Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

Numéro de la page:close

external-link copy
54 : 10

وَلَوۡ أَنَّ لِكُلِّ نَفۡسٖ ظَلَمَتۡ مَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لَٱفۡتَدَتۡ بِهِۦۗ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۖ وَقُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na lau kwamba kila nafsi iliyomshirikisha na kumkanusha Mwenyezi Mungu itakuwa na vyote vilivyomo ardhini, na ikamkinika kuvifanya ni fidia yake ya kujikomboa na adhabu hiyo, ingalijikomboa kwavyo. Na wale ambao walidhulumu wataficha majuto yao watakapoiona adhabu ya Mwenyezi Mungu imewashukia wao wote. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Atahukumu baina yao kwa uadilifu, na wao hawatadhulumiwa, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Hamuadhibu yoyote isipokuwa kwa dhambi zake. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 10

أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ أَلَآ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Jua utanabahi kwamba kila kilichoko mbinguni na ardhini ni milki ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, hakuna kitu chochote kati ya hivyo ni cha yoyote isipokuwa Yeye. Jua utanabahi kwamba kukutana na Mwenyezi Mungu kuko na adhabu Yake kwa washirikina ni yenye kuwa, lakini wengi wao hawaujui uhakika wa hilo. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 10

هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kuhuisha na Mwenye kufisha, Hashindwi kuwahuisha watu baada ya kufa kwao, kama ambavyo hakumshindi Yeye kuwafisha Atakapo hilo. Na wao ni wenye kurejea Kwake baada ya kufa kwao. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 10

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَتۡكُم مَّوۡعِظَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَشِفَآءٞ لِّمَا فِي ٱلصُّدُورِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ

Enyi watu yamewajia nyinyi mawaidha kutoka kwa Mola wenu yanayowakumbusha mateso ya Mwenyezi Mungu na yanayowaonya makamio Yake, nayo ni Qur’ani na yale iliyoyakusanya ya miujiza na mawaidha ili kuzitengeneza tabia zenu na matendo yenu. Na ndani yake muna dawa ya yaliyomo nyoyoni ya ujinga na ushirikina na magonjwa mengineyo, na muna uongofu kwa viumbe wenye kuifuata iwaokoe na maangamivu. Mwanyezi mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Ameijaalia ni neema na rehema kwa Waumini. Na Amewahusu Waumini kwa hilo, kwa kuwa wao ndio wenye kunufaika na Imani. Ama makafiri, hiyo Qur’ani kwao ni giza. info
التفاسير:

external-link copy
58 : 10

قُلۡ بِفَضۡلِ ٱللَّهِ وَبِرَحۡمَتِهِۦ فَبِذَٰلِكَ فَلۡيَفۡرَحُواْ هُوَ خَيۡرٞ مِّمَّا يَجۡمَعُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu wote, «Kwa wema wa Mwenyezi Mungu na rehema Yake, basi na wawe na furaha.» Wema wa Mwenyezi mungu na rehema Yake ni Uislamu ambao ni uongofu na ni Dini ya haki aliyokuja nayo Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwani Uislamu ambao Mwenyezi Mungu Amewaita wao waufuate, na Qur’ani ambayo Aliiteremsha kwa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye ni bora kuliko taka za ulimwengu wanazozikusanya na anasa zilizomo ndani yake zenye kutoeka kuondoka. info
التفاسير:

external-link copy
59 : 10

قُلۡ أَرَءَيۡتُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ لَكُم مِّن رِّزۡقٖ فَجَعَلۡتُم مِّنۡهُ حَرَامٗا وَحَلَٰلٗا قُلۡ ءَآللَّهُ أَذِنَ لَكُمۡۖ أَمۡ عَلَى ٱللَّهِ تَفۡتَرُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wanaokataa wahyi, «Nipeni habari juu ya hii riziki ya wanyama, mimea na vitu vizuri ambavyo Mwenyezi Mungu Amewaumbia nyinyi, mkajihalalishia baadhi ya hivyo na mkajiharamishia vinginevyo.» Waambie, «Je, Mwenyezi Mungu Amewaruhusu hilo au mnaongea maneno ya ubatilifu ya kumzulia Mwenyezi Mungu na mnasema urongo?» Hakika wao wanaongea maneno ya ubatilifu ya kumzulia Mwenyezi Mungu na wanasema urongo. info
التفاسير:

external-link copy
60 : 10

وَمَا ظَنُّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَشۡكُرُونَ

Na hawa wanaomzulia Mwenyezi Mungu urongo, wakamnasibishia uharamishaji wa vitu ambavyo Yeye Hakuviharamisha kati ya riziki na vyakula, wanadhani kuwa Mwenyezi Mungu Atawafanya nini Siku ya Kiyama, siku ya wao kuhesabiwa, kwa urongo wao waliomzulia? Je,wanadhani kwamba Yeye Atawaacha na Atawasamehe? Mwenyezi Mungu Ana wema mwingi kwa viumbe Wake kwa kuacha Kwake kuyaharakisha mateso duniani kwa aliyemzulia urongo, na badala yake kumpa muhula. Lakini wengi zaidi wa watu hawamshukuru Mwenyezi Mungu kwa wema wake juu yao kwa hilo. info
التفاسير:

external-link copy
61 : 10

وَمَا تَكُونُ فِي شَأۡنٖ وَمَا تَتۡلُواْ مِنۡهُ مِن قُرۡءَانٖ وَلَا تَعۡمَلُونَ مِنۡ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيۡكُمۡ شُهُودًا إِذۡ تُفِيضُونَ فِيهِۚ وَمَا يَعۡزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثۡقَالِ ذَرَّةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِ وَلَآ أَصۡغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡبَرَ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٍ

Na huwi, ewe Mtume, kwenye jambo lolote katika mambo yako, na husomi chochote kile katika aya za Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na hafanyi yoyote katika ummah huu tendo lolote lema au baya, isipokuwa sisi huwa ni mashahidi juu yenu ni wenye kuliona hilo, mnapolichukua na kulitenda, tukawahifadhia na tukawalipa kwalo. Na haufichamani na ujuzi wa Mwenyezi Mungu uzito wa chungu mdogo ardhini wala mbinguni, wala kitu kidogo kabisa wala kikubwa kabisa, isipokuwa kiko kwenye Kitabu kilichoko kwa Mwenyezi Mungu kilicho waziwazi chenye ufafanuzi, ujuzi Wake umekizunguka na Kalamu Yake imekiandika. info
التفاسير: