo haya kuwa ndio mwisho wa mtu! info
التفاسير:

external-link copy
116 : 4

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا

Hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Hasamehe Akishirikishwa na Anasamehe madhambi yaliyo chini ya ushirikina kwa Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na mwenye kumfanyia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Aliye Mmoja, Aliye Pekee, mshirika yoyote, miongoni mwa waja Wake, atakuwa yuko mbali sana na haki. info
التفاسير:

external-link copy
117 : 4

إِن يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ إِنَٰثٗا وَإِن يَدۡعُونَ إِلَّا شَيۡطَٰنٗا مَّرِيدٗا

Vile wanavyoviabudu washirikina badala ya Mwenyezi Mungu si chochote isipokuwa ni masanamu yasiyonufaisha wala kudhuru, na hawaabudu isipokuwa Shetani aliyemuasi Mwenyezi Mungu aliyefikia kiasi kikubwa cha kuharibika na kuharibu. info
التفاسير:

external-link copy
118 : 4

لَّعَنَهُ ٱللَّهُۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنۡ عِبَادِكَ نَصِيبٗا مَّفۡرُوضٗا

Mwenyezi Mungu Alimfukuza kwenye rehema Yake. Na Shetani Akasema, «Nitalichukua fungu maalumu la waja wako niwapoteze kimaneno na kivitendo. info
التفاسير:

external-link copy
119 : 4

وَلَأُضِلَّنَّهُمۡ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمۡ وَلَأٓمُرَنَّهُمۡ فَلَيُبَتِّكُنَّ ءَاذَانَ ٱلۡأَنۡعَٰمِ وَلَأٓمُرَنَّهُمۡ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلۡقَ ٱللَّهِۚ وَمَن يَتَّخِذِ ٱلشَّيۡطَٰنَ وَلِيّٗا مِّن دُونِ ٱللَّهِ فَقَدۡ خَسِرَ خُسۡرَانٗا مُّبِينٗا

«Na nitawaepusha na haki wenye kunifuata, nitawaahidi kwa urongo mambo wanayoyatamani, nitawaita wayakate na kuyapasua masikio ya wanyama-hoa kwa kuwapambia walifanye jambo hili la ubatili na nitawalingania wageuze umbo la Mwenyezi Mungu Alilowaumbia nalo katika tabia za kimaumbile na hali ya viumbe vile walivyo.» Na mwenye kukubali mwito wa Shetani na kumfanya yeye ndiye muokozi wake badala ya Mwenyezi Mungu, ameangamia maangamivu yaliyo wazi. info
التفاسير:

external-link copy
120 : 4

يَعِدُهُمۡ وَيُمَنِّيهِمۡۖ وَمَا يَعِدُهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ إِلَّا غُرُورًا

Shetani anawaahidi wafuasi wake ahadi za urongo na anawavutia kwa matamanio ya urongo yenye udanganyifu; ahadi zake kwao hazikuwa isipokuwa ni udanganyifu usio na ukweli wala dalili. info
التفاسير:

external-link copy
121 : 4

أُوْلَٰٓئِكَ مَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُ وَلَا يَجِدُونَ عَنۡهَا مَحِيصٗا

Hao marejeo yao ni Jahanamu; na hawatapata mapenyo wala mahali pa kukimbilia ili kuepukana nayo. info
التفاسير: