Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Abdullah Məhəmməd və Nasir Xamis.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
220 : 2

فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۗ وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡيَتَٰمَىٰۖ قُلۡ إِصۡلَاحٞ لَّهُمۡ خَيۡرٞۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمۡ فَإِخۡوَٰنُكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ ٱلۡمُفۡسِدَ مِنَ ٱلۡمُصۡلِحِۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَأَعۡنَتَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

duniani na Akhera. Na wanakuuliza, ewe Mtume, kuhusu mayatima, waingiliane nao vipi katika maisha yao na mali yao. Waambie, «Kuwatengezea kwenu mambo yao ni bora. Basi, wafanyieni daima yanayowafaa wao zaidi.Na iwapo mtatangamana nao katika mambo ya maisha, basi wao ni ndugu zenu katika Dini. Na ni juu ya ndugu kuyalinda maslahi ya ndugu yake.Mwenyezi Mungu Anamjua mpotezaji wa mali ya mayatima na yule mwenye pupa la kuyahifadhi. Na lau Mwenyezi Mungu Angetaka, angewatia dhiki na mashaka kwa kuwaharamishia mtangamano. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwingi wa hekima katika uumbaji Wake, uendeshaji mambo Wake na upitishaji sheria Wake. info
التفاسير:

external-link copy
221 : 2

وَلَا تَنكِحُواْ ٱلۡمُشۡرِكَٰتِ حَتَّىٰ يُؤۡمِنَّۚ وَلَأَمَةٞ مُّؤۡمِنَةٌ خَيۡرٞ مِّن مُّشۡرِكَةٖ وَلَوۡ أَعۡجَبَتۡكُمۡۗ وَلَا تُنكِحُواْ ٱلۡمُشۡرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤۡمِنُواْۚ وَلَعَبۡدٞ مُّؤۡمِنٌ خَيۡرٞ مِّن مُّشۡرِكٖ وَلَوۡ أَعۡجَبَكُمۡۗ أُوْلَٰٓئِكَ يَدۡعُونَ إِلَى ٱلنَّارِۖ وَٱللَّهُ يَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱلۡجَنَّةِ وَٱلۡمَغۡفِرَةِ بِإِذۡنِهِۦۖ وَيُبَيِّنُ ءَايَٰتِهِۦ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ

Wala msiwaoe, enyi Waislamu, wanawake washirikina wanaoabudu masanamu mpaka waingie katika Uislamu. Na mjue kwamba mwanamke kijakazi, asiyekuwa na mali wala utukufu wa nasaba, anayemuamini Mwenyezi Mungu, ni bora kuliko mwanamke mshirikina, hata kama huyo mshirikina muungwana atawavutia. Wala msiwaoze wanawake wenu waumini, wakiwa ni vijakazi au waungwana, wanaume washirikina mpaka wamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Na mjue kwamba mtumwa mwenye Imani, pamoja na ufukara wake, ni bora kuliko mshirikina, hata kama huyo mshirikina atawavutia. Hao wasifikao na ushirikina, wanaume na wanawake, wanamwita kila atangamanaye nao kwenye mambo yapelekayo Motoni. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, Anawaita waja Wake kwenye dini Yake ya haki inayowapeleka Peponi na kusamehawa madhambi yao kwa idhini Yake. Na Yeye Anabainisha aya Zake na hukumu Zake kwa watu, ili wapate kukumbuka na wazingatie. info
التفاسير:

external-link copy
222 : 2

وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡمَحِيضِۖ قُلۡ هُوَ أَذٗى فَٱعۡتَزِلُواْ ٱلنِّسَآءَ فِي ٱلۡمَحِيضِ وَلَا تَقۡرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطۡهُرۡنَۖ فَإِذَا تَطَهَّرۡنَ فَأۡتُوهُنَّ مِنۡ حَيۡثُ أَمَرَكُمُ ٱللَّهُۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلتَّوَّٰبِينَ وَيُحِبُّ ٱلۡمُتَطَهِّرِينَ

Na wanakuuliza kuhusu hedhi, nayo ni damu inayotiririka kimaumbile kutoka kwenye uzao wa wanawake katika nyakati maalumu.Waambie, ewe Mtume, «Hiyo hedhi ni udhia wenye manyezi unaomdhuru mwenye kuusongelea. Hivyo basi, jiepusheni kuwaingilia wanawake kwenye kipindi cha hedhi mpaka damu ikome. Damu ikomapo, na wakaoga, waingilieni kupitia pale pahali Alipowahalalishia Mwenyezi Mungu, napo ni tupu ya mbele siyo ya nyuma. Hakika Mwenyezi Mungu Anawapenda waja Wake wenye kutubia na kuomba msamaha kwa wingi na Anawapenda waja Wake wenye kujisafisha ambao hujitenga na maovu na uchafu. info
التفاسير:

external-link copy
223 : 2

نِسَآؤُكُمۡ حَرۡثٞ لَّكُمۡ فَأۡتُواْ حَرۡثَكُمۡ أَنَّىٰ شِئۡتُمۡۖ وَقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُمۡۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُم مُّلَٰقُوهُۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Wake zenu ni pahali pa makulima yenu, mnaweka tone la manii ndani ya uzao wao, wakatoka humo watoto kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, waingilieni pale pahali pake pa kuingiliwa tu, napo ni tupu ya mbele, kwa namna yoyote mtakayo. Na zitangulizieni nafsi zenu amali njema kwa kuzitunga amri za Mwenyezi Mungu. Na muogopeni Mwenyezi Mungu na mjue kwamba mtakutana na Yeye kwa kuhesabiwe Siku ya Kiyama. Na wape bishara njema Waumini, ewe Nabii, kwa yale ambayo yatawafurahisha na kuwapendeza ya malipo mema huko Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
224 : 2

وَلَا تَجۡعَلُواْ ٱللَّهَ عُرۡضَةٗ لِّأَيۡمَٰنِكُمۡ أَن تَبَرُّواْ وَتَتَّقُواْ وَتُصۡلِحُواْ بَيۡنَ ٱلنَّاسِۚ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Wala msikifanye, enyi Waislamu, kiapo chenu kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni chenye kuwazuia nyinyi kufanya wema, kuunga kizazi, kumcha Mwenyezi Mungu na kusuluhisha kati ya watu. Nako ni iwapo mtaitwa kufanya lolote katika hayo, mkakataa na kutoa hoja kwamba mliapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa hamtalifanya. Bali ni juu ya Mwenye kuapa ageuze kiapo chake, afanye vitendo vya kheri na atoe kafara ya kiapo chake wala asizowee jambo hilo. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyasikia maneno yenu, ni Mwenye kuzijua hali zenu zote. info
التفاسير: