Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Ali Muhsin el-Beruani

Numri i faqes:close

external-link copy
94 : 9

يَعۡتَذِرُونَ إِلَيۡكُمۡ إِذَا رَجَعۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡۚ قُل لَّا تَعۡتَذِرُواْ لَن نُّؤۡمِنَ لَكُمۡ قَدۡ نَبَّأَنَا ٱللَّهُ مِنۡ أَخۡبَارِكُمۡۚ وَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمۡ وَرَسُولُهُۥ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

WATAKUTOLEENI UDHURU mtapo warudia. Sema: Msitoe udhuru; hatukuaminini. Mwenyezi Mungu amekwisha tueleza khabari zenu. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wataviona vitendo vyenu. Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa ya siri na ya dhaahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda. info

Enyi Waumini Mujaahidina! Hao walio bakia nyuma na wakafanya taksiri watakutoleeni udhuru mtapo rejea kutoka vitani na mkakutana nao. Ewe Mtume! Waambie: Msitoe udhuru, kwani hakika sisi hatukusadikini. Mwenyezi Mungu amekwisha bainisha wazi ukweli wa roho zenu, na amemfunulia Nabii wake baadhi ya uwongo wenu. Na baada ya hayo Mwenyezi Mungu na Mtume wake watavijua vitendo vyenu. Na mwisho wenu baada ya maisha ya duniani ni kuendea kwa Mwenyezi Mungu ambaye anayajua yaliyo fichikana na yanayo onekana wazi. Naye atakulipeni kwa mliyo kuwa mkiyatenda. Na atakulipeni kwa mnavyo stahiki.

التفاسير:

external-link copy
95 : 9

سَيَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمۡ إِذَا ٱنقَلَبۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡ لِتُعۡرِضُواْ عَنۡهُمۡۖ فَأَعۡرِضُواْ عَنۡهُمۡۖ إِنَّهُمۡ رِجۡسٞۖ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُ جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Watakuapieni kwa Mwenyezi Mungu mtakapo rudi kwao ili muwaachilie mbali. Basi waachilieni mbali. Hakika hao ni najsi, na makaazi yao ni Jahannamu, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyachuma. info

Watakuapieni kwa Mwenyezi Mungu pale mtapo rejea kwao, kwamba wao wanasema kweli katika kutoa udhuru wao, ili muwaridhie na kwa hivyo waghafilike na vitendo vyao. Basi msiwakubalie kwa lengo lao hilo. Bali watengeni na muwachukie, kwani wao wako daraja ya mwisho kabisa ya ukhabithi wa roho na ukafiri. Na mwisho wao ni Jahannamu, kuwa ndio adabu yao kwa madhambi na maasi walio yatenda!

التفاسير:

external-link copy
96 : 9

يَحۡلِفُونَ لَكُمۡ لِتَرۡضَوۡاْ عَنۡهُمۡۖ فَإِن تَرۡضَوۡاْ عَنۡهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَرۡضَىٰ عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Wanakuapieni ili muwe radhi nao. Basi hata mkiwa radhi nao nyiye, Mwenyezi Mungu hawi radhi na watu wapotofu. info

Wanakuapieni kwa tamaa ya kutaka muwe radhi nao. Hata mkakhadaika kwa viapo vyao na mkawaridhia, radhi zenu nyinyi peke yenu hazitowafaa, kwa sababu Mwenyezi Mungu amekasirika nao kwa upotovu wao na uasi wao kuipinga Dini!

التفاسير:

external-link copy
97 : 9

ٱلۡأَعۡرَابُ أَشَدُّ كُفۡرٗا وَنِفَاقٗا وَأَجۡدَرُ أَلَّا يَعۡلَمُواْ حُدُودَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Mabedui wamezidi sana katika ukafiri na unaafiki, na wameelekea zaidi kutojua mipaka ya aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. info

Mabedui, Waarabu wa majangwani, ndio wakubwa wa kuikataa Haki na wa unaafiki. Hao hakika wamefika upeo wa mwisho katika hayo. Na hayo ni hivyo kwa kuwa wao wapo mbali na maarifa na mwahali mwenye vitovu vya ilimu. Na wao ndio wameelekea zaidi kuwa wasiijue mipaka ya Mwenyezi Mungu, na aliyo mteremshia Mtume wake katika sharia na hukumu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa pande zote mbili, na ni Mwenye hikima katika malipo anayo yakadiria.

التفاسير:

external-link copy
98 : 9

وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغۡرَمٗا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ ٱلدَّوَآئِرَۚ عَلَيۡهِمۡ دَآئِرَةُ ٱلسَّوۡءِۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Na katika Mabedui hao wapo wanao fikiri kuwa wanayo yatoa ni gharama ya bure, na wanakungojeleeni mambo yakugeukieni. Mageuko maovu yatakuwa juu yao! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. info

Na baadhi ya hawa wanaafiki katika watu wa majangwani wanaona kuwa wanacho kitoa katika Sabiili-Llahi (Njia ya Mwenyezi Mungu) kuwa ni gharama na khasara ya bure, kwa kuwa vile hawaamini kuwa kuna malipo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nao wanataraji na wanangojea hali ya vita ikugeukieni nyinyi Waumini. Bali hayo mageuko yatawageukia wao! Na hiyo shari wanayo ingojea ikufikieni itawafika wao iwazunguke! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzisikia kauli zao, na Mwenye kuvijua vitendo vyao na niya zao, na madhambi wanayo yachuma.

التفاسير:

external-link copy
99 : 9

وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَٰتٍ عِندَ ٱللَّهِ وَصَلَوَٰتِ ٱلرَّسُولِۚ أَلَآ إِنَّهَا قُرۡبَةٞ لَّهُمۡۚ سَيُدۡخِلُهُمُ ٱللَّهُ فِي رَحۡمَتِهِۦٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na katika Mabedui wapo wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaitakidi kuwa wanayo yatoa ndiyo ya kuwasogeza kwa Mwenyezi Mungu na ya kuwapatia dua za Mtume. Naam! Hayo ni kweli mambo ya kuwasogeza. Mwenyezi Mungu atawaingiza katika rehema yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mwenye kurehemu. info

Wala si kama Mabedui wote ni hali hiyo. Wamo kati yao wanao muamini Mwenyezi Mungu, na wanaisadiki Siku ya Kiyama, na wanaitakidi kuwa kwa kutoa katika Njia ya Mwenyezi Mungu wanajikaribisha kwa Mwenyezi Mungu, na ni sababu ya Mtume s.a.w. kuwaombea wao, kwa kuwa yeye alikuwa akiwaombea kheri na baraka wale wanao toa sadaka. Na hayo bila ya shaka ni njia kubwa ya kuwakaribisha watu kwa Mwenyezi Mungu na kuwafikishia yale wayatakayo. Basi hakika Mwenyezi Mungu atawamiminia rehema yake, kwani Yeye ni Mwenye kusamehe madhambi, Mwenye kuwarehemu viumbe vyake.

التفاسير: