Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Əli Muhsin əl-Bərvani.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
84 : 3

قُلۡ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا وَمَآ أُنزِلَ عَلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَمَآ أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَٱلنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمۡ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّنۡهُمۡ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ

Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyo teremshiwa sisi, na aliyo teremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wajukuu zao, na aliyo pewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi ni wenye kusilimu kwake. info

Mwenyezi Mungu ametilia mkazo kuwa Yeye ni Mmoja, na Ujumbe wake ni mmoja. Amemuamrisha Nabii wake na walio pamoja naye wasema: Tumesadiki kuwa Mwenyezi Mungu ndiye peke yake anaye faa kuabudiwa, na ndiye anaye watuma Mitume wake. Na tumeiamini Qur'ani na Sharia aliyo tuteremshia Mwenyezi Mungu, na pia tumeamini Vitabu na Sharia alizo wateremshia Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na watoto wao thinaashara, na aliyo teremsha Mwenyezi Mungu kwa Musa, nayo ni Taurati, na kwa Isa, nayo ni Injili, na walio teremshiwa Manabii wote walio baki. Hapana khitilafu katika kuamini baina ya yeyote katika wao. Na sisi kwa hivyo tumeuelekeza uso wetu kwa Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
85 : 3

وَمَن يَبۡتَغِ غَيۡرَ ٱلۡإِسۡلَٰمِ دِينٗا فَلَن يُقۡبَلَ مِنۡهُ وَهُوَ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Na anaye tafuta Dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri. info

Baada ya kupata utume Muhammad s.a.w. akitaka mtu Dini na sharia zisio kuwa Dini ya Islamu na Sharia yake, Mwenyezi Mungu hatamkubalia. Na malipo ya mtu huyo Siku ya Malipo ni kuwa miongoni mwa walio zikhasiri nafsi zao, ikawajibikia adhabu chungu.

التفاسير:

external-link copy
86 : 3

كَيۡفَ يَهۡدِي ٱللَّهُ قَوۡمٗا كَفَرُواْ بَعۡدَ إِيمَٰنِهِمۡ وَشَهِدُوٓاْ أَنَّ ٱلرَّسُولَ حَقّٞ وَجَآءَهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Mwenyezi Mungu atawaongoaje watu walio kufuru baada ya kuamini kwao, na wakashuhudia ya kuwa Mtume huyu ni wa haki, na zikawafikia hoja zilizo wazi? Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu. info

Mwenyezi Mungu hakubaliani na watu walio kwisha shuhudia kuwa Mtume ni wa haki, na zikawajia dalili za kuonyesha hayo, kisha baada ya yote hayo wakamkataa, na wakakataa miujiza yake. Huo basi ni udhaalimu wao, na Mwenyezi Mungu hakubaliani na madhaalimu.

التفاسير:

external-link copy
87 : 3

أُوْلَٰٓئِكَ جَزَآؤُهُمۡ أَنَّ عَلَيۡهِمۡ لَعۡنَةَ ٱللَّهِ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ وَٱلنَّاسِ أَجۡمَعِينَ

Hao malipo yao ni kuwa ipo juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote. info

Adhabu ya watu hao wataipata kutoka kwa Mwenyezi Mungu kama wanavyo stahiki kukasirika kwake juu yao, na laana yake, na laana ya bora ya viumbe vyake miongoni mwa Malaika na wanaadamu.

التفاسير:

external-link copy
88 : 3

خَٰلِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ

Humo watadumu. Hawatapunguziwa adhabu wala hawatapewa nafasi. info

Laana hiyo haitowabanduka, wala hawatapunguziwa adhabu, wala hawapewi muhula.

التفاسير:

external-link copy
89 : 3

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. info

Lakini wale ambao wamejing'oa na madhambi yao, wakaingia kati ya watu wema, wakayaondoa waliyo yaharibu, basi hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu atawafutia madhambi yao, kwani maghfira na rehema ni miongoni mwa sifa za dhati yake Tukufu.

التفاسير:

external-link copy
90 : 3

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بَعۡدَ إِيمَٰنِهِمۡ ثُمَّ ٱزۡدَادُواْ كُفۡرٗا لَّن تُقۡبَلَ تَوۡبَتُهُمۡ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلضَّآلُّونَ

Hakika wale walio kufuru baada ya kuamini kwao, kisha wakazidi kukufuru, toba yao haitakubaliwa, na hao ndio walio potea. info

Kukubaliwa toba na kupata rehema ya maghfira kunashurutishwa mtu adumu juu ya Imani. Wanao ipinga Haki baada ya ut'iifu na kusadiki, na wakazidisha upinzani na ufisadi na kuwaudhi Waumini, Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la hatokubali toba yao. Haiwezi kuwa toba yao hiyo ni kweli na safi na hali wanaendelea na vitendo vyao, wapo mbali na Haki na wanaigeuzia nyuso zao.

التفاسير:

external-link copy
91 : 3

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَمَاتُواْ وَهُمۡ كُفَّارٞ فَلَن يُقۡبَلَ مِنۡ أَحَدِهِم مِّلۡءُ ٱلۡأَرۡضِ ذَهَبٗا وَلَوِ ٱفۡتَدَىٰ بِهِۦٓۗ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ وَمَا لَهُم مِّن نَّٰصِرِينَ

Hakika wale walio kufuru, na wakafa hali ni makafiri haitakubaliwa kutoka kwa yeyote wao fidia ya dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wangeli itoa. Hao watapata adhabu chungu, wala hawatakuwa na wa kuwanusuru. info

Wale wanao ipinga Haki wala hawaifuati, na wanaendelea na uwovu wao mpaka wakafa nao ni wapinzani tu, basi yeyote miongoni mwao hawezi kujitolea fidia ya kujiepusha na adhabu ya Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la, hata ikawa anacho kitoa kuwa fidia ni dhahabu ya kujaza dunia nzima kama angeweza. Na adhabu yao ina uchungu mkali.

التفاسير: