Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Abdullah Məhəmməd və Nasir Xamis.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
246 : 2

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلۡمَلَإِ مِنۢ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ مِنۢ بَعۡدِ مُوسَىٰٓ إِذۡ قَالُواْ لِنَبِيّٖ لَّهُمُ ٱبۡعَثۡ لَنَا مَلِكٗا نُّقَٰتِلۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ قَالَ هَلۡ عَسَيۡتُمۡ إِن كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِتَالُ أَلَّا تُقَٰتِلُواْۖ قَالُواْ وَمَا لَنَآ أَلَّا نُقَٰتِلَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَقَدۡ أُخۡرِجۡنَا مِن دِيَٰرِنَا وَأَبۡنَآئِنَاۖ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقِتَالُ تَوَلَّوۡاْ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِٱلظَّٰلِمِينَ

Kwani hukukijua, ewe Mtume, kisa cha watukufu na mabwana, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, baada ya zama za Musa kupita? Walipomtaka Mtume wao amtawalishe kwao mfalme, wapate kukusanyika chini ya uongozi wake na wapate kupigana na maadui zao katika njia ya Mwenyezi Mungu. Nabii wao akawaambia, «Je, mambo ni kama vile ninavyoyatarajia kwamba lau mtafaradhiwa kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa hamtapigana? Kwani mimi nachelea mtaogopa na mtakimbia vitani.» Wakasema wakikanusha matarajio ya Nabii wao, «Ni kizuizi kipi kitakacho kutuzuia tusipigane katika njia ya Mwenyezi Mungu, ambapo adui yetu ametutoa kwenye Makao yetu na akatutenganisha na na watoto wetu kwa kutuua na kututeka?» Basi Mwenyezi Mungu Alipowafaradhia kupigana wakiwa na mfalme Aliyewachagulia walikuwa waoga na wakakimbia vitani, isipokuwa wachache kati yao waliojikita imara kwa fadhila za Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Anawajua mno madhalimu, wenye kuzivunja ahadi zao. info
التفاسير:

external-link copy
247 : 2

وَقَالَ لَهُمۡ نَبِيُّهُمۡ إِنَّ ٱللَّهَ قَدۡ بَعَثَ لَكُمۡ طَالُوتَ مَلِكٗاۚ قَالُوٓاْ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ ٱلۡمُلۡكُ عَلَيۡنَا وَنَحۡنُ أَحَقُّ بِٱلۡمُلۡكِ مِنۡهُ وَلَمۡ يُؤۡتَ سَعَةٗ مِّنَ ٱلۡمَالِۚ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ ٱصۡطَفَىٰهُ عَلَيۡكُمۡ وَزَادَهُۥ بَسۡطَةٗ فِي ٱلۡعِلۡمِ وَٱلۡجِسۡمِۖ وَٱللَّهُ يُؤۡتِي مُلۡكَهُۥ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ

Na Mtume wao aliwaambia, «Hakika Mwenyezi Mungu Amewaltea Tālūt kuwa ni mfalme, ikiwa ni kuyaitikia maombi yenu, ili awaongoze katika kupigana na adui yenu kama mlivyoomba.» Wakasema wakuu wa Wana wa Isrāīl, «Vipi Tālūt atakuwa mfalme kwetu, hali yeye hastahiki hilo? Yeye si katika wajukuu wa wafalme, wala hatoki kwenye nyumba ya utume na wala hakupewa ukunjufu wa mali ya kujisaidia nayo katika ufalme wake. Sisi tuna haki zaidi ya huu ufalme kuliko yeye. Kwani sisi ni wajukuu wa wafalme na tunatoka kwenye nyumba ya utume.» Mtume wao akawaambia, «Hakika Mwenyezi Mungu Amewachagulia, na Yeye, Aliyetakasika na kila sifa mbaya, Anayajua zaidi mambo ya waja Wake, na Amemuengezea ukunjufu wa elimu na nguvu ya mwili ya kupigana na adui. Na Mwenyezi Mungu ni Mmiliki wa ufalme. Anampa ufalme wake Anayemtaka katika waja wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa fadhila na utoaji, ni Mjuzi kabisa wa ukweli wa mambo, hapana chenye kufichika Kwake.» info
التفاسير:

external-link copy
248 : 2

وَقَالَ لَهُمۡ نَبِيُّهُمۡ إِنَّ ءَايَةَ مُلۡكِهِۦٓ أَن يَأۡتِيَكُمُ ٱلتَّابُوتُ فِيهِ سَكِينَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَبَقِيَّةٞ مِّمَّا تَرَكَ ءَالُ مُوسَىٰ وَءَالُ هَٰرُونَ تَحۡمِلُهُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Mtume wao aliwaambia, «Hakika alama ya ufalme wake ni kuwajilieni sanduku ambalo ndani yake muna Taurati,- Sanduku ambalo maadui wao walikuwa wamewanyang’anya-. Ndani yake muna utulivu kutoka kwa Mola wenu unaozithibitisha nyoyo za wenye ikhlasi. Na muna ndani yake mabaki ya vitu vilivyoachwa na jamaa za Musa na jamaa za Hārūn, kama fimbo na vipande vya mbao, yanabebwa na Malaika. Hakika muna katika hayo hoja kubwa kuwa Tālūt amechaguliwa kuwa mfalme wenu kwa amri ya Mwenyezi Mungu, iwapo mnamuamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake.» info
التفاسير: