Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Abdullah Məhəmməd və Nasir Xamis.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
84 : 2

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَكُمۡ لَا تَسۡفِكُونَ دِمَآءَكُمۡ وَلَا تُخۡرِجُونَ أَنفُسَكُم مِّن دِيَٰرِكُمۡ ثُمَّ أَقۡرَرۡتُمۡ وَأَنتُمۡ تَشۡهَدُونَ

Na Kumbukeni, enyi Wana wa Isrāīl, tulipochukua kwenu ahadi ya mkazo katika Taurati ya kuharamisha umwagaji damu baina yenu, nyinyi kwa nyinyi, na kutoana majumbani nyinyi kwa nyinyi. Kisha mkakubali hilo na hali nyinyi mnashuhudia kuwa ni kweli. info
التفاسير:

external-link copy
85 : 2

ثُمَّ أَنتُمۡ هَٰٓؤُلَآءِ تَقۡتُلُونَ أَنفُسَكُمۡ وَتُخۡرِجُونَ فَرِيقٗا مِّنكُم مِّن دِيَٰرِهِمۡ تَظَٰهَرُونَ عَلَيۡهِم بِٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَإِن يَأۡتُوكُمۡ أُسَٰرَىٰ تُفَٰدُوهُمۡ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيۡكُمۡ إِخۡرَاجُهُمۡۚ أَفَتُؤۡمِنُونَ بِبَعۡضِ ٱلۡكِتَٰبِ وَتَكۡفُرُونَ بِبَعۡضٖۚ فَمَا جَزَآءُ مَن يَفۡعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمۡ إِلَّا خِزۡيٞ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰٓ أَشَدِّ ٱلۡعَذَابِۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Kisha nyinyi kwa nyinyi mnauana, baadhi yenu wanawaua wengine, na baadhi yenu wanawatoa wengine majumbani mwao; na kila kundi kati yenu linajitafutia nguvu kwa maadui dhidi ya ndugu zake kwa njia ya udhalimu na uonevu. Na mkijiwa nao, hao ndugu zenu, ni mateka kwenye mikono ya maadui, mnafanya haraka kuwakomboa kwa kulipa fidia, pamoja na kuwa imeharamishwa kwenu kuwatoa majumbani mwao. Ni ubaya ulioje mnaoufanya wa kuziamini baadhi ya hukumu za Taurati na kuzikanusha nyingine! Basi Malipo ya wanaoyafanaya hayo si mengine ila ni unyonge na fedheha ulimwenguni, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali sana ndani ya Moto. Na Mwenyezi Mungu si Mwenye kughafilika kwa mnayoyafanya. info
التفاسير:

external-link copy
86 : 2

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشۡتَرَوُاْ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا بِٱلۡأٓخِرَةِۖ فَلَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Hao ndio waliofadhilisha uhai wa ulimwenguni juu ya Akhera, basi hawatapunguziwa adhabu wala wao hawatakuwa na msaidizi wa kuwanusuru na adhabu ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
87 : 2

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَقَفَّيۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِۦ بِٱلرُّسُلِۖ وَءَاتَيۡنَا عِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَأَيَّدۡنَٰهُ بِرُوحِ ٱلۡقُدُسِۗ أَفَكُلَّمَا جَآءَكُمۡ رَسُولُۢ بِمَا لَا تَهۡوَىٰٓ أَنفُسُكُمُ ٱسۡتَكۡبَرۡتُمۡ فَفَرِيقٗا كَذَّبۡتُمۡ وَفَرِيقٗا تَقۡتُلُونَ

Hakika tulimpa Mūsā Taurati, na kuwaleta baada yake Mitume wengine miongoni mwa Wana wa Isrāīl. Na tulimpa ' Īsā mwana wa Maryam miujiza iliyo wazi na kumtilia nguvu kwa Jibrili, amani imshukie. Kwani nyinyi mumekuwa kila Mtume anapowajia na Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, usiolingana na matamanio yenu, mnamfanyia kiburi, wengine mkiwakanusha na wengine mkiwaua? info
التفاسير:

external-link copy
88 : 2

وَقَالُواْ قُلُوبُنَا غُلۡفُۢۚ بَل لَّعَنَهُمُ ٱللَّهُ بِكُفۡرِهِمۡ فَقَلِيلٗا مَّا يُؤۡمِنُونَ

Wana wa Isrāīl walisema kumwambia Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, “Nyoyo zetu zimezibwa kwa namna ambayo maneno yako hayapenyezi ndani yake.” Mambo si kama walivyodai. Bali nyonyo zao zimelaaniwa, zimepigwa muhuri juu ya hiyo laana. Na wao wamefukuzwa kutoka kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kukanusha kwao. Wao hawaamini isipokuwa imani chache isiyowafaa. info
التفاسير: