Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Abdullah Məhəmməd və Nasir Xamis.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
113 : 2

وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ لَيۡسَتِ ٱلنَّصَٰرَىٰ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَقَالَتِ ٱلنَّصَٰرَىٰ لَيۡسَتِ ٱلۡيَهُودُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَهُمۡ يَتۡلُونَ ٱلۡكِتَٰبَۗ كَذَٰلِكَ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ مِثۡلَ قَوۡلِهِمۡۚ فَٱللَّهُ يَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Na walisema Mayahudi, “Wanaswara hawako kwenye dini sahihi. Ndivyo hivyo kama walivyosema Wanaswara kuhusu Mayahudi, na hali wote wanasoma Taurati na Injili, ambapo ndani yake kuna ulazima wa kuwaamini Mitume wote. Hivyo ndivyo pia walivyosema wasiojua miongoni mwa washirikina: Waarabu na wengineo. Yaani, walisema kumwambia kila mwenye dini, “Wewe huko kwenye kitu chochote cha maana.” Basi Mwenyezi Mungu Ataamua baina yao Siku ya Kiyama katika yale mambo ya kidini waliotafautiana juu yake, na kumlipa kila mtu kwa matendo yake aliyoyafanya. info
التفاسير:

external-link copy
114 : 2

وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ أَن يُذۡكَرَ فِيهَا ٱسۡمُهُۥ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَآۚ أُوْلَٰٓئِكَ مَا كَانَ لَهُمۡ أَن يَدۡخُلُوهَآ إِلَّا خَآئِفِينَۚ لَهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا خِزۡيٞ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Hakuna dhalimu zaidi kuliko wale waliozuia kutajwa Mwenyezi Mungu katika msikiti, kama kusimamisha Swala na kusoma Qur’ani na mengine mfano wa hayo, na wakafanya bidii kuifanya magofu kwa kuivunja au kuifunga au kwa kuwazuia Waumini kuijia. Madhalimu hao haikuwa yapasa kwao kuingia hiyo msikiti isipokuwa wakiwa katika hali ya kuogopa na kutishika wasipate adhabu. Kwa matendo yao hayo, watakuwa na unyonge na fedheha ulimwenguni, na watakuwa na adhabu kali kesho Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
115 : 2

وَلِلَّهِ ٱلۡمَشۡرِقُ وَٱلۡمَغۡرِبُۚ فَأَيۡنَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجۡهُ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ

Zote pande mbili, upande wa kuchomoza jua na wa kutwa kwake na vilivyo baina yake, ni vya Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mmiliki wa ardhi yote. Basi pande wowote mnaouelekea kwenye Swala zenu kwa kuwa mmeamrishwa na Mwenyezi Mungu, Hakika nyinyi huwa mnaukusudia Uso Wake, hamkutoka kwenye ufalme Wake na utiifu wenu Kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye rehema za kuenea kwa waja Wake, ni Mjuzi wa vitendo vyao, hakuna chochote chenye kufichika Kwake Asikijue. info
التفاسير:

external-link copy
116 : 2

وَقَالُواْ ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ وَلَدٗاۗ سُبۡحَٰنَهُۥۖ بَل لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ كُلّٞ لَّهُۥ قَٰنِتُونَ

Na walisema Mayahudi na Wanaswara, “Mwenyezi Mungu Amejifanyia mtoto.” Ameepukana Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa pungufu ni Kwake, na neno hilo la batili! Kwani wote walioko mbinguni na ardhini ni milki Yake na ni watumwa Wake. Wote wanamnyenyekea Yeye na wanapelekewa wakiwa chini ya uendeshaji Wake. info
التفاسير:

external-link copy
117 : 2

بَدِيعُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَإِذَا قَضَىٰٓ أَمۡرٗا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ndiye Muumba mbingu na ardhi, bila ya kuwa na mfano uliotangulia. Na Anapolikadiri jambo na Akataka liwe, huliambia, “Kuwa,” likawa. info
التفاسير:

external-link copy
118 : 2

وَقَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ لَوۡلَا يُكَلِّمُنَا ٱللَّهُ أَوۡ تَأۡتِينَآ ءَايَةٞۗ كَذَٰلِكَ قَالَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِم مِّثۡلَ قَوۡلِهِمۡۘ تَشَٰبَهَتۡ قُلُوبُهُمۡۗ قَدۡ بَيَّنَّا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يُوقِنُونَ

Walisema wajinga miongoni mwa Watu wa Kitabu na wengineo kumwambia Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad, rehema na amani zimshukie, kwa njia ya inadi, “Si aseme na sisi Mwenyezi Mungu moja kwa moja Atuambie kwamba wewe ni Mtume Wake au itujie miujiza itokayo kwa Mwenyezi Mungu yenye kuonyesha ukweli wako.” Neno kama hili walilisema ummah waliopata kuwaambia Mitume wao, kwa njia ya ukaidi na ujeuri, kwa sababu ya kufanana nyoyo za waliotangulia na waliofuata katika ukafiri na upotevu. Hakika Tumezifafanua aya kwa wale wanaoamini Imani ya kikweli, kwa kumuamini kwao Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kuzifuata kwao Sheria Alizowawekea. info
التفاسير:

external-link copy
119 : 2

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ بَشِيرٗا وَنَذِيرٗاۖ وَلَا تُسۡـَٔلُ عَنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡجَحِيمِ

Sisi tumekutumiliza, ewe Mtume, kwa Dini ya haki iliyotiliwa nguvu kwa hoja na miujiza. Basi ifikishe kwa watu, pamoja na kuwapa Waumini bishara ya kheri ya dunia na ya Akhera, na kuwatisha wakaidi na adhabu ya Mwenyezi Mungu inayowangojea. Na baada ya kufikisha ujumbe, hutaulizwa juu ya ukafiri wa wenye kukukanusha. Wao wataingia Motoni, Siku ya Kiyama, wala hawatatoka humo. info
التفاسير: