Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Abdullah Məhəmməd və Nasir Xamis.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
77 : 2

أَوَلَا يَعۡلَمُونَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَ

Je, kwani wanafanya uhalifu wote huu na hali wao hawajui kuwa Mwenyezi Mungu Anayajua yote wanayoyaficha na kuyadhihirisha? info
التفاسير:

external-link copy
78 : 2

وَمِنۡهُمۡ أُمِّيُّونَ لَا يَعۡلَمُونَ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّآ أَمَانِيَّ وَإِنۡ هُمۡ إِلَّا يَظُنُّونَ

Na kati yao kuna watu wasiojua kusoma na kuandika, na wasioijua Taurati na yaliyomo ndani yake ya sifa za Nabii na Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na hawana chochote kuhusu hayo isipokuwa ni maneno ya urongo na dhana mbovu. info
التفاسير:

external-link copy
79 : 2

فَوَيۡلٞ لِّلَّذِينَ يَكۡتُبُونَ ٱلۡكِتَٰبَ بِأَيۡدِيهِمۡ ثُمَّ يَقُولُونَ هَٰذَا مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ لِيَشۡتَرُواْ بِهِۦ ثَمَنٗا قَلِيلٗاۖ فَوَيۡلٞ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتۡ أَيۡدِيهِمۡ وَوَيۡلٞ لَّهُم مِّمَّا يَكۡسِبُونَ

Maangamivu na onyo kali kwa wanavyuoni wa shari wa Kiyahudi ambao wanaandika kitabu kwa mikono yao kisha wanaosema, “Hiki kinatoka kwa Mwenyezi Mungu.” Nacho kinaenda kinyume na yale ambayo Mwenyezi Mungu Amemteremshia Nabii wake Mūsā rehema na amani zimshukie, ili wapokee, kwa kitendo hicho, manufaa ya ulimwenguni. Basi wao watapata mateso yenye kuangamiza kwa sababu ya kuuandika kwao ubatilifu huu kwa mikono yao, na watapata mateso yenye kuangamiza kwa sababu ya mali ya haramu wanayoyachukua kwa shughuli yao hiyo, kama hongo na mfano wake. info
التفاسير:

external-link copy
80 : 2

وَقَالُواْ لَن تَمَسَّنَا ٱلنَّارُ إِلَّآ أَيَّامٗا مَّعۡدُودَةٗۚ قُلۡ أَتَّخَذۡتُمۡ عِندَ ٱللَّهِ عَهۡدٗا فَلَن يُخۡلِفَ ٱللَّهُ عَهۡدَهُۥٓۖ أَمۡ تَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Walisema Wana wa Israili, “Moto hautupati huko Akhera isipokuwa kwa siku chache zinazohesabika.” Waambie, ewe Mtume, kwa kuyavunja madai yao, “Kwani nyinyi muna ahadi, kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ya jambo hilo? Mwenyezi Mungu Haendi kinyume ahadi yake. Lakini nyinyi munasema kuhusu Mwenyezi Mungu msiyoyajua kwa kuzua kwenu urongo.” info
التفاسير:

external-link copy
81 : 2

بَلَىٰۚ مَن كَسَبَ سَيِّئَةٗ وَأَحَٰطَتۡ بِهِۦ خَطِيٓـَٔتُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Hukumu ya Mwenyezi Mungu imethibiti kwamba mwenye kutenda makosa mpaka yakamtia ukafirini na madhambi yake yakamtawala yeye sehemu zake zote, na hali hii haiwi isipokuwa kwa mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, wote hao, washirikina na makafiri, ndio wenye kukaa Motoni makao ya milele yasiyokatika. info
التفاسير:

external-link copy
82 : 2

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Na hukumu ya Mwenyezi Mungu iliyothibiti, kwa upande mwengine, ni kwamba wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake imani ya kikweli iliyosafika na Wakafanya vitendo vinavyoambatana na Sheria ya Mwenyezi Mungu Aliyowapelekea Mitume Wake kwa njia ya Wahyi, hao watakaa Peponi makao ya milele yasiyokatika huko Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
83 : 2

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ لَا تَعۡبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَانٗا وَذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَقُولُواْ لِلنَّاسِ حُسۡنٗا وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ ثُمَّ تَوَلَّيۡتُمۡ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنكُمۡ وَأَنتُم مُّعۡرِضُونَ

Na Kumbukeni, enyi Wana wa Isrāīl, tulipochukua ahadi ya mkazo kwenu kwamba mtamuabudu Mwenyezi Mungu peke Yake Asiye na mshirika, muwafanyie wema wazazi wawili na watoto waliofiliwa na baba zao nao wako chini ya umri wa kubaleghe na masikini na kwamba muwaambie watu maneno mazuri, pamoja na kusimamisha Swala na kutoa Zaka. Kisha mkageuka na mkavunja ahadi, isipokuwa wachache katika nyinyi waliosimama imara juu yake. Na nyinyi bado mnaendelea kugeuka kwenu. info
التفاسير: