Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Abdullah Məhəmməd və Nasir Xamis.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
170 : 2

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّبِعُواْ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُواْ بَلۡ نَتَّبِعُ مَآ أَلۡفَيۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَآۚ أَوَلَوۡ كَانَ ءَابَآؤُهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ شَيۡـٔٗا وَلَا يَهۡتَدُونَ

Na pindi Waumini wasemapo, wakiwanasihi viongozi wa upotofu, «Fuateni Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Qur’ani na uongofu,» wao huendelea kuwa wakakamavu katika kuwaigiza wakale wao washirikina, huku wakisema, «Hatufuati dini yenu, bali tunayafuata yale tuliyowakuta wazazi wetu wakiyafanya.» Wanawafuata baba zao hata kama walikuwa hawaelewi chochote kutoka kwa Mwenyezi Mungu wala hawana muelekeo wowote? info
التفاسير:

external-link copy
171 : 2

وَمَثَلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ كَمَثَلِ ٱلَّذِي يَنۡعِقُ بِمَا لَا يَسۡمَعُ إِلَّا دُعَآءٗ وَنِدَآءٗۚ صُمُّۢ بُكۡمٌ عُمۡيٞ فَهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ

Na sifa za waliokufuru na wale walinganizi wao katika uongofu na imani ni kama sifa ya mchunga anayewapigia kelele wanyama na kuwakaripia, hali wao hawaelewi maana ya maneno yake isipokuwa wanasikia mwito na mlio wa sauti tu. Makafiri hao ni viziwi wameziba masikizi yao wasisikie haki, ni mabubu wamezifunga ndimi zao wasiitamke haki, ni vipofu macho yao hayazioni hoja za haki zilizo wazi. Kwa hivyo, wao hawatumii akili zao kwa mambo yenye kuwafaa. info
التفاسير:

external-link copy
172 : 2

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡ وَٱشۡكُرُواْ لِلَّهِ إِن كُنتُمۡ إِيَّاهُ تَعۡبُدُونَ

Enyi Waumini, kuleni katika vyakula mnavyovipenda vilivyo halali ambavyo tumewaruzuku, wala msiwe kama makafiri ambao wanaviharamisha vizuri na kuvihalalisha viovu na mumshukurie Mwenyezi Mungu neema Zake kubwa kwenu kwa nyoyo zenu, ndimi zenu na viungo vyenu, iwapo kwa kweli nyinyi mnafuata amri Yake, ni wenye kusikia na kumtii Yeye, mnamuabudu Yeye Peke Yake Asiyekuwa na mshirika. info
التفاسير:

external-link copy
173 : 2

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحۡمَ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ بِهِۦ لِغَيۡرِ ٱللَّهِۖ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ غَيۡرَ بَاغٖ وَلَا عَادٖ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Hakika Mwenyezi Mungu Amewaharamishia nyinyi kinachowadhuru, kama mfu ambaye hakuchinjwa kwa njia ya kisheria, na damu inayotiririka, na nyama ya nguruwe, na vichinjwa ambavyo vilikusudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Na katika wema wa Mwenyezi Mungu na usahilishaji Wake kwenu ni kwamba Amewahalalishia nyinyi kuvila vitu hivi vilivyoharamishwa wakati wa dharura. Hivyo basi, yoyote ambaye dharura ilimpelekea kula kitu katika hivyo, pasi na kuwa ni mwenye kudhulumu katika kula kwake kwa kupitisha kipimo cha haja yake, wala kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu katika yale aliyohalalishiwa, basi huyo hana dhambi kwa hilo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe waja Wake, ni Mwenye huruma kwao. info
التفاسير:

external-link copy
174 : 2

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡتُمُونَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَيَشۡتَرُونَ بِهِۦ ثَمَنٗا قَلِيلًا أُوْلَٰٓئِكَ مَا يَأۡكُلُونَ فِي بُطُونِهِمۡ إِلَّا ٱلنَّارَ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ ٱللَّهُ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Hakika wale wafichao yale Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika vitabu vyake miongoni mwa sifa za Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na mengineyo ya haki na wakawa na pupa la kuchukua badali ndogo ya pambo la maisha ya duniani kama malipo ya kuficha hayo. Hawa hawakili kile wakilacho kwa kuficha haki isipokuwa moto wa Jahanamu utakaokuwa ukiwaka kwa ukali katika matumbo yao. Wala Mwenyezi Mungu Hatasema nao Siku ya Kiyama kwa hasira Zake na machukivu Yake juu yao, wala Hatawatakasa na uchafu wa madhambi yao na ukafiri wao, na itawapata adhabu iumizayo. info
التفاسير:

external-link copy
175 : 2

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشۡتَرَوُاْ ٱلضَّلَٰلَةَ بِٱلۡهُدَىٰ وَٱلۡعَذَابَ بِٱلۡمَغۡفِرَةِۚ فَمَآ أَصۡبَرَهُمۡ عَلَى ٱلنَّارِ

Hao wanaosifika na sifa hizi wamechagua upotevu wakaacha uongofu, na wakachagua adhabu ya Mwenyezi Mungu wakaacha msamaha wake. Ni ujasiri ulioje wao wa kuchagua Moto kwa kufanya vitendo vya watu wa Motoni! Anastaajabu Mwenyezi Mungu kwa kujitokeza kwao kulifanya hilo. Basi oneni ajabu, enyi watu, juu ya ujasiri wao na uvumilivu wao kwenye Moto na kukaa kwao humo. Maneno haya yametumika kwa njia ya kuwatweza na kuwachezea. info
التفاسير:

external-link copy
176 : 2

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ نَزَّلَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّۗ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِي ٱلۡكِتَٰبِ لَفِي شِقَاقِۭ بَعِيدٖ

Adhabu hiyo ambayo wamestahili iwapate, ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu Ameteremsha Vitabu Vyake, kwa Mitume Wake, vikiwa ni vyenye kukusanya haki iliyo wazi, wakaikanusha haki hiyo. Na kwa hakika, wale waliohitalifiana katika Kitabu, wakaamini baadhi yake na kukanusha baadhi yake, wako katika ugonvi na mfarakano ulio mbali na uongofu na usawa. info
التفاسير: