Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Əli Muhsin əl-Bərvani.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
53 : 3

رَبَّنَآ ءَامَنَّا بِمَآ أَنزَلۡتَ وَٱتَّبَعۡنَا ٱلرَّسُولَ فَٱكۡتُبۡنَا مَعَ ٱلشَّٰهِدِينَ

Mola wetu Mlezi! Tumeyaamini uliyo yateremsha, na tumemfuata huyu Mtume, basi tuandike pamoja na wanao shuhudia. info

Na sisi tunasema: Ewe Mola Mlezi wetu! Tumekisadiki Kitabu chako ulicho mteremshia Nabii wako, na tunaifuata amri ya Mtume wako, Isa a.s. Basi tuthibitishe kuwa miongoni mwa wenye kumshuhudia Mtume wako katika kufikisha ujumbe, na kuwashuhudia Wana wa Israili katika ukafiri wao na upinzani wao.

التفاسير:

external-link copy
54 : 3

وَمَكَرُواْ وَمَكَرَ ٱللَّهُۖ وَٱللَّهُ خَيۡرُ ٱلۡمَٰكِرِينَ

Na Makafiri walipanga mipango na Mwenyezi Mungu akapanga mipango, na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wenye kupanga. info

Ama hao makafiri wapinzani walipanga njama za chini kwa chini kuupiga vita wito (Da'wa) wa Isa. Mwenyezi Mungu alizibat'ilisha njama zao, wasifanikiwe kuyapata waliyo yakusudia. Na Mwenyezi Mungu kwa hikima yake anawashinda watu wote wafanyao hila.

التفاسير:

external-link copy
55 : 3

إِذۡ قَالَ ٱللَّهُ يَٰعِيسَىٰٓ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَجَاعِلُ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوكَ فَوۡقَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِۖ ثُمَّ إِلَيَّ مَرۡجِعُكُمۡ فَأَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡ فِيمَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ

Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata juu ya wale walio kufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyo kuwa mkikhitalifiana. info

Taja ewe Nabii, pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa Mimi nitakutimizia ajali yako,(yaani nitakufisha kifo cha kawaida kama alivyo sema Ibn Abbas r.a. Taz. Ibn Kathir) wala sitamwezesha mtu yeyote kukuuwa. Nami nitakunyanyua pahala pa utukufu wangu, na nitakuepusha na maadui wako wanao kusudia kukuuwa, na nitawafanya wanao kufuata wasio kengeuka na dini yako, wawe na nguvu na utawala juu ya wale wasio fuata uwongofu wako, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu ni Akhera. Hapo nitawahukumu katika hayo mlio kuwa mkizozana kwayo katika mambo ya dini.

التفاسير:

external-link copy
56 : 3

فَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَأُعَذِّبُهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدٗا فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّٰصِرِينَ

Ama wale walio kufuru, nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na Akhera, wala hawatapata wa kuwanusuru. info

Ama wale wanao kataa kwa ukafiri nitawaonjesha adhabu ya hizaya na mateso kwa kuwasalitisha mataifa mengine juu yao katika dunia, na hakika adhabu ya Akhera ni kali zaidi na ina hizaya zaidi. Na wala hawana wa kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
57 : 3

وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فَيُوَفِّيهِمۡ أُجُورَهُمۡۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلظَّٰلِمِينَ

Na ama wale walio amini na wakatenda mema basi Mwenyezi Mungu atawalipa ujira wao kaamili. Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhaalimu. info

Na ama walio ongoka kwa uwongofu wa Mwenyezi Mungu, wakatenda vitendo vya kufuata mwendo wa kheri, Mwenyezi Mungu atawapa malipo ya kutosha kwa hizo a'mali zao. Na ndiyo shani yake Mwenyezi Mungu kuwa hawalipi thawabu zake wale wanao pindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu wakafanya jeuri ya kutoitikia wito wake na kumtendea wema. Wala hawanyanyulii cheo chao.

التفاسير:

external-link copy
58 : 3

ذَٰلِكَ نَتۡلُوهُ عَلَيۡكَ مِنَ ٱلۡأٓيَٰتِ وَٱلذِّكۡرِ ٱلۡحَكِيمِ

Haya tunayo kusomea ni katika Aya na Ukumbusho wenye hikima. info

Hayo tuliyo kusimulia ni miongoni ya hoja zenye kuonyesha ukweli wa ujumbe wako, nayo ni katika Qur'ani Tukufu yenye kukumbusha, na yenye kukusanya ilimu ya manufaa.

التفاسير:

external-link copy
59 : 3

إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ ٱللَّهِ كَمَثَلِ ءَادَمَۖ خَلَقَهُۥ مِن تُرَابٖ ثُمَّ قَالَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa. info

Baadhi ya watu wamepotea katika kadhiya ya Isa, wakadai ati kuwa yeye ni Mwana wa Mwenyezi Mungu kwa kuwa kazaliwa bila ya baba. Mwenyezi Mungu anawaambia: Hakika shani ya Isa katika kuumbwa kwake bila ya baba ni kama shani ya Adam alivyo umbwa kwa udongo bila ya baba wala mama. Mwenyezi Mungu alimfanya na akataka awe, akawa mtu sawasawa.

التفاسير:

external-link copy
60 : 3

ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ

Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanao fanya shaka. info

Bayana hii katika kuumbwa Isa ndiyo ukweli wenyewe ambao unabainisha hakika yaliyo tokea katika khabari za Mola Mlezi wa viumbe vyote. Basi wewe dumu katika yakini yako wala usiwe katika wenye kutia shaka.

التفاسير:

external-link copy
61 : 3

فَمَنۡ حَآجَّكَ فِيهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ فَقُلۡ تَعَالَوۡاْ نَدۡعُ أَبۡنَآءَنَا وَأَبۡنَآءَكُمۡ وَنِسَآءَنَا وَنِسَآءَكُمۡ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمۡ ثُمَّ نَبۡتَهِلۡ فَنَجۡعَل لَّعۡنَتَ ٱللَّهِ عَلَى ٱلۡكَٰذِبِينَ

Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikilia ilimu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wake zetu na wake zenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo. info

Basi wenye kujadiliana nawe, ewe Nabii, katika shani ya Isa baada ya kukujia wewe khabari iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu na ambayo haina ubabaifu ndani yake, basi waambie kauli itakayo dhihirisha ujuzi wako wa yakini na upotovu wao wa uwongo: Njooni! Kila mmoja wetu na wenu awaite watoto wake, na wakeze na wenyewe nafsi zao. Kisha tumnyenyekee Mwenyezi Mungu kumtaka ateremshe ghadhabu yake na nakama yake juu ya aliye mwongo katika hili jambo la Isa kuzaliwa bila ya baba na kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu wala si Mwana wa Mungu.

التفاسير: