Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Vertimas į suahilių k. - Abdullah Muchamed ir Nasir Khamis

Puslapio numeris:close

external-link copy
12 : 4

۞ وَلَكُمۡ نِصۡفُ مَا تَرَكَ أَزۡوَٰجُكُمۡ إِن لَّمۡ يَكُن لَّهُنَّ وَلَدٞۚ فَإِن كَانَ لَهُنَّ وَلَدٞ فَلَكُمُ ٱلرُّبُعُ مِمَّا تَرَكۡنَۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ يُوصِينَ بِهَآ أَوۡ دَيۡنٖۚ وَلَهُنَّ ٱلرُّبُعُ مِمَّا تَرَكۡتُمۡ إِن لَّمۡ يَكُن لَّكُمۡ وَلَدٞۚ فَإِن كَانَ لَكُمۡ وَلَدٞ فَلَهُنَّ ٱلثُّمُنُ مِمَّا تَرَكۡتُمۚ مِّنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ تُوصُونَ بِهَآ أَوۡ دَيۡنٖۗ وَإِن كَانَ رَجُلٞ يُورَثُ كَلَٰلَةً أَوِ ٱمۡرَأَةٞ وَلَهُۥٓ أَخٌ أَوۡ أُخۡتٞ فَلِكُلِّ وَٰحِدٖ مِّنۡهُمَا ٱلسُّدُسُۚ فَإِن كَانُوٓاْ أَكۡثَرَ مِن ذَٰلِكَ فَهُمۡ شُرَكَآءُ فِي ٱلثُّلُثِۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ يُوصَىٰ بِهَآ أَوۡ دَيۡنٍ غَيۡرَ مُضَآرّٖۚ وَصِيَّةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَلِيمٞ

Na nyinyi, enyi wanaume, muna nusu ya kilioachwa na wake zenu baada ya kufa kwao, iwapo hawana watoto wa kiume au wa kike, na ikiwa wana watoto, basi mtapata robo ya walichokiacha ambacho mtakirithi baada ya kutekeleza wasia wao unaofaa au baada ya kulipa deni lao kwa wastahiki. Na wake zenu, enyi waume, watapata robo ya mlichokiacha iwapo hamuna mwana wa kiume au wa kike kutoka kwao, hao wake zenu, au wengineo mliokuwa mumewaoa. Na iwapo mtakuwa na mwana wa kiume au wa kike, basi hao wake zenu watapata thumni ya mlichokiacha. Hiyo robo au thumni itagawanywa kati yao; na iwapo ni mke mmoja, basi hiyo robo au thumni itakuwa ndio fungu lake. Hii ni baada ya kutekeleza kile mlichousia kitekelezwe katika nyasia zifaazo, au kulipa deni lenu. Na iwapo mwanamume au mwanamke atakufa, na akawa hana mwana wala mzazi, na akawa na ndugu mmoja wa kwa mama, wa kiume au wa kike, basi kila mmoja kati yao wawili atapata sudusi; wakiwa ni zaidi ya mmoja watashirikiana katika theluthi itakayogawanywa baina yao kwa usawa bila kutafautisha baina ya mwanamume na mwanamke. Hili ndilo fungu Alilowaekea Mwenyezi Mungu ndugu wa kwa mama, wa kiume na wa kike, likiwa ni urithi wao, baada ya kutekeleza wasia wa aliyekufa iwapo aliusia chochote ambacho hakina madhara kwa mawarithi au baada ya kulipa madeni yake. Kwa hili Amewausia Mola wenu, wasia wenye manufaa kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi mno kwa yanayowafaa viumbe Wake, ni Mpole, Hana haraka ya kuwaadhibu. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 4

تِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۚ وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ يُدۡخِلۡهُ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Hukumu hizo za Kimungu zilizowekwa na Mwenyezi Mungu, kuhusu mayatima, wanawake na mirathi, ni Sheria Zake zioneshazo kuwa zinatoka kwa Mwenyezi Mungu Aliye Mjuzi, Aliye Mwingi wa hekima. Na yoyote mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika hukumu hizi na nyenginezo zilizowekwa na Mwenyezi Mungu kwa waja Wake, Atamuingiza kwenye mabustani ya Peponi, yenye miti mingi na majumba ya fahari mengi, inayopita chini yake mito yenye maji tamu. Watasalia kwenye neema hii, hawatoki humo. Malipo hayo ndio kufuzu kukubwa. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 4

وَمَن يَعۡصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُۥ يُدۡخِلۡهُ نَارًا خَٰلِدٗا فِيهَا وَلَهُۥ عَذَابٞ مُّهِينٞ

Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake , kwa kuzikanusha hukumu za Mwenyezi Mungu na kuzikiuka Sheria Zake kwa waja Wake, kwa kuzibadilisha au kuacha kuzitumia, huyo Atamuingiza Motoni, adumu humo; na atapata adhabu ya kumtweza na kumfanya mnyonge. info
التفاسير: