Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

Numéro de la page:close

external-link copy
43 : 10

وَمِنۡهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيۡكَۚ أَفَأَنتَ تَهۡدِي ٱلۡعُمۡيَ وَلَوۡ كَانُواْ لَا يُبۡصِرُونَ

Na miongoni mwao kuna wanaokutazama wewe na dalili za unabii wako wa kweli, lakini wao hawaioni nuru ya Imani Aliyokupa Mwenyezi Mungu. Je, unaweza , ewe Mtume, kuwaumbia vipofu macho ya kuwafanya wao waongoke. Vilevile huwezi kuwaongoa wao iwapo hawana busara. Hakika yote hayo yako kwa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 10

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَظۡلِمُ ٱلنَّاسَ شَيۡـٔٗا وَلَٰكِنَّ ٱلنَّاسَ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ

Mwenyezi Mungu Hawadhulumu watu kitu chochote, kwa kuwaongezea makosa yao na kuwapunguzia mema yao, lakini watu ndio wanaojidhulumu nafsi zao kwa kukufuru, kuasi na kwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na makatazo Yake. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 10

وَيَوۡمَ يَحۡشُرُهُمۡ كَأَن لَّمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا سَاعَةٗ مِّنَ ٱلنَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيۡنَهُمۡۚ قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِلِقَآءِ ٱللَّهِ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ

Na siku Mwenyezi Mungu Atawakusanya washirikina hawa, Siku ya kufufuliwa na kuhesabiwa, kama kwamba wao kabla ya hapo hawakukaa katika maisha ya duniani isipokuwa kadiri ya muda mchache wa kipindi cha mchana, watajuana wao kwa wao kama walivyokuwa duniani, kisha kujuana huko kutakatika na muda huo utapita. Hakika wamepata hasara wale waliokataa na kukanusha kuwa watakutana na Mwenyezi Mungu na kuwa Ana thwabu na Ana adhabu. Na hawakuwa ni wenye kuafikiwa kupata uongofu katika yale waliyoyafanya. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 10

وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعۡضَ ٱلَّذِي نَعِدُهُمۡ أَوۡ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيۡنَا مَرۡجِعُهُمۡ ثُمَّ ٱللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ

Na iwapo tutakuonesha, ewe Mtume, katika uhai wako baadhi ya mateso tunayowaahidi duniani, au tukakufisha kabla hatujakuonesha hayo kwao, ni kwetu sisi peke yetu marejeo ya mambo yao katika hali zote mbili, kisha Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa vitendo vyao waliokuwa wakivifanya duniani, hakuna chochote kati ya hivyo kinafichika Kwake, na Atawalipa malipo yao wanayostahiki kwa vitendo vyao hivyo. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 10

وَلِكُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولٞۖ فَإِذَا جَآءَ رَسُولُهُمۡ قُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na kila ummah uliopita kabla yenu, enyti watu, ulikuwa na mjumbe niliyemtuma kwao, kama nilivyomtuma Muhammad kwenu Alinganie kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu na kuwa na utiifu Kwake. Basi huyo mjumbe wao atakapokuja Akhera, hapo kutaamuliwa baina yao kwa uadilifu, na wao hawatadhulumiwa katika malipo ya matendo yao chochote. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 10

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡوَعۡدُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na washirikina katika watu wako, ewe Mtume, wanasema, «Ni lini kitasimama Kiyama iwapo wewe na waliokufuata ni miongoni mwa wakweli katika yale mnayotuahidi kwayo?» info
التفاسير:

external-link copy
49 : 10

قُل لَّآ أَمۡلِكُ لِنَفۡسِي ضَرّٗا وَلَا نَفۡعًا إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۗ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌۚ إِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ فَلَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ

Waambie, ewe Mtume, «Siwezi kuiepushia nafsi yangu madhara wala kuiletea manufaa isipokuwa Akiwa Mwenyezi Mungu Ametaka kuniepushia madhara au kuniletea manufaa. Kila watu wana wakati wa kumalizika muda wao na kipindi chao cha kuishi, basi ujapo wakati wa kumalizika kipindi chao cha kuishi na kukoma umri wao, hawatachelewa hata kwa muhula wa saa moja wala hautatangulia muda wa maisha yao mbele ya wakati maalumu. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 10

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُهُۥ بَيَٰتًا أَوۡ نَهَارٗا مَّاذَا يَسۡتَعۡجِلُ مِنۡهُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Nipeni habari ikiwajia adhabu ya Mwenyezi Mungu mchana au usiku, ni kitu gani mnachokifanyia haraka, enyi wahalifu, kuwa adhabu iteremke? info
التفاسير:

external-link copy
51 : 10

أَثُمَّ إِذَا مَا وَقَعَ ءَامَنتُم بِهِۦٓۚ ءَآلۡـَٰٔنَ وَقَدۡ كُنتُم بِهِۦ تَسۡتَعۡجِلُونَ

Je, baada ya kushuka adhabu ya Mwenyezi Mungu kwenu, enyi washirikina, ndipo mtaamini, wakati ambapo Imani haitawafaa? Wakati huo mtaambiwa, ‘Je, sasa ndipo mnaamini na hapo nyuma mlikuwa mnaifanyia haraka?’» info
التفاسير:

external-link copy
52 : 10

ثُمَّ قِيلَ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ ذُوقُواْ عَذَابَ ٱلۡخُلۡدِ هَلۡ تُجۡزَوۡنَ إِلَّا بِمَا كُنتُمۡ تَكۡسِبُونَ

Kisha wataambiwa waliozidhulumu nafsi zao kwa kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu, «Onjeni adhabu ya Mwenyezi Mungu ya daima milele kwenu, kwani mnateswa isipokuwa ni kwa yale matendo ya kumuasi Mwenyezi Mungu mliokuwa mkiyafanya katika maisha yenu. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 10

۞ وَيَسۡتَنۢبِـُٔونَكَ أَحَقٌّ هُوَۖ قُلۡ إِي وَرَبِّيٓ إِنَّهُۥ لَحَقّٞۖ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ

Na hao washirikina miongoni mwa watu wako, ewe Mtume, wanataka uwape habari kuhusu adhabu Siku ya Kiyama, «Je, ni kweli hiyo? Waambie, ewe Mtume, «Ndio, naapa kwa Mola wangu, hiyo ni kweli isiokuwa na shaka.Na nyinyi si wenye kumlemea Mwenyezi Mungu Asiwafufue na kuwalipa, kwani nyinyi muko kwenye udhibiti wa Mwenyezi Mungu na mamlaka Yake. info
التفاسير: