Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Vertimas į suahilių k. - Abdullah Muchamed ir Nasir Khamis

Puslapio numeris:close

external-link copy
95 : 4

لَّا يَسۡتَوِي ٱلۡقَٰعِدُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ غَيۡرُ أُوْلِي ٱلضَّرَرِ وَٱلۡمُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡۚ فَضَّلَ ٱللَّهُ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ عَلَى ٱلۡقَٰعِدِينَ دَرَجَةٗۚ وَكُلّٗا وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَفَضَّلَ ٱللَّهُ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ عَلَى ٱلۡقَٰعِدِينَ أَجۡرًا عَظِيمٗا

Wenye kusalia nyuma wakaacha kuhudhuria jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa wenye nyudhuru kati yao, hawalingani na wenye kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amewafadhilisha wenye kupigana jihadi juu ya wenye kukaa na Ameitukuza daraja yao Peponi kwa kiwango cha juu. Na Mwenyezi Mungu Amewaahidi wote: wenye kupigana jihadi kwa mali yao na kwa nafsi zao na wenye kukaa, miongoni mwa watu wenye nyudhuru, kwa kutoa kwao na kujitolea katika njia ya haki. Na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amewafadhilisha wale wenye kupigana jihadi juu ya wenye kukaa kwa kuwapa thawabu nyingi. info
التفاسير:

external-link copy
96 : 4

دَرَجَٰتٖ مِّنۡهُ وَمَغۡفِرَةٗ وَرَحۡمَةٗۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمًا

Thawabu nyingi hizi ni daraja za juu, katika mabustani ya Pepo, zitokazo kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, walizopewa waja Wake maalumu wenye kupigana katika njia Yake, na msamaha wa madhambi yao na rehema kunjufu ambayo ndani yake wananeemeshwa. Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa anayetubia Kwake na kurejea, ni Mwingi wa rehema kwa wenye kumtii, wenye kupigana jihadi katika njia Yake. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 4

إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ ظَالِمِيٓ أَنفُسِهِمۡ قَالُواْ فِيمَ كُنتُمۡۖ قَالُواْ كُنَّا مُسۡتَضۡعَفِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ قَالُوٓاْ أَلَمۡ تَكُنۡ أَرۡضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةٗ فَتُهَاجِرُواْ فِيهَاۚ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرًا

Hakika wale ambao Malaika waliwafisha na wao wako katika hali ya kujidhulumu wenyewe kwa kukaa katika nchi ya ukafiri na kuacha kuhama, Malaika watawaambia kwa njia ya kuwalaumu, «Mlikuwa katika nini kuhusu mambo ya Dini yenu?’ watasema, «Tulikuwa wanyonge nchini kwetu, tumelemewa kuweza kujiepushia dhuluma na maonevu.» Malaika watawaambia kwa njia ya kuwalaumu, «Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa kunjufu mkatoka kwenye ardhi yenu mkaenda ardhi nyingine ambapo mtaaminika na Dini yenu?» Basi hao makao yao ni Moto. Na haya ni makao mabaya ya mtu kuishilia. info
التفاسير:

external-link copy
98 : 4

إِلَّا ٱلۡمُسۡتَضۡعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلۡوِلۡدَٰنِ لَا يَسۡتَطِيعُونَ حِيلَةٗ وَلَا يَهۡتَدُونَ سَبِيلٗا

Wataepushwa na mwisho huo wakongwe wanaume na wanawake na watoto ambao hawawezi kujiondolea udhalimu na uonevu na hawajui njia yoyote ya kuwaokoa wao na mateso. info
التفاسير:

external-link copy
99 : 4

فَأُوْلَٰٓئِكَ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَعۡفُوَ عَنۡهُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَفُوًّا غَفُورٗا

Wanyonge hawa ndio wanaotarajiwa kupata msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, kwa kuwa Yeye Anaujua uhakika wa mambo yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Anawasamehe makosa yao na Anawafinikia na kuwasitiria. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 4

۞ وَمَن يُهَاجِرۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ يَجِدۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُرَٰغَمٗا كَثِيرٗا وَسَعَةٗۚ وَمَن يَخۡرُجۡ مِنۢ بَيۡتِهِۦ مُهَاجِرًا إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ يُدۡرِكۡهُ ٱلۡمَوۡتُ فَقَدۡ وَقَعَ أَجۡرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا

Na yoyote mwenye kutoka kwenye ardhi ya ushirikina kwenda kwenye ardhi ya Uislamu kwa ajili ya kukimbia na dini Yake, akitaraji fadhila za Mola wake na akikusudia kuinusuru dini Yake, atapata katika ardhi mahali pa kuelekea ambapo ataneemeka, pawe ni sababu ya yeye kupata nguvu na maadui zake kuwa wanyonge, pamoja na kupata ukunjufu wa riziki na maisha. Na yoyote mwenye kutoka nyumbani kwake kwa lengo la kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye na kulitukuza neno la Mwenyezi Mungu kisha akapatikana na kifo kabla ya kufikia lengo lake, basi malipo ya kitendo chake yameshathibiti kwa Mwenyezi Mungu, kwa fadhila Zake na wema Wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, ni Mwingi wa huruma kwa waja Wake. info
التفاسير:

external-link copy
101 : 4

وَإِذَا ضَرَبۡتُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَقۡصُرُواْ مِنَ ٱلصَّلَوٰةِ إِنۡ خِفۡتُمۡ أَن يَفۡتِنَكُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْۚ إِنَّ ٱلۡكَٰفِرِينَ كَانُواْ لَكُمۡ عَدُوّٗا مُّبِينٗا

Na mnaposafiri, enyi Waumini, kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, hamuna makosa wala dhambi kukupunguza Swala, mkiogopa kufanyiwa uadui na makafiri mkiwa kwenye Swala. Safari nyinygi za Waislamu, katika mwanzo wa Uislamu, zilikuwa za kutisha. Na kupunguza Swala ni ruhusa iliyotolewa kwenye safari, katika hali ya amani au vitisho. Hakika makafiri ni wenye kudhihirisha uadui wao kwenu, basi jihadharini nao. info
التفاسير: