Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Ali Muhsin el-Beruani

Numri i faqes:close

external-link copy
12 : 7

قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسۡجُدَ إِذۡ أَمَرۡتُكَۖ قَالَ أَنَا۠ خَيۡرٞ مِّنۡهُ خَلَقۡتَنِي مِن نَّارٖ وَخَلَقۡتَهُۥ مِن طِينٖ

Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo info

Mwenyezi Mungu kwa kuudhika naye kwa uasi wake alimwambia: Nini kilicho kuzuia usimtukuze Adam, na hali Mimi nimekuamrisha ufanye hivyo? Iblisi akajibu kwa inda na kiburi: Mimi bora kuliko Adam. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo. Na moto ni mtukufu zaidi kuliko udongo.

التفاسير:

external-link copy
13 : 7

قَالَ فَٱهۡبِطۡ مِنۡهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَن تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَٱخۡرُجۡ إِنَّكَ مِنَ ٱلصَّٰغِرِينَ

Akasema: Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka! Hakika wewe u miongoni mwa walio duni. info

Mwenyezi Mungu alimlipa kwa inda yake na kiburi chake kwa kumfukuza katika makao ya utukufu wake, na akamwambia: Teremka kutoka hapo baada ya kuwa katika pahala pa juu. Haikufalii ukapandwa kichwa na ukaasi humo! Toka huko, nawe umehukumiwa hizaya na udhalili!

التفاسير:

external-link copy
14 : 7

قَالَ أَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ

Akasema: Nipe muhula mpaka siku watakapo fufuliwa. info

Iblisi akamwambia Mwenyezi Mungu: Nipe muhula, unibakishe mpaka Siku ya Kiyama.

التفاسير:

external-link copy
15 : 7

قَالَ إِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ

Akasema: Utakuwa miongoni mwa walio pewa muhula info

Mwenyezi Mungu akamjibu: Wewe utakuwa katika walio bakishwa wa mwisho.

التفاسير:

external-link copy
16 : 7

قَالَ فَبِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأَقۡعُدَنَّ لَهُمۡ صِرَٰطَكَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ

Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka. info

Kwa kumchukia Adam na kumhusudu alisema: Kwa sababu ya kunihukumia kupotoka na kupotea, nakuapia nitawapoteza wana wa Adam wasiifuate Njia yako Iliyo Nyooka, kwa kutumia kila hila zinazo mkinika.

التفاسير:

external-link copy
17 : 7

ثُمَّ لَأٓتِيَنَّهُم مِّنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيهِمۡ وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ وَعَنۡ أَيۡمَٰنِهِمۡ وَعَن شَمَآئِلِهِمۡۖ وَلَا تَجِدُ أَكۡثَرَهُمۡ شَٰكِرِينَ

Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani. info

Na ninaapa, nitawatokelea mbele yao, na nyuma yao, na kuliani kwao, na kushotoni kwao, na kila upande ninao weza, nikitafuta kila kipengee cha kughafilika kwao au udhaifu wao, nipate kuwapotosha, hata wasiwe wengi wao wanao kuamini Wewe, kwa kuto shukuru neema yako.

التفاسير:

external-link copy
18 : 7

قَالَ ٱخۡرُجۡ مِنۡهَا مَذۡءُومٗا مَّدۡحُورٗاۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنۡهُمۡ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمۡ أَجۡمَعِينَ

Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote info

Mwenyezi Mungu akazidi kuudhika, akamwambia: Toka kwenye makao ya ukarimu wangu, wewe ulio hizika kwa kiburi chako na uasi wako, na khatima yako ni kuhiliki tu! Na ninaapa nitaijaza Jahannamu kwa wewe na hao wana wa Adam watao kufuata nyote pamoja!

التفاسير:

external-link copy
19 : 7

وَيَٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ فَكُلَا مِنۡ حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii, na kuleni humo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, mkawa katika wale walio dhulumu info

Na ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika makao ya ukarimu wangu, nayo ndiyo hiyo Bustani, mneemeke humo, mkila kila chakula mpendacho, isipo kuwa mti huu. Msiukaribie! Msije mkawa wenye kujidhulumu nafsi zenu kwa adhabu itayo kupateni kwa kuvunja amri.

التفاسير:

external-link copy
20 : 7

فَوَسۡوَسَ لَهُمَا ٱلشَّيۡطَٰنُ لِيُبۡدِيَ لَهُمَا مَا وُۥرِيَ عَنۡهُمَا مِن سَوۡءَٰتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَىٰكُمَا رَبُّكُمَا عَنۡ هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةِ إِلَّآ أَن تَكُونَا مَلَكَيۡنِ أَوۡ تَكُونَا مِنَ ٱلۡخَٰلِدِينَ

Basi Shet'ani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizo fichiwa, na akasema: Mola Mlezi wenu hakukukatazeni mti huu ila msije mkawa Malaika, au msije mkawa katika wanao ishi milele. info

Shetani akawazaini waivunje amri ya Mwenyezi Mungu, ziwavuke nguo zilizo wasitiri zikashifike tupu zao. Akawaambia: Mola wenu Mlezi hakukukatazeni mti huu ila ni kwa kuwa hataki muwe Malaika, au msije mkawa mnaishi milele, na neema yenu haikatiki daima katika makao haya!

التفاسير:

external-link copy
21 : 7

وَقَاسَمَهُمَآ إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ ٱلنَّٰصِحِينَ

Naye akawaapia: Kwa yakini mimi ni miongoni wa wanao kunasihini. info

Naye akawaapia kuwa ati yeye ni katika wanao wapa nasaha njema, na akakariri kiapo chake.

التفاسير:

external-link copy
22 : 7

فَدَلَّىٰهُمَا بِغُرُورٖۚ فَلَمَّا ذَاقَا ٱلشَّجَرَةَ بَدَتۡ لَهُمَا سَوۡءَٰتُهُمَا وَطَفِقَا يَخۡصِفَانِ عَلَيۡهِمَا مِن وَرَقِ ٱلۡجَنَّةِۖ وَنَادَىٰهُمَا رَبُّهُمَآ أَلَمۡ أَنۡهَكُمَا عَن تِلۡكُمَا ٱلشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَآ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لَكُمَا عَدُوّٞ مُّبِينٞ

Basi akawateka kwa khadaa. Walipo uonja ule mti, tupu zao zilifichuka na wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao Mlezi akawaita: Je, sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet'ani ni adui yenu wa dhaahiri? info

Basi akawachochea kwa udanganyifu mpaka wakenda kula ule mti. Walipo uonja tupu zao zikafichuka, wakaingia wanakusanya majani ya miti kujisitiri tupu zao. Mola wao Mlezi akawakaripia, na akawatanabahisha makosa yao kwa kuwambia: Mimi sikukukatazeni mti ule, na nikakwambieni kuwa Shetani ni adui yenu wa dhaahiri, hakutakieni kheri?

التفاسير: